Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Watu wasiopungua kumi wameripotiwa kuuwawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Arusha Tanzania, kwenye makabiliano baina ya Polisi na wafuasi wa chama cha upinzani cha CHADEMA.

Ghasia zilianza baada ya Polisi kumkamata mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema, wakiwa wanaelekea kuhutubia mkutano wa kisiasa.

Baadaye polisi pia walimkamata aliyekuwa mgombea wa chama hicho cha CHADEMA kwenye uchaguzi wa Urais uliofanyika mwezi Oktoba Dr Wilbroad Slaa.

Taarifa zinasema biashara kadhaa zilichomwa moto kwenye vurugu hizo.

Kwa mujibu wa waandishi wa habari mjini Arusha, Polisi walikuwa wamewakataza viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao kufanya maandamanao kabla ya mkutano wa kisiasa wa Jumatano, lakini mamia ya wafuasi wa chama hicho wakawafuata viongozi hao walipokuwa wanaelekea eneo la mkutano.

Bwana Slaa amenukuliwa akisema maandamano hayo yalikuwa ya kupinga ufisadi katika serikali mpya ya Rais Jakaya Kikwete.

Polisi walifyatua risasi hewani mara kadhaa kutoa tahadhari kwa maelfu ya wafuasi waliokwenda kutaka viongozi wao waachiwe huru, na baadaye wakafyatua gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya.

Walioshuhudia wanasema Polisi waliendelea kufyatua risasi mchana kutwa, huku wafuasi wa CHADEMA wakiendelea kukabiliana na askari Polisi katika maeneo mbali mbali ya mji wa Arusha.

Kwenye mkutano huo wa kisiasa, Dr Slaa aliwataka Polisi kumwachilia huru Bwana Mbowe na wengine, na pia akamtaka Rais Kikwete kujiuzulu.

Hadi kufikia Jumatano jioni hakuna taarifa iliyokuwa imetolewa na serikali kuhusu mzozo huo.

Kumekuwa na mvutano wa kisiasa nchini Tanzania tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Urais ambao vyama vya upinzani vinadai ulikuwa na udanganyifu.

Kufuatia uchaguzi huo shinikizo zinaendelea za kutaka Tanzania iwe na katiba mpya tofauti na iliyopo sasa, ambayo hairuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais kupingwa mahakamani yanapotangazwa na tume ya uchaguzi.

gonga hapaaaa bbc:BBC Swahili - Habari - 10 wauwawa kwenye ghasia mjini Arusha
 
Waliandamana CUF mkawabeza. WAHUNI WALE WAVAA BUIBUI NA VIBALAGHASHIA. waliuawa watu wengi kule pemba mkazidi kubeza. Leo mnasema CUF ni CCM-B. Mlisahau historia ya mapambano na DIRA ya siasa na uzalendo wa kitaifa. Aliwahi kuvunjwa mkono Profesa wa UCHUMI mkabeza eti Profesa uchwara. SASA ONJENI SHUBIRI HIYO NA MJUE SERIKALI IPO. NGOMA IKILIA SANA MWISHOWE HUPASUKA.
Sifurahii ila nakumbushia!! viva Dr. Slaa dr wa ukweli
 
poeni wafiwa wote na Mungu aturehemu watz na kutuepusha na kikombe hiki. amina
 
Aisee nimesikia bbc network Africa ya saa tatu usiku kuwa watu zaidi ya 10 wameuawa kwa risasi za moto.

Mwenye habari zaidi atupe wana JF

Mauaji haya yametokea wapi Mkuu? Arusha?

Aisee nimesikia bbc network Africa ya saa tatu usiku kuwa watu zaidi ya 10 wameuawa kwa risasi za moto.

Mwenye habari zaidi atupe wana JF

10 wauwawa kwenye ghasia mjini Arusha

Dr Wilbroad Slaa naye pia amekamatwa

Watu wasiopungua kumi wameripotiwa kuuwawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Arusha Tanzania, kwenye makabiliano baina ya Polisi na wafuasi wa chama cha upinzani cha CHADEMA.

Ghasia zilianza baada ya Polisi kumkamata mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema, wakiwa wanaelekea kuhutubia mkutano wa kisiasa.

Baadaye polisi pia walimkamata aliyekuwa mgombea wa chama hicho cha CHADEMA kwenye uchaguzi wa Urais uliofanyika mwezi Oktoba Dr Wilbroad Slaa.

Taarifa zinasema biashara kadhaa zilichomwa moto kwenye vurugu hizo.

Kwa mujibu wa waandishi wa habari mjini Arusha, Polisi walikuwa wamewakataza viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao kufanya maandamanao kabla ya mkutano wa kisiasa wa Jumatano, lakini mamia ya wafuasi wa chama hicho wakawafuata viongozi hao walipokuwa wanaelekea eneo la mkutano.

Bwana Slaa amenukuliwa akisema maandamano hayo yalikuwa ya kupinga ufisadi katika serikali mpya ya Rais Jakaya Kikwete.

Polisi walifyatua risasi hewani mara kadhaa kutoa tahadhari kwa maelfu ya wafuasi waliokwenda kutaka viongozi wao waachiwe huru, na baadaye wakafyatua gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya.

Walioshuhudia wanasema Polisi waliendelea kufyatua risasi mchana kutwa, huku wafuasi wa CHADEMA wakiendelea kukabiliana na askari Polisi katika maeneo mbali mbali ya mji wa Arusha.

Kwenye mkutano huo wa kisiasa, Dr Slaa aliwataka Polisi kumwachilia huru Bwana Mbowe na wengine, na pia akamtaka Rais Kikwete kujiuzulu.

Hadi kufikia Jumatano jioni hakuna taarifa iliyokuwa imetolewa na serikali kuhusu mzozo huo.

Kumekuwa na mvutano wa kisiasa nchini Tanzania tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Urais ambao vyama vya upinzani vinadai ulikuwa na udanganyifu.

Kufuatia uchaguzi huo shinikizo zinaendelea za kutaka Tanzania iwe na katiba mpya tofauti na iliyopo sasa, ambayo hairuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais kupingwa mahakamani yanapotangazwa na tume ya uchaguzi.
source. BBC Swahili - Habari - 10 wauwawa kwenye ghasia mjini Arusha
 
Arusha kukataa maonyo ya Lowasa kuwa ccm na chadema wakae pamoja ili kuzuia umwagaji damu ndiyo hayo. Tatizo ccm hawa ni vipofu, wamelewa madaraka miaka 50 ya utawala. Sasa mtauambiaje ulimwengu baada ya polisi kuuwa wananchi bila makosa? Jirudini haraka mkae kwenye meza ya mazungumzo la sivyo lililotukia Arusha litaenea nchi nzima.
 
Waliandamana CUF mkawabeza. WAHUNI WALE WAVAA BUIBUI NA VIBALAGHASHIA. waliuawa watu wengi kule pemba mkazidi kubeza. Leo mnasema CUF ni CCM-B. Mlisahau historia ya mapambano na DIRA ya siasa na uzalendo wa kitaifa. Aliwahi kuvunjwa mkono Profesa wa UCHUMI mkabeza eti Profesa uchwara. SASA ONJENI SHUBIRI HIYO NA MJUE SERIKALI IPO. NGOMA IKILIA SANA MWISHOWE HUPASUKA.
Sifurahii ila nakumbushia!! viva Dr. Slaa dr wa ukweli

Ndugu,

sidhani kama ni lazima katika kila jambo iwe ni kulinganisha CUF na CHADEMA, hapa tunazungumzia watanganyika zaidi ya 10 waliodhulumiwa haki yao ya kuishi ili kupisha matakwa ya watawala kuona kila kitu kinatokea kama watakavyo wao hata kama itagharimu maisha ya watu. Kweli ilitokea visiwani na kila mmoja anajua. Sidhani inatosha kuhalalisha mauwaji haya ati tu kwakua na visiwani wakiongozwa na cuf ilisha tokea.

Ndugu zangu tutiane shime. Moto waliouwasha Arusha hautazimika kamwe, bravo Mbowe, Lema na Silaa, ukombozi unagharama zake na sasa tunakuja, watatuua ila hatutaisha, watatuua wakitumaliza tutaishi tena labda watutokomeze na vizazi pamoja na wake na watoto wao, maana nao ni makamanda ktk haya mapambano.

Nguvu ya uma ni nguvu kuu kuliko dola, mabomu na mitutu...hakuna kulala mpaka kieleweke
 
Matokeo ya kuzuia maandamano tunayaona na matokeo ya kukubali maandamano tumeyaona, na tumeshajua fujo ni matokeo ya kuzuia maandamano,maandamano ya TZ ni kupongeza tu si kukosoa! In the end someone will be held responsible for the innocent blood
 
Poleni sana wafiwa. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.
 
poleni wana Arusha, huu ni mkosi kwa JK na siri...kali yake, saikolojia ya kiumbe hai anayeitwa binadamu inasema huwezi kumnyamazisha binadamu anapotaka kuongea au anapotafuta unafuu kutokana na ukandamizaji kwa kumuua binadamu mwenzie ili iwe mfano au kumuudhibu, bali kwa kumshawishi kisaikolojia na kumpatia haki yake ndiyo njia sahihi ya kutatua tatizo, hili linadhihirishwa na filamu kama escape from sobibo.
 
Wana JF, kwanza niwatakieni Heri za Mwaka Mpya, na Tumshukuru Mungu kwa kutupa another chance ya kuuona mwaka 2011. Lakini sielewi kama kweli Watanzania tunafahamu maana ya kupewa another chance ya kuuona mwaka 2010.

Habari hii ya Arusha, kwa kweli imeshtua sana, na nimejaribu kuifuatilia ktk vyombo vya habari vya hapa nchini, vingi vimekuwa havina taarifa ya wazi ya mauaji hayo. Ingawa kwa hali ilivyo, sintashangaa kuwa kuna watu zaidi ya hao ambao wameshapoteza maisha yao.

My take: Nimesha wahi kusema ktk moja ya thread zangu huko nyuma kuwa, watu walio na madaraka kwa sasa wawe waangalifu ktk maamuzi yao, kwani historia itakuja kuwahukumu. Kwa hayo yaliyotokea Arusha leo, kama ni ya kweli, basi tayari viongozi hao limesha wa cost. Damu ya raia wema, wanaodai haki yao, pale imwagikapo, hata kama ni mtu mmoja tu, damu hiyo itawalilia siku zote. Sasa tunasikia ni zaidi ya kumi, ukweli si bure. Nionavyo mimi, hali hii itaamsha mambo mapya ya kutokuelewana baina ya watanzani wa vyama tofauti, kama ilivyokuwa Zanzibar miaka kadhaa iliyopita. Ukiangalia kwa makini, hatua zilele ilizopita Zanzibar, ndio Bara tunakoelekea. Kwa vile wameamua hivyo kwa maslahi yao, basi hakuna budi hali hii kutokea. Ila cha msingi ni kuwa, siku zote Nguvu ya Umma hushinda.
 
Aisee nimesikia bbc network Africa ya saa tatu usiku kuwa watu zaidi ya 10 wameuawa kwa risasi za moto.

Mwenye habari zaidi atupe wana JF

kwa habari niliyo pata ni Police wawili na Raia 3 inakuwa watano(5) na Jengo la Salimu ally nyuma ya St. Thomasi Hospital ndio liliungua ambako ni floor ya kwanza ambako wanasema kuwa kuna furniture ila haijajulikana kama ni raia ndio walichoma moto au Police katika kurusha rusha madude yao ndio kulisababisha kuwaka moto na kuvunjika viooooo?

Twende mbele turudi nyuma Police ndio chanzo cha vurugu kama raia wailisha tembea zaidi ya Km2 na hakujatokea vurugu na waandamanaji walikuwa wamebakiza kama Km 5 kufika viwanja vya NMC kanin police msihakikishe wamefika salama na kuahakikisha mkutano wao umekwishaa.

Said Mwema yeye akae mkao wa kujua ipo siku The Hague inamuhusu kwanini waliwahaidi watakuwa na maandamano na ghafla usiku anasema hakuna maandamano kwa sababu za ki intelligencer kivipi leo Police wakutanapo na raia wakiandamana ndio kuwe na machafuko na kusema hakuna usalama mbona wao wameshindwa kugundua wizi wa mabenki kama kweli wao wanadhani kwa security wise wako fit??? ni waoongo police kabisa Mwema hajui intelligence yy ni kufuata order toka IKULU yaaani ni upuuzi mtu dalili ya fujo haikuwepo kabisa ila utaratibu wa police huwa ni mubovu kabisa tumeona dar.

Hizi ni habari za kutia simanzi sana'CCM na serekali yake wanaipeleka wapi hii Nchi?
 
Ndugu,

sidhani kama ni lazima katika kila jambo iwe ni kulinganisha CUF na CHADEMA, hapa tunazungumzia watanganyika zaidi ya 10 waliodhulumiwa haki yao ya kuishi ili kupisha matakwa ya watawala kuona kila kitu kinatokea kama watakavyo wao hata kama itagharimu maisha ya watu. Kweli ilitokea visiwani na kila mmoja anajua. Sidhani inatosha kuhalalisha mauwaji haya ati tu kwakua na visiwani wakiongozwa na cuf ilisha tokea.

Ndugu zangu tutiane shime. Moto waliouwasha Arusha hautazimika kamwe, bravo Mbowe, Lema na Silaa, ukombozi unagharama zake na sasa tunakuja, watatuua ila hatutaisha, watatuua wakitumaliza tutaishi tena labda watutokomeze na vizazi pamoja na wake na watoto wao, maana nao ni makamanda ktk haya mapambano.

Nguvu ya uma ni nguvu kuu kuliko dola, mabomu na mitutu...hakuna kulala mpaka kieleweke

CCM waliua Zanzibar, waliua Mwembechai, wamekua wakiendela kuua mtu mmoja mmoja kwa visingizio mbalimbali - Kombe, wafanyabiashara wa madini, mataxi drivers, leo watanzania wa Arusha; wataendelea kuua mpaka lini, wanataka waue mpaka wangapi ndiyo waridhike? Huko ambako tunasikia watu wana vita, wanauana kila siku, siyo kwamba wanapenda kufa, bali dhuluma na ukatili kama huu vinakuwa vimefikia mwisho wa kuvumiliwa. Mtanzania yeyote, awe CCM, CUF, CHADEMA, ; NCCR, TLP, NRA, n.k; wana haki ya kuishi, na kumwua yeyote ni kuwaua watanzania, utawala wa namna hiyo usikubalike kamwe.
 
Arusha kukataa maonyo ya Lowasa kuwa ccm na chadema wakae pamoja ili kuzuia umwagaji damu ndiyo hayo. Tatizo ccm hawa ni vipofu, wamelewa madaraka miaka 50 ya utawala. Sasa mtauambiaje ulimwengu baada ya polisi kuuwa wananchi bila makosa? Jirudini haraka mkae kwenye meza ya mazungumzo la sivyo lililotukia Arusha litaenea nchi nzima.

Mbaya zaidi kuna watu humo ndani ya CCM sijui wao hili haliwaumi au wanadhani ndio poaaaaa??? wajua wafanya biashara wengi walichanga pesa na kumsaidia batilda kwenye kampeni na cha ajabu wengi wa wafanyabiashara waliigeuka CCM na kuipigia CHADEMA, Kamanda Mateo hakukubaliana na kupindishwa kwa matokeo kwani alijua fika ile ilikuwa ni kura ya wananchi na kuipinga ni kumwaga dama leo huyo RPC aliye pelekwa Arusha sijui anafanya makusudi akidhani atakuwa IGP akumbuke watu wako kwenye mchakato wa katiba hili litamkuta tuuu aombe kufa mapema tuu.

Na habari nilizo zipata toka kwa mdau mmoja arusha anasema kuna bomu la machozi lilipigwa yapata saa kumi na moja na karibu na New Arusha Hotel na kufanya watu huko Hotelini kuhamia nje upande wa assembly kwani moshi w bomu la machozi ulitinga ndani ya jengo hilo hii yote ni tiali kulihalibu biashara ya hiyo Hotel na kwa ulimwengu kwani sindio nyie Mwaiita Arusha kama Geneva of Africa.

Kumbukeni Fujo kubwa ndani ya nchi hii lazima tuu itaaanzia huko Kanda ya kaskazini kwani watu wa kule hawana dogo wale kuna mchnganyiko na wameru mmhhhh
 
CCM waliua Zanzibar, waliua Mwembechai, wamekua wakiendela kuua mtu mmoja mmoja kwa visingizio mbalimbali - Kombe, wafanyabiashara wa madini, mataxi drivers, leo watanzania wa Arusha; wataendelea kuua mpaka lini, wanataka waue mpaka wangapi ndiyo waridhike? Huko ambako tunasikia watu wana vita, wanauana kila siku, siyo kwamba wanapenda kufa, bali dhuluma na ukatili kama huu vinakuwa vimefikia mwisho wa kuvumiliwa. Mtanzania yeyote, awe CCM, CUF, CHADEMA, ; NCCR, TLP, NRA, n.k; wana haki ya kuishi, na kumwua yeyote ni kuwaua watanzania, utawala wa namna hiyo usikubalike kamwe.

Safi sana ulichokisema ndio maana hii nchi inatawaliwa au inaongozwa na watu au kundi la watu wachache sana kwani hata nasikia ule uchaguzi wa mayor Arusha kuna baadhi ya viongozi wa juu CCM hawajapendezwa na hilo esp mawaziri na hata EL ambaye anasemwa vibaya na watu aliongea point na kusema CCM na CDM wakae waongelee swala hilo nashangaa sana Mayor aliye chaguliwa nae bado analidhia uchaguzi huwa ulio mweka kuwa Mayor wa Arusha hawa watu huwa hawana familia zao zika washauli au ni njaaaa hizo

Back
Top Bottom