Ya Bandari, Rasilimali za Taifa, Umasikini na Rushwa: Je, sisi ni Taifa huru? Aina tatu za uhuru

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Asalam,
bado naendelea kujiuliza uliza, je tuna uhuru wa aina gani? je jirani yangu yuko huru? je Mzee Mwanakijiji yuko huru? Je FaizaFox Yuko huru? na Mzee Paschal Mayala yuko Huru? Vipi Mamdenyi na Esta hapa?

Uhuru wa Kisiasa

Uhuru wa kisiasa ni uhuru ambao watu binafsi wanao kushiriki katika michakato ya kisiasa, kutoa maoni yao, na kushiriki katika shughuli za kisiasa bila shuruti au ushawishi usiofaa. Inajumuisha haki kama vile uhuru wa kujieleza, uhuru wa kukusanyika, uhuru wa vyombo vya habari, na haki ya kupiga kura. Uhuru wa kisiasa unahakikisha kwamba watu binafsi wanaweza kuwa na sauti katika michakato ya utawala na maamuzi ya jamii zao. Uhuru huu unahusu ulinzi na usimamizi wa rasilimali za taifa.

Uhuru wa Kibinafsi

Uhuru wa kibinafsi, unaojulikana pia kama uhuru wa mtu binafsi, unazingatia uhuru na uamuzi wa mtu binafsi katika nyanja mbalimbali za maisha yao. Inahusisha uwezo wa kufanya maamuzi na kufuata malengo na maslahi ya mtu mwenyewe, mradi tu hayakiuki haki na uhuru wa wengine. Uhuru wa kibinafsi unahusu uhuru wa kufikiri, kiuchumi, uwezo wa kununua na kupata huduma mbali mbali, uwezo kwenda unapotaka.

Uhuru wa Bendera

Huu hata hauna maelezo mengi. Ni ule wa kushusha bendera hii na kupandisha nyingine. Ni uhuru pia, na kuna watu hapa duniani wanasherehekea huo uhuru. Usicheke, tafakari.

Sasa tuchunguze

Je tuko huru kisiasa?


Kwenye uhuru wa kisiasa yako mengi bado ya kufanya, suala la mtu anaitwa mkoloni kuondoka ni jambo moja na pia kaondokaje? Kimwili? Au na mipango yake? Kama tunasema Mwingireza aliondoka na tunamfuata tena kwake kwa mkopo si bora tungemuacha hapa hapa tu? Tuna kauli juu ya rasilimali za Taifa?

Je tuna uhuru binafsi

Watanzania wangapi wana uwezo wa kununua bidhaa muhimu kwa Maisha yao? Wangapi wanauwezo wa kujitibia maradhi yao kwa uhakika hata kama ni kwa bima mfano? Wangapi wanaweza kuchagua namna bora ya usafiri wanapotoka sehemu A kwenda sehemu B? wangapi wanakauwezo japo ka kula mlo kamili mmoja kwa siku?

Uhuru wa bendera

Je huu ndio unaotuhusu ?

Tuendelee kujiuliza
 
Asalam,
bado naendelea kujiuliza uliza, je tuna uhuru wa aina gani? je jirani yangu yuko huru? je Mzee Mwanakijiji yuko huru? Je FaizaFox Yuko huru? na Mzee Paschal Mayala yuko Huru? Vipi Mamdenyi na Esta hapa?
Tuko huru kwa upande wa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, freedom of expression ndio maana kila uchao, tuna tiririka humu.
P
 
Back
Top Bottom