Kimwili tuko katika ardhi huru ya Tanzania, kifikra tuko utumwani Ulaya

Jelavic

Senior Member
Dec 28, 2016
180
380
KIMWILI TUKO KATIKA ARDHI HURU YA TANZANIA, KIFIKRA TUKO UTUMWANI ULAYA.

Siku ya leo miaka 62 iliyopita ardhi yetu ya Tanzania ilitambulika rasmi kama ardhi huru.

Kwajitihada za wazee wetu ambao pengine baada uhuru hawakujulikana sana.

Lakin swali la kujiuliza, Ardhi imekuwa huru sio mali tena ya Taifa la mwingereza lakin je watu wake wako huru..?.

Mifano kadhaa itupe mwanga.

Mtu anaikataa rangi yake nzuri nyeusi anakesha kwenye make up na kujichubua yaani anaona mweupe ni bora kuliko yeye je yuko huru..?

Mtu anakataa nywele zake tena nzuri za asili anaenda kujifunga nywele za bandia, anaamini kuwa nywele zetu hizi fupi ni mbaya, je yuko huru..?

Mtu anakataa kope za macho yake sababu ni fupi anaweka kope ndefu za bandia je yupo huru..?

Usizungumzie kucha za mikono na miguu na maumbile ya mwili kwa ujumla ili tu tufanane na wale tuliowakataa waondoke je tunajivunia uhuru upi..?

wakijografia tu au wa nyanja zote za kimaisha..?

haya yote ni sababu ya utumwa wa kifikra, tunawaza zaidi uzungu na umagharibi, ilihali ukoloni wa kijografia ni mbaya zaidi kuliko utumwa wa kifra.

wazee wetu walikuwa watumwa wakijografia wakapigania ardhi yao iwe huru lakin hawakuwa watumwa wakifikra, lakin tumeachiwa ardhi yetu tuishi bila kuingiliwa utaratibu wetu wakawaida wa maisha ila tumejikuta tumeingia kwenye utumwa mwingine wa kifikra, tumekuwa tunaishi katika ardhi tuliopata uhuru kimwili lakin tuko bado huko ulaya utumwani kifikra.

Tumekataa rangi zetu, tumekataa nywele zetu, tumekataa kucha zetu,tumekataa miili yetu, tumekataa mpaka lugha yetu kila baada ya maneno mawili la tatu kingereza, tumebakia huru kwenye nini.?

Kama tunapenda kuwa huru na kufurahia uhuru wetu tujivunie uasili wetu , tusiharibu asili tuliyoumbwa nayo kwa sababu ya kuiga vitu VIBAYA.
Kuhifadhi akili dhidi ya fikra mbovu ni moja ya kufurahia uhuru, tuutumie vizuri uhuru wetu.

9.Dec.2023
 
Hapana hicho sio kigezo cha kua utumwani au kua huru, watu wana choice and preference..........unge ongelea masuala muhimu ya Elimu, afya makazi demokurasia, mimi ninge kuelewa zaidi.......nchi yetu iko standstill tangu tupate uhuru Nyerere alitujengea msingi mbomvu wa ujamaa watu hawahitambui kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom