Msimamo wa CCM kwa rasilimali za Taifa ni upi?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Kwa mujibu wa katiba ya JMT suala la rasilimali za Taifa limejengewa wigo mpana wa ulinzi wake kupitia ibara ya
27.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Jamhuri ya Muungano, mali ya mamlaka ya nchi, mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuheshimu mali ya mtu mwingine.

(2) Watu wote watatakiwa kisheria kulinda mali ya mamlaka ya nchi na mali zote zinazomilikiwa kwa pamoja na wananchi, kupambana na aina zote za ubadhirifu na ubadhirifu, na kusimamia uchumi wa taifa kwa umakini na mtazamo wa watu mabwana wa hatima yaotaifa.

Kwa msingi wa ibara hizi utaona kuwa jukumu la ulinzi wa rasilimali za Taifa ni la kila mwananchi,japo msingi wa ulinzi kwa Sasa kwa rasilimali hizi ni utashi wa kiongozi aliyeko madarakani bila kujali wala kuzingatia mamlaka ya kisheria.

Sakata la bandari na mikataba funganizi inayoingiwa na serikali mbali na kukiuka katiba ya JMT Ina ligawa Taifa katika misingi ya watawaliwa na watawala katika muktadha mzima mamlaka ya wananchi.

Ikiwa mamlaka na madaraka ya SERIKALI yatatoka kwa wananchi iweje Leo aliyepewa madaraka hayo ayatumie kama fimbo ya kuwatisha WALIOTOA madaraka hayo pale wanapolinda rasilimali za Taifa.

Kuwatisha wakosoaji ambao jukumu la ulinzi wa rasilimali za Taifa ni lao ni kupingana na katiba ambayo mbali na kumuweka Rais aliyeko madarakani lakini ndiyo inayotambua mamlaka ya ulinzi wa rasilimali hizo.

Mbali na ukiukwaji wa katiba unafanywa na serikali,serikali ya CCM kupitia watawala wake imeleta sintofahamu katika ujinga wa kutoielewa katiba. Pia inazua maswali yasiyo na majibu na kuchochea madai ya katiba mpya kwa kipindi hiki kuliko wakati wowote ule.

Tumeona utaofauti Mkubwa wa Rais anayechaguliwa na wananchi kwa kura kwa mujibu wa katiba na Rais anayepatikana kwa takwa la katiba bila kupigiwa kura.

Hii inasababisha kuzua tofauti za uwazi kiutendaji mbali na kuwatumikia wananchi na uwajibikaji wake kwa wananchi.

Huyu aliyeibeza katiba na kuita kitabu kwake kuwajibika kwa wananchi ni utashi kuliko huyu aliyepata ridhaa ya kupigiwa kura kwa kuwa madaraka na mamlaka yake yametoka direct kwa wananchi,ndiyo maana ulinzi wa rasilimali za Taifa kwake kuhojiwa ni matusi na fedheha.

Kinachosikitisha chama cha wananchi kinapogeuka kuwa chama Dola,kinapoteza uwezo wake wa kuogoza zaidi ya kutumia mabavu.

Athari yake kubwa kinapoteza thinking tank ya chama kwa kuwa vyombo vya Dola vinajibu hoja za wananchi kwa nguvu ya mabavu, na kutweza utu wa wahanga wa mfumo usioamini katika umoja wa Taifa.

SULUHISHO

Kwa kuwa suala la mchakato wa katiba mpya kabla ya uchaguzi linaelekea kukwama,na kwa kuwa moja ya maridhiano ya kisiasa kwa vyama viwili vilivyohasimiana vimeshindwa kupatiwa uvumbuzi ni muhimu Sasa kwa wananchi kujua umuhimu kwanza wa kulinda Kodi zao zilizo tumika kwa ajili ya uratibu wa maoni ya rasimu ya Warioba,kwa kupitia AZAKI kulazimisha kuendelea na tulipoishia kwenye bunge la katiba na kuitaka serikali iheshimu maoni ya wananchi kwa kuandaa kura ya maoni.

Serikali iheshimu KATIBA iliyoko na iache mara moja kuwatisha na kuwasumbua wakosoaji wenye malengo mazuri ya kulinda rasilimali za Taifa.

Wanasheria,wananchi kwa umoja wao,vyama vya siasa na AZAKI zifungue kesi ya ubadhilifu wa mali ya umma uliofanywa na serikali kupitia mgongo wa mchakato wa katiba mpya.
 
Back
Top Bottom