Wizara ya habari kuchunguza tukio la DED wa Temeke kuwaweka chini ya ulinzi waandishi kwa kufika kwenye kikao chake bila mwaliko

Wanahabari Christopher James wa ITV&RADIO ONE na Dickson Billikwija wa Island TV waliwekwa chini ya ulinzi kwa saa 3 kwa maagizo ya Mkurugenzi Manispaa ya Temeke Lusabilo Mwakabibi, baada ya wanahabari hao kufika kwenye kikao cha wafanyabiashara wa soko la Mbagala Rangi Tatu na Mkurugenzi huyo bila mwaliko.

"Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tunafuatilia malalamiko ya wadau wa Tasnia ya Habari juu ya DED wa Manispaa ya Temeke,Mwakabibi, kuweka chini ya ulinzi Wanahabari, tunaomba Wanahabari wawe na subira wakati allegations hizi za kusikitisha zinafanyiwa kazi”-BASHUNGWA

Pia soma > Mkurugenzi wa Temeke, Mwakabibi awasweka ndani waandishi wa habari ili wasihudhurie kikao chake na wafanyabiashara
Tatizo kubwa tanzania ni kuwa jeshi la polisi halijui madaraka yake na wala polisi wenyewe hawajui wanachukua amri kutoka kwa nani? Kila kiongozi wa serikali anadhani kuwa ana uwezo wa kuwapa amri polisi kukamata na kuweka ndani raia, na polisi nao wanadhani kila amri wanayopewa na kiongozi wa serikali basi ni lazima waitekeleze.

Kiongozi wa serikali anao uwezo wa kuomba msaada wa kipolisi kuzuia mtu au watu kuingia mahali pa shuhuli za serikali ikiwa hawatakiwi kuwepo hapo au wanaleta fujo. Katika hali hii ofisa wa polisi anatakiwa kufanya uchunguzi wa haraka kujua chanzo cha tatizo hilo na kujaribu kulitatua au kuwaondosha wale wanaoleta matatizo. Ofisa polisi kwa wakati huo anao uwezo kwa majukumu ya kazi yake (sio amri ya kiongozi wa serikali) kuwaweka kuzuizini wale wote watakao kataa kufuata amri au uamuzi wake.

Kikawaida viongozi wa serikali hutakiwa kuwataka askari kuchunguza lawama au tuhuma na sio kuwapa amri askari kukamata kamata na kuweka watu jela. Sasa mfano Tanzania kiongozi anatembelea mahali na baada ya malalamiko ya watu anaamrisha askari watu fulani wakamatwe na askari wanatii amri. Hii si sahihi katika nchi ya kidemokrasia, kinachotakiwa kufanyika ni kiongozi huyo kuwataka askari kufanya uchungunguzi pamoja na kuzungumza na pande zote husika halafu ndio wao askari ndio waamue kama kuna mashitaka ya kujibiwa na nani na nani wakamatwe.
 
Huyu ni afisa kipenyo ana masifa sana .....tusubiri tuone ubabe wake mwisho wake nini....ana misifa sana na bado ataonyesha ubabe wake tena anajua wanamuogopa sababu anatekeleza watakayo wakubwa
 
Wanahabari Christopher James wa ITV&RADIO ONE na Dickson Billikwija wa Island TV waliwekwa chini ya ulinzi kwa saa 3 kwa maagizo ya Mkurugenzi Manispaa ya Temeke Lusabilo Mwakabibi, baada ya wanahabari hao kufika kwenye kikao cha wafanyabiashara wa soko la Mbagala Rangi Tatu na Mkurugenzi huyo bila mwaliko...
Kinachunguzwa nini hapa sasa wakati kila kitu kilisemwa mubashara?!
 
Tatizo kubwa tanzania ni kuwa jeshi la polisi halijui madaraka yake na wala polisi wenyewe hawajui wanachukua amri kutoka kwa nani? Kila kiongozi wa serikali anadhani kuwa ana uwezo wa kuwapa amri polisi kukamata na kuweka ndani raia, na polisi nao wanadhani kila amri wanayopewa na kiongozi wa serikali basi ni lazima waitekeleze...
Hapa tatizo ni sheria ya polisi na polisi wasaidizi ndio inawataja hao wateule was rais kuwa na amri juu yao!
 
Mwakabibi.jpg

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mh Bashungwa amesema Serikali inachunguza suala la Mkurugenzi wa Temeke Dkt. Mwakibibi kuwasweka ndani waandishi wa habari.

Baada ya uchunguzi hatua stahiki zitachukuliwa.

Chanzo: ITV habari

Ramadhan Kareem!
 
Mwakabibi jamani ana dharau sijapata ona daahh!mwaka 2019 alinioneshea dharau moja subhana llaaah!sisahau mpk naingia kaburini!kwa kweli yule DEO hapana km Mimi tu alinoneshea action ile tena hanijui!sipati picha hao watumishi wake au watu wengine!

Yule baba sina hamu!Mungu huko aliko atanilipia
 
Huyo Bashungwa hamjui vzr amwite amuhoji atakipata chake yuke dharau sababu anajiona afisa kipenyo
 
Itaje hiyo dharau.
 
Huyo Bashungwa hamjui vzr amwite amuhoji atakipata chake yuke dharau sababu anajiona afisa kipenyo
Afisa kipenyo hana mamlaka ya kufanya uhuni akiwa kwenye ofisi za umma, kama huu ushamba ndio unampa kiburi alichonacho hafai kuendelea kuwepo ofisini.
 
Mwakabibi jamani ana dharau sijapata ona daahh!mwaka 2019 alinioneshea dharau moja subhana llaaah!sisahau mpk naingia kaburini!kwa kweli yule DEO hapana km Mimi tu alinoneshea action ile tena hanijui!sipati picha hao watumishi wake au watu wengine!

Yule baba sina hamu!Mungu huko aliko atanilipia
Hiyo dharau yake ilikuathiri kwa namna yoyote? Funguka, maana sio mara kwanza wewe kulisemea hili.
 
Kuna clip flan niliiona ya Dc flan akimfokea mwaume mwenzie ka mtoto.sijui wapoje tu.
Mbona huo si utamaduni wetu jamani.
 
Hiyo dharau yake ilikuathiri kwa namna yoyote? Funguka, maana sio mara kwanza wewe kulisemea hili.
Mnoooo!maana nilikua nafuatilia haki ya mzazi wangu nikaambiwa nikaonane na DED yeye ndo msemaji wa mwisho nimefika pale ndani kwa sekretari wake namsubiria maana alikua na mgeni,sasa akatoka yule mgeni,Mimi nikawa nataka kuingia ndani niongee nae huwezi amini alinifungia mlango kwa nguvu (maana alimsindikiza mpk mlangoni yule mgeni)hapo ndo nilikua nataka nimsalimie hakuitika salami yangu akabamiza mlango akafunga kabisa na funguo.Yule secretary aliguna tu akanipa pole.Kiukweli aliniumiza mnooo mpk mchozi ulinitoka!!
Nikawaza wangapi wanafanyiwa kama Mimi nyuma ya pazia,amenionaje?who is he?yuko pale kwa kazi gani kama si kutusikiliza wananchi?mbona afisa utumishi alinipokea vzr na akanipa mpk business card yake akaniambia NENDA KWA DED THEN ANYTHING rudi au nipigie nikusaidie.
Huyo baba ana dharau mnooo.Simpendi na simchukii lakini ipo siku Mungu atanilipia hiii!
 
Afisa kipenyo hana mamlaka ya kufanya uhuni akiwa kwenye ofisi za umma, kama huu ushamba ndio unampa kiburi alichonacho hafai kuendelea kuwepo ofisini.
Hiyo ndio jeuri yake .....dharau na kiburi hiko tu labda arudi kambini tena arusha ndio kituo chake cha mwisho ......
 
Wanahabari Christopher James wa ITV&RADIO ONE na Dickson Billikwija wa Island TV waliwekwa chini ya ulinzi kwa saa 3 kwa maagizo ya Mkurugenzi Manispaa ya Temeke Lusabilo Mwakabibi, baada ya wanahabari hao kufika kwenye kikao cha wafanyabiashara wa soko la Mbagala Rangi Tatu na Mkurugenzi huyo bila mwaliko.

"Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tunafuatilia malalamiko ya wadau wa Tasnia ya Habari juu ya DED wa Manispaa ya Temeke,Mwakabibi, kuweka chini ya ulinzi Wanahabari, tunaomba Wanahabari wawe na subira wakati allegations hizi za kusikitisha zinafanyiwa kazi”-BASHUNGWA

Pia soma > Mkurugenzi wa Temeke, Mwakabibi awasweka ndani waandishi wa habari ili wasihudhurie kikao chake na wafanyabiashara
Mnamchunguzaje mtu ambaye yupo ofisini?, wachunguzi hao hawajui wakifanyalo!.
 
Back
Top Bottom