Mkurugenzi wa Temeke, Mwakabibi awasweka ndani waandishi wa habari ili wasihudhurie kikao chake na wafanyabiashara

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,808
141,711
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Dkt. Mwakibibi leo aliwaweka chini ya ulinzi waandishi wa habari waliofika ofisini kwake kuripoti yanayojiri katika kikao cha mkurugenzi huyo na wafanyabiashara.

Waandishi hao walifika ili kupata ukweli wa madai ya wafamyabiashara hao kwamba Dkt. Mwakibibi anawakatia risiti feki wanapolipia kodi za vibanda vyao.

Waandishi wamedai kuwekwa ndani hadi mkutano ulipokwisha ndipo wakaachiliwa huru.

Chanzo: ITV habari

My take; Mwakibibi anajisahau sana utawala huu siyo wa mwendazake!

Pia soma Ummy Mwalimu awatumbua Mkurugenzi wa Temeke (Mwakabibi) na Mkurugenzi wa Sumbawanga (Msemakweli)
 
Hivi bado hawasomi alama za nyakati? Si ndiye huyo huyo Mkurugenzi wa Temeke alimjibu mwandishi kuwa si hadhi yake kuonana labda Mkurugenzi wa chombo husika. Km huwahitaji waandishi wa habari kwenye kikao chako, ni kiasi cha kuwaelekeza tu.

This is too much, wanawachafua hata waliowateua. Nafikiri huyu DED atakuwa wa kwanza kuyumbuliwa ktk hizo nafasi za Ukurugenzi.

Viongozi wasome alama za nyakati, Wamwelewe Mh. Rais SSH.
 
Hivi bado hawasomi alama za nyakati? Si ndiye huyo huyo Mkurugenzi wa Temeke alimjibu mwandishi kuwa si hadhi yake kuonana labda Mkurugenzi wa chombo husika. Km huwahitaji waandishi wa habari kwenye kikao chako, ni kiasi cha kuwaelekeza tu. This is too much, wanawachafua hata waliowateua. Nafikiri huyu DED atakuwa wa kwanza kuyumbuliwa ktk hizo nafasi za Ukurugenzi. Viongozi wasome alama za nyakati, Wamwelewe Mh. Rais SSH.

Hao ndio wakurugenzi wa enzi za utawala wa dhalimu, hawa walitumika kunajisi uchaguzi, hivyo wanajua serikali iliyopo iko madarakani kwa wizi wa kura, na yeye anajua hakuna chochote kufahamika kama ule wizi wa kura aliosimamia.
 
Huyu ndugu sijui kama atatoboa, kama kumbukumbu zangu zipo sawa kama siyo mwaka huu ni last year mwishoni alimjibu vibaya mwandishi wa aitivi
 
Ukiona wanakuwa na uadui na vyombo vya Habari basi ujue kuna uozo wanaouficha na ni Wezi wa Mali za Umma
 
Back
Top Bottom