WITO-Chenge Jiuzulu kamati ya maadili ya Chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WITO-Chenge Jiuzulu kamati ya maadili ya Chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Apr 21, 2008.

  1. Mpaka Kieleweke

    Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

    #1
    Apr 21, 2008
    Joined: Feb 27, 2007
    Messages: 4,135
    Likes Received: 51
    Trophy Points: 145
    Huu sasa ni wakati wa kumtaka Chenge pamoja na viongozi wa CCM kuhakikisha kuwa wanamwajibisha Chenge kwa kumfukuza uenyekiti wa kamati ya maadili ya CCM.

    Kama kweli CCM inapinga vufisadi yafaa sasa na Cheenge aiachie kasmati ya maadfili kwa watu wenye maadili khuu ni utanio kwa umma na matusi kwa wana CCM wote eti huyu ndio awe kinara wa maadili wa chama .

    Huu ni wito wana CCM amueni sasa ......
     
  2. Gaijin

    Gaijin JF-Expert Member

    #2
    Apr 21, 2008
    Joined: Aug 21, 2007
    Messages: 11,850
    Likes Received: 35
    Trophy Points: 0
    hivi chenge ni mweyekiti wa kamati ya maadili!! kwa maadili gani aliyonayo?
    iwapo ccm haitomuuzulu cheo hicho nitajua hawa watu wanawadharau watanzania kwa kuwaona wasiojua maana
     
  3. Gembe

    Gembe JF-Expert Member

    #3
    Apr 21, 2008
    Joined: Sep 25, 2007
    Messages: 2,506
    Likes Received: 10
    Trophy Points: 135
    Kwanini Ajiuzuru katika kamati ya maadili ya chama?

    ibara ya kumi na tatu ya CCM inaelezea jinsi uanachama unavyokoma kwa Mwana CCM

    Na ibara ya kumi na nne kifungu cha 4,kinaelezea jinsi mwanachama anavyokwa na haki ya kujitetea na sio kmfukza mtu kwasababu katuhumiwa,CCm sio chama cha wahuni na kinaongozwa na katiba .Tuache uchunguzi umalizike kwanza na ajitetea ili kuwe na Natural Justice
     
  4. Mtu wa Pwani

    Mtu wa Pwani JF-Expert Member

    #4
    Apr 21, 2008
    Joined: Dec 26, 2006
    Messages: 4,096
    Likes Received: 21
    Trophy Points: 135
    labda chadema hutimuana bila ya kupeana nafasi za kujitetea
     
  5. Azimio Jipya

    Azimio Jipya JF-Expert Member

    #5
    Apr 21, 2008
    Joined: Nov 27, 2007
    Messages: 3,370
    Likes Received: 13
    Trophy Points: 135
    Chenge amejiuzuli UWAZIRI: That is not a concept any longer.

    Sifikiri kilichomfanya afikie uamuzi huo kinampa SIFA za kumfanya kinara na mfano wa kuigwa ndani ya Kamati ya maadili ya chama chake. Si maadili mema na yakuigwa yaliyompelekea Bw vijisenti kujiuzulu Uwaziri. Si maadili ya kutukuka na ya kusufiwa kwa kishindo yaliyompelekea Mhesimiwa Chenge Kujiuzulu.

    Sifa zilizo mkosesha Vigezo vya kuendelea kuwa waziri kwa wakati huu ... sioni kuwa zinakubalika na kupaliliwa na Wanachama safi wa chama chake.

    Kama kisicho mpa sifa na qualifications za kuendela kukaa kwenye nafasi ya uwaziri .... kinakubalika na chama chake ...Chama hicho tukiiteje? Chama hicho kitafsiriwe vipi kimaadili?

    I wish Change asinge kuwa na sababu nzito za kujiuzulu .... Ili tuenedelee kumtetea kuwa safi kabisa na awe kweye kamati ya maadili....Lakini amesha jiuzulu...Na kilichompelekea kujiuzulu...Si maadili ya kutukuzwa...iweje awe wa kuongoza wengine... kuelekea kwenye maadili asiyokuwa nayo?

    Change must be brought down...kutoka kwenye kamati..bila kuchelewa!
     
  6. M

    Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

    #6
    Apr 21, 2008
    Joined: Jul 5, 2007
    Messages: 5,194
    Likes Received: 9
    Trophy Points: 0
    Mhh,

    nilidhani Chenge ametimuliwa na Kikwete kama wengine walivyotaka niamini hapa???/!!!!??/
     
  7. Bongolander

    Bongolander JF-Expert Member

    #7
    Apr 21, 2008
    Joined: Jul 10, 2007
    Messages: 4,882
    Likes Received: 33
    Trophy Points: 135
    MY GOODNESS, yaani Chenge ndio Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya Chama, sasa kama Mwenyekiti wa kamati ya maadili anaweza kufanya aliyofanya, je wasio na maadili wamefanya nini?? We gonna die for sure!
     
  8. Masanilo

    Masanilo JF-Expert Member

    #8
    Apr 21, 2008
    Joined: Oct 2, 2007
    Messages: 22,319
    Likes Received: 144
    Trophy Points: 160
    Kwa hili Watson, alisema kweli ndivyo tulivyo...
     
  9. Mzee Mwanakijiji

    Mzee Mwanakijiji Platinum Member

    #9
    Apr 21, 2008
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 31,071
    Likes Received: 5,209
    Trophy Points: 280
    uchunguzi gani tuuache umalizike?
     
  10. Gembe

    Gembe JF-Expert Member

    #10
    Apr 21, 2008
    Joined: Sep 25, 2007
    Messages: 2,506
    Likes Received: 10
    Trophy Points: 135
    Uchunguzi wa kama kweli pesa alizonazo huko nje alizipata kwa njia ya Rushwa au kihalali..that is the argument and nothing else.
     
  11. Mwiba

    Mwiba JF-Expert Member

    #11
    Apr 21, 2008
    Joined: Oct 23, 2007
    Messages: 7,606
    Likes Received: 201
    Trophy Points: 160
    kama jamaa hio ela ni yake au kapewa aitunze ,usishangae ukasikia wengine wanakufa kwa shinikizo la damu ,kama unakumbuka Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa akimaliza kusanya anampelekea rafiki yake kipenzi Jamal amuekee benki utafikiri Nyerere hakusoma ,eti akimuona Jamali ndio hana matata ,Jamali akiandikisha kwa jina lake mauzo yote ya Nyerere baati mbaya Jamali akafariki mwanzo ,Nyerere kuenda kudai Pesa Mke wa jamali akamjibu Bana haikuacha feza yako kwangu ,embu angalia hii hesabu yake yote ipo ona zote hizi meandika Jamali hamna Nyerere veve nenda Dar kama nikiona nitakujulisha ,si umeona menyewe hakuna jina lako,dah Mchonga kusikia kauli hiyo ya mke wa Jamali hakurudi tena ndio safari ya kusafiri kuelekea kusiko julikana na msafiri mwenyewe.
    Sasa kisanga cha Chenge huwezi kujua feza yote ni ya nani ,je mwenyewe atajitokeza maana hata ukimpigia mahesabu kwa feza ya KiTz sijui kwa siku alikuwa anaweka na kutunza kiasi gani au ni biashara ipi ambayo ingempatia kipato cha vijisent vyote hivyo
    ukijumlisha miaka aliyoanzia kazi kama mfanya kazi wa serikali ,mtu ambae hakuinukia na Tanu kama vingunge wengine ambao raha yao ni kupanda kwenye majukwaa wakishindana kwa mabezo na vyama vya upinzani ,hili gurupu la mafisadi ukilikusanya utaona ni vijana walioinukia juzi juzi tu hata hawakujulikana kwenye siasa na ujanja wao ndio walikuwa wanawagonganisha vichwa akina kingunge Kawawa na wananchi kwenye vilili vya mikutano ,hawa hata sijawaona kuhutubia kwenye mikutano ya Hazara ,huachiwa akina Makamba ,yaani CCM ina wazee wababaishaji kibao ambao wao kazi yao ni kuweka ngumu na propaganda yaani hawa akina mafisadi wakimsifu Kingunge basi kingunge anaona hakuna mwana siasa machachali kama yeye kumbe jamaa wana mambo zao ,sasa akina makamba na kingungu wamebaki mido wazi.
     
  12. M

    Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

    #12
    Apr 21, 2008
    Joined: Jul 5, 2007
    Messages: 5,194
    Likes Received: 9
    Trophy Points: 0
    Haya yote ni uongo mtupu!
     
  13. Pundit

    Pundit JF-Expert Member

    #13
    Apr 21, 2008
    Joined: Feb 4, 2007
    Messages: 3,741
    Likes Received: 21
    Trophy Points: 0

    Gembe unaongelea uchunguzi wa SFO ya Uingereza au upi huo?

    Maana mpaka leo sina taarifa kwamba kuna uchunguzi bongo, au Tume ya Maadili imeshaanza uchunguzi?
     
  14. Gaijin

    Gaijin JF-Expert Member

    #14
    Apr 22, 2008
    Joined: Aug 21, 2007
    Messages: 11,850
    Likes Received: 35
    Trophy Points: 0
    kama tuache uchunguzi wa kuonyesha anayo maadili au la, nadhani jamii ya kitanzania ishamhukumu kuwa hana maadili pale alivyoita bilioni moja kuwa ni vijisenti.
     
  15. N

    Nsololi JF-Expert Member

    #15
    Apr 22, 2008
    Joined: Mar 8, 2007
    Messages: 263
    Likes Received: 6
    Trophy Points: 35
    Kweli watu wakipenda kitu hawaoni chongo.... Yaani mtu mwenye akili timamu anaamini kuwa waziri wa serikali ya Uingereza mwenye pesa yake aliyoipata kihalali anaweza kuja kuweka pesa yake kwenye benki nchini Tanzania iliyoko visiwa vya Mafia au Songosongo????

    Chenge kuweka pesa yake visiwa vya Jessey bado mtu anataka tuamini kuwa hakuzificha hizo pesa ili watu wasijue???

    Kawaulize watu wenye wabilioni yao halali (ingawa pia wanaweza wakawa wamejiongezea na nyingine zisizo halali) kama akina mengi, Dialo, Mungai, Mkono, Mohamed Dewji, Ndesamburo, n.k. kama wanaficha pesa zao kama huyo jambazi/fisadi Chenge??? Haya mambo hafai kupigiwa chapo na watu wenye itikadi za kiupinzani bali waTZ wote kwani wote tumedhurumiwa na hiyo mifisadi.

    Ni hatari kama mambo ya kitaifa kama haya watu wengine wanayafanya ya ki-vyama zaidi.

    Ahsanteni,
     
  16. Gigo

    Gigo JF-Expert Member

    #16
    Apr 22, 2008
    Joined: Aug 6, 2006
    Messages: 455
    Likes Received: 39
    Trophy Points: 45
    Kama Chenge alifaa kuwepo kwenye uwenyekiti wa kamati ya maadili....basi hata mwenyekiti wa Chama anaweza akawa Fisadi!!
     
  17. Mpangwa Asilia

    Mpangwa Asilia Member

    #17
    Apr 22, 2008
    Joined: Mar 6, 2008
    Messages: 25
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Mwiba, unauhakika wa haya uliyoyaandika? Au unataka kutufurahisha na KUTUUDHI?? Au ndo unalengo la kuficha ukweli wa akina AC? Na maanisha hiyo story yako ya Jamal na Nyerere. "Mungu mlaze pema peponi mwl. Nyerere."
     
  18. Gembe

    Gembe JF-Expert Member

    #18
    Apr 22, 2008
    Joined: Sep 25, 2007
    Messages: 2,506
    Likes Received: 10
    Trophy Points: 135
    Yes I said ,Nangojea kwa hamu sana majibu haya coz wao ndio waliosema kwamba Chenege anahusika na ulaji wa pesa.

    Hivi hakuna sheria ambayo inaweza kumgusa mtu ambaye aliagizwa kampuni flani wauuziwe kitu kwa kuwa yeye ana madaral flani?
     
  19. Mtu wa Pwani

    Mtu wa Pwani JF-Expert Member

    #19
    Apr 22, 2008
    Joined: Dec 26, 2006
    Messages: 4,096
    Likes Received: 21
    Trophy Points: 135
    jamani NNaomba huyu msimwite AC maana mm hunipa tabu kujua Amina Chifupa(marehemu) au Huyu Andrew Chenge

    nnashauri kama ikiwezekana tuongeze iwe ACh
     
  20. K

    KakindoMaster JF-Expert Member

    #20
    Apr 22, 2008
    Joined: Dec 5, 2006
    Messages: 1,315
    Likes Received: 36
    Trophy Points: 145
    Hivi unauliza hili?
     
Loading...