CCM waanza mchakato wa kumshughulikia Luhanga Mpina, awasili mbele ya kamati ya maadili CCM

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,770
18,181
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, habari kutoka ndani ya CCM zinabainisha kuwa CCM wameishaanza mchakato wa kumfukuza uanachama mbunge wa Kisesa, ndugu Luhanga Mpina.

1706164657528.png


Inasemekana kabla mama hajasafiri kwenda Indonesia alitoa maagizo kwamba akirudi asikumkute Mpina bado akiwa ndani ya CCM. Sababu za kufukuzwa ndugu Mpina hazijawekwa wazi lakini kwa siku za hivi karibuni Mpina amekuwa mwiba mkali kwa mafisadi na chawa wanaofisadi na kuuza rasilimali za taifa kwa wageni huku wananchi wakiendelea kutopea kwenye umaskini na huduma mbovu za jamii.

Habari zaidi zinasema kabla ya kufukuzwa ndugu Mpina atapewa nafasi ya kujitetea mbele ya kamati maalumu ya CCM iliyoteuliwa na Rais kushughulikia suala hili ambalo wao wameliita "tatizo la kinidhamu ndani ya chama". Haikuweza kufahamika mara moja kamati hiyo inaundwa na akina nani lakini chanzo kingine kutoka CCM kinadai katika kamati hiyo wamo Kinana, Makonda, Yusufu Makamba na wazee wengine mashuhuri wa CCM.


----
Mpina awasili mbele ya kamati ya maadili CCM

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameitikia wito wa Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu iliyomtaka afike leo, Alhamisi 2024 kwa ajili ya mahojiano ya masuala mbalimbali.
Mpina aliyewahi kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi amewasili mchana wa leo Alhamisi, Januari 25, 2024 kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Usalama na Maadili ya wilaya hiyo.

Jana Jumatano, Katibu wa CCM Wilaya ya Meatu, Joel Makwaia aliiambia Mwananchi Digital kuwa wamemwita Mpina mbele ya kamati hiyo kutokana na mambo mbalimbali yaliyojitokeza.


---
MAONI YANGU
Kufukuzwa kwa Mpina kutoka CCM kulikuwa dhahiri tangu alipoanza kuwavalia njuga mafisadi, wauza nchi na chawa wanaotafuna rasilimali za nchi bila kuhojiwa. Hili lilikolezwa na msimamo wake dhabiti wa kupinga uuzaji wa bandari kwa waarabu wa DP World.

Jambo ambalo mpaka sasa haliko dhahiri ni kwamba je akifukuzwa CCM atahamia chama gani? Possibly itakuwa CHADEMA kwa sababu baadhi ya wazalendo na wana intelejensia wanadai kuwa Mpina ni kada wa CHADEMA aliyetumwa kuingia ndani ya CCM kimkakati ili kukipeleleza chama hicho.

Lakini mpaka sasa hakuna mwenye uhakika 100% kuhusu chama ambacho mpina atatimkia ili kimteue kugombea kwenye uchaguzi mkuu 2025 pindi akitupiwa virago na CCM. Huenda hata akuibukia ACT-Wazalendo. You never know but time will tell. Let us wait until the end of the movie.

Pia soma:
1.
Tetesi: - Wabunge washauri Luhaga Mpina afukuzwe CCM

2.
Tetesi: - Karibu CHADEMA Luhaga Mpina, Kazi tulikutuma CCM umeitendea haki.
 
Kama mtamchukua awe mwanachama wa kawaida,Mkirogwa kumchukua Chadema mtapoteana na hamtaamn,huu ni mkakati uliosukwa vzuri kuandaa kada mtiifu wa CCM, mtu mwenye ushawishi na anayeendana na sera za chadema Ili apewe nafasi ya maamuzi ktk upinzan na awavuruge.
 
Kama mtamchukua awe mwanachama wa kawaida,Mkirogwa kumchukua Chadema mtapoteana na hamtaamn,huu ni mkakati uliosukwa vzuri kuandaa kada mtiifu wa CCM, mtu mwenye ushawishi na anayeendana na sera za chadema Ili apewe nafasi ya maamuzi ktk upinzan na awavuruge.
Mpaka sasa hakuna mwenye uhakika atatimkia chama kipi. Uwe unasoma uzi usiishie kusoma heading tu.
 
Back
Top Bottom