Rais wa TLS azitaka kamati za maadili ya Mawakili zitende haki

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,177
7,750
Rais wa Chama Cha Mawakili Tanganyika ndg. Harold Sungusiya amezitaka Kamati za Maadili za Mawakili na Mahimu kuwatendea haki pindi wanapo tuhumiwa na kufikishwa mbele ya Kamati hizo.

Amesisitiza kuwa, pamekuwepo na uonevu na ukandamizwaji wa watuhumiwa wanapo fikishwa mbele ya kamati hizo. Hivyo ameziomba kamati zinazo shughulikia maadili ya Mawakili na Mahakimu kuwatendea haki na sio kuonea watuhumiwa..

Kamati za maadili zisitumike kuwakomoa ama kuwaonea watuhumiwa au kuwaharibia taaluma na kazi zao.

Chanzo utv/tbc/itv na chanel ten.
Maadhimisho ya kilele cha siku ya Sheria kutoka viwanja vya Chinagali Dodoma tarehe 1/02/2024.
 
Ni

Ni wakili ama hakimu gani huyo alionelewa na kamati?

Binafsi hupenda kuona mtu yeyote anayehukumu wenzake naye akihukumiwa.

Hupenda kuona mkamataji naye akikamatwa, muuaji naye akiuawa, mwizi naye akiibiwa.

Hupenda kuona wanyama wanaokula wenzao mfano simba akiliwa na mbwa mwitu, fisi akiliwa na simba, nyoka akiliwa na nguchiro nk nk.
Karma is really!!
 
Rais wa Chama Cha Mawakili Tanganyika ndg. Harold Sungusiya amezitaka Kamati za Maadili za Mawakili na Mahimu kuwatendea haki pindi wanapo tuhumiwa na kufikishwa mbele ya Kamati hizo.

Amesisitiza kuwa, pamekuwepo na uonevu na ukandamizwaji wa watuhumiwa wanapo fikishwa mbele ya kamati hizo. Hivyo ameziomba kamati zinazo shughulikia maadili ya Mawakili na Mahakimu kuwatendea haki na sio kuonea watuhumiwa..

Kamati za maadili zisitumike kuwakomoa ama kuwaonea watuhumiwa au kuwaharibia taaluma na kazi zao.

Chanzo utv/tbc/itv na chanel ten.
Maadhimisho ya kilele cha siku ya Sheria kutoka viwanja vya Chinagali Dodoma tarehe 1/02/2024.
Hakimu ama wakili gani alionelewa?

Binafsi hupenda kuona anayehukumu wenzake, naye akihukumiwa.

Hupenda kuona mchawi naye akirogwa, mwizi naye akiibiwa, muuaji naye akiuawa, mkamataji naye akiswendekwa ndani.

Hupenda kuangalia documentaries za wanyama kuona namna ya wanyama wanaokula wenzao jinsi ambavyo nao huliwa, mfano hupenda kuona fisi akiliwa na simba, simba akiliwa na mbwa mwitu, nyoka akiliwa na nguchiro,mamba akiliwa na chui nk nk.

Pia hupenda kuona wachimba makaburi na wachonga majeneza nao wakizikwa.

Sasa hao staff wa vyombo vya haki imekuwaje wanalalamika huku wao wakilalamikiwa kupindisha haki za watu?
 
Yeye katoa maoni yake kwa ujumla kuwa watuhumiwa wa makosa ya Kimaadili pindi wanapo fikishwa mbele ya kamati za maadili basi watendewe haki, wasionewe wala kunyimwa haki zao za kimsingi.

Alicho kisema kimewafikia walengwa.
Haki kutendeka bila uonevu ndio jambo la kuzingatiwa hapo sio jingine.
 
Hakimu ama wakili gani alionelewa?

Binafsi hupenda kuona anayehukumu wenzake, naye akihukumiwa.

Hupenda kuona mchawi naye akirogwa, mwizi naye akiibiwa, muuaji naye akiuawa, mkamataji naye akiswendekwa ndani.

Hupenda kuangalia documentaries za wanyama kuona namna ya wanyama wanaokula wenzao jinsi ambavyo nao huliwa, mfano hupenda kuona fisi akiliwa na simba, simba akiliwa na mbwa mwitu, nyoka akiliwa na nguchiro,mamba akiliwa na chui nk nk.

Pia hupenda kuona wachimba makaburi na wachonga majeneza nao wakizikwa.

Sasa hao staff wa vyombo vya haki imekuwaje wanalalamika huku wao wakilalamikiwa kupindisha haki za watu?
Wachimba makaburi? Unawaonea
 
Wachimba makaburi? Unawaonea
Ujue nini mkuu, haujawekeza akili zako kuwachunguza wachimba makaburi pamoja na watu wa mortuary!

Ukiwakuta wakifanya hiyo shughuli, wakati ninyi mkilia na kuomboleza, wao ni kupiga soga na kucheka bila kujawa na huzuni yoyote.

Kuna siku moja, staff mmoja wa mortuary, ingawa alinieleza kimzaha mzaha kuwa: ... 'Wewe mzee ukifa nitakupamba vizuri sana na ndevu zako hizo ntazinyoa'..., mtu huyo tayari tunavojadili hapa, siku nyingi alishatangulia mbele za haki.

Alikuwa akiniwazia mimi kufa kwa vigezo anavyovijua, huku yeye akijiweka pembeni.

Kwa hiyo wao huandaa makaburi huku akili zao zikisoma kuwa kaburi wanalolichimba haliwahusu anakuja kuzikwa mwingine.
 
Watahuzunika kwa watu wangapi? Kila siku huzuni kazi itafanyika kweli?
 
Back
Top Bottom