Nimewasilisha malalamiko yangu Sekretariati ya Maadili dhidi ya Pauline Philipo Gekul (Mb)

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Maadili ya viongozi wa Umma Sura. No.398( R.E 2020) kifungu cha 25(1) kinachotoa fursa kwa mtu yeyote kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya kiongozi wa Umma juu ya uvunjifu wa sheria ya Maadili ,pia kwa mujibu wa Katiba 1977 ibara ya 26(2) inayotoa agizo la wajibu na haki kwa kila mtu kulinda katiba ya JMT na sheria zingine za nchi.

Leo tar.27/Novemba/2023 nimewasilisha malalamiko yangu kwa Kamishna Sekretariati ya Maadili ya viongozi wa Umma dhidi ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul juu ya tuhuma zinazoendelea dhidi yake juu ya unyanyasaji dhidi ya Hashimu Ally Philimone.

Nikiamini ya kwamba Pauline Gekul amevunja sheria ya Maadili ya viongozi wa Umma Sura No.398 (R.E 2020) kifungu cha 6(1)(a) na 6(1)(b)(i) vifungu hivi vinahitaji viongozi wa Umma kutenda majukumu yao ya kiofisi hata majukumu binafsi kwa kuzingatia Maadili, uaminifu, huruma na uadilifu.

Hivyo, nimewasilisha malalamiko yangu kwa Kamishna Sekretariati ya Maadili iliyopo chini ya Ofisi ya Rais ili Ofisi yake ianze uchunguzi dhidi ya tuhuma hizi kwa mujibu wa Katiba ya JMT 1977 ibara ya 132(1) na sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Sura 398 [R.E 2020)] kifungu cha 16(2)(b)(c)(e), 25(2)(b) na 25(4-7). Na ikiwa itathibitika kwamba tuhuma hizi dhidi ya Pauline Gekul basi Gekul atakuwa amevunja masharti ya sheria ya Maadili ya viongozi wa Umma kifungu cha 6(1)(a) na 6(1)(b)(i). Na hivyo moja kwa moja Pauline Gekul atakoma kuwa Mbunge wa JMT.

Kwa mujibu wa katiba ya JMT 1977 ibara ya 71(1)(d) inasema kwamba "Mbunge atakoma kuwa Mbunge ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma". Nimewasilisha flash-Memory yenye ushahidi wa Video ya Dakika 14 kutoka Gaditv

Pia nimetuma nakala kwa Spika wa Bunge, Ofisi ya Rais Ikulu na Katibu Mkuu Chama cha Mapinduzi (CCM).

Ahsante. Unaweza Soma barua ya malalamiko yangu kwa Kamishna Sekretariati ya Maadili ya viongozi wa Umma.

Abdul Omary Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa -ACT Wazalendo

826517382.jpg
484259350.jpg
1722987491.jpg
 
Watu wengine wakihusishwa tuu na uhalifu wanashikwa kwa kupigwa mateke na virungu alafu uchunguzi unafuata badae wakiwa mahabusu, lakini wenye nafasi zao watu wanaanza kujadili namna ya kuwashika, yani wanakua kama wanataka kuyapaka mafuta makosa yake yaonekane ni makosa ya kawaida, muda ni hakimu mzuri lakini hili nalo litapita tuu kama ya kina sabaya
 
watu wengine wakihusishwa tuu na uhalifu wanashikwa kwa kupigwa mateke na virungu alafu uchunguzi unafuata badae wakiwa mahabusu, lakini wenye nafasi zao watu wanaanza kujadili namna ya kuwashika, yani wanakua kama wanataka kuyapaka mafuta makosa yake yaonekane ni makosa ya kawaida, muda ni hakimu mzuri lakini hili nalo litapita tuu kama ya kina sabaya
Nchi Ina mambo ya hovyo sana hii.
 
Back
Top Bottom