Wimbo bora wa kwaya wa siku zote (Best of all times)

Grey256

JF-Expert Member
Sep 1, 2016
1,066
2,188
Shaloom wakuu,

Tasnia ya muziki wa injili kwa vikundi vya kwaya hapa Tanzania ni tasnia kongwe na iliyotawala zaidi kwenye chati za nyimbo za dini ya Kikristo mpaka ilipofikia miaka ya 2000's ambapo walianza kuibuka waimbaji wa kujitegemea wa nyimbo za injili na kwa wingi wao imepelekea umaarufu wa vikundi na nyimbo za kwaya kushuka kwa miaka ya karibuni.

Binafsi ni mpenzi mkubwa wa nyimbo za kwaya toka miaka hiyo mpaka sasa na leo niliamka nikiwaza ni nyimbo gani ya injili ya kwaya ambayo tunaweza kusema ndio nyimbo bora zaidi kupata kutengenezwa/kuimbwa hapa Tanzania toka mziki huu uanzishwe.

Naomba mnisaidie kuchagua namba moja kwenye list ya nyimbo za kwaya ninazoona ziliwahi kutikisa sana tasnia ya nyimbo za injili na wewe pia unaweza kuongezea chaguo lako kama unaona haipo kwenye orodha hiyo;

1. Tabata Menonite - Kunyata nyata
2. AIC Makongoro- Utumwa wa waisrael & Kekundu
3. Mtoni Evangelical- Lulu
4. Bethel Gospel - Yupo Mungu
5. Barabara ya 13- Samson na Delila
6. Mapigano Ulyankuru- Katika viumbe vyote & Goliati & Fahari ya vijana
7. Nkinga choir - Sauli wanitesa
8. KKKT Mabibo - Nijaposema kwa lugha & Sauti ikatoka.
9. AIC Chang'ombe - Gusa
10. Zablon Singers - Mkono wa Bwana
11. Jerusalem choir - Kesho ni yako
12. Kijitonyama uinjilisti - Hakuna Mungu kama wewe & Simba wa Yuda
13. Pastor Alex & Mary Atieno - Sodoma na Gomorrah
14. Eternal life gospel - Sio sisi
15. Mtakatifu Kizito Makuburi - Mimina & Yesu ni mwema
16. Mt. Theresia Matogoro - I love you
17. Kapotive star- Nimeonja pendo lako
18. Arusha town - Kila mtu na mzigo wake
19. Tafes (Ardhi)- Maserafi
20. Essence of worship- Mimi siwezi
21. The reapers - Ninaye rafiki
22. Muungano choir- Natembea mimi ni marehemu.
23. Mt Kizito- Watoto wa nyumba zote

Karibuni.
 

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
22,059
26,311
Muungano kwaya (Adventist) - Natembea mimi ni Marehemu

St.James/Tumaini kwaya Arusha /Shangilieni - Habari ya Mwana mpotevu, Nuhu, Nakulilia Jehova etc.

- Kijitonyama Upendo group - Hakuna Mungu kama wewe, BamBam, Masiya Wanyi, Hakuna Mwanaume kama Yesu etc.
 

Mandingo

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
4,405
3,499
Hakuna Mungu kama wewe ikipigwa Club au Bar walevi wote lazima waserebuke...

Miaka hiyo mkesha wa mwaka mpya tuko club na brother wangu Dj ,mara paap umeme umekatika na ndio inakaribia saa sita kamili na hakuna plan b ya generator,nikamwambia bro ukirudi tu umeme weka hii ngoma kama saa 6 dk 5 ivi kurudi aisee ilivyo wekwa watu waliimba utafikiri wako church!!!
 
31 Reactions
Reply
Top Bottom