Wakatoliki kwa kwaya na ufundi wa vinanda ni sawa na samaki na maji

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,038
12,364
Hawa Wakatoliki kwaya na ufundi wa upigaji vinanda kwao ni sawa na samaki na maji ni ngumu kuwatenganisha.

Kwa kweli RC ni mafundi haswa katika upande huu wa uburudishaji kwa nyimbo zao za gospel ukichanganya na vinanda vyao.

Ukikutana na mpiga kinanda fundi wa RC mpaka kichwa anatikisa huwa nafurahi sana😁

Nyimbo zao zimetulia sauti zimepangika kuanzia ya kwanza mpaka ya nne ukichanganya na ufundi wa vinanda ni mwendo wa kuburudika tu.

R.C mnatisha balaa.



Tahadhari: Huu uzi sio wa mashindano ya kidini.
 
Mikono na miguu inafanya kazi Kwa wakati mmoja ufundi uliopitiliza!
Umeona hii kitu😁
1-019-019917-Technics-SX-U60.jpg
 
Kanisa Katoliki limejaliwa hazina ya watunzi bora kabisa wa nyimbo za Kanisa, na pia wapiga kinanda mahiri kabisa!!

Siku hizi kuna vijana wadogo kabisa kama akina Ray Ufunguo, Tumaini Swai, Credo Mbogoye, Thomas Mashibe (huyu kinanda kinamheshimu sana), Mushobozi (huyu anatumia miguu yote miwili kwenye pedal) na wengineo wengi wakali!! Wanafanya vizuri sana.

Miaka hiyo wakali wa kinanda walikuwa ni akina John Mgandu, Mkude Sekulu, John Maja, nk.
 
Back
Top Bottom