Mfahamu Mika: Mwimbaji wa wimbo wa Relax

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,712
2,285
Ni Alhamisi Magaidi watatu walijitoa mhanga kwa kujilipua mabomu matatu ya kujitengenezea wenyewe wakiwa ndani ya treni za chini ya ardhi katika Jiji la London huko Uingereza. Baadaye, gaidi wa nne alilipua bomu lingine kwenye basi lililokuwa Makutano ya Tavistock Square.

_83823960_bombers_names_credit_976.jpg


Katika mashambulizi hayo, watu zaidi ya 52 ambao walikuwa ni raia wa Uingereza pamoja na wengine kutoka mataifa 18 tofauti waliuawa huku zaidi ya watu 700 wakijeruhiwa katika mashambulizi hayo. Lilikuwa ni tukio baya zaidi la kigaidi nchini Uingereza tangu kulipuliwa kwa ndege ya Pan Am Flight 103 mwaka 1988 karibu na Lockerbie, na shambulio la kwanza la kujitoa mhanga nchini Uingereza.
london.jpg

"Relax, Take It Easy"


34a8f400f0228743b0b00dfeccb10204.jpg

Hivi karibuni katika mitandao ya Kijamii ya Youtube pamoja na Tiktok imeshuhudia watumiaji wake wakipata nafasi za kusikiliza nyimbo za kitambo ambazo zinaleta hisia sana, nyimbo ambazo mwanzoni hazikupata nafasi ya kuwa na umaarufu mkubwa kutokana na utandawazi kufika sehemu chache. Leo nikukutanishe na Albamu ya Life in Cartoon Motion ambayo ndani yake ilikuwa na wimbo wa Relax, Take It Easy ambao hivi karibuni umepata kuwa maarufu sana.
maxresdefault (1).jpg

Relax, Take It Easy ni wimbo ambao kwa kiasi fulani umetumia ala ya muziki na toni ya wimbo maarufu wa "(I Just) Died in Your Arms" kutoka kundi la Cutting Crew, Relax, Take It Easy ilipata bahati ya kutumiwa kwenye filamu za Were the World Mine pamoja na Monte Carlo ya mwaka 2011. Wengi tumepata kusikiliza kwa chini chini wimbo huu huku tukipenda sana ala yake pamoja na mpangilio wa mashairi ila kiundani ni wimbo wenye kubeba huzuni ndani yake. Mtunzi na muimbaji wa wimbo huu anaitwa Mika.
maxresdefault.jpg

Nilitumia nguvu na utundu mwingi katika kuandaa utunzi wa wimbo huu, na mwanzo haukuwa na ala ya mapigo kama ilivyo sasa, nilijitahidi kutengeneza sauti na ala kwa kutumia vifaa muziki halisi na sio kompyuta, niliona ni vyema kuwa nikitumia vifaa halisi, hivyo niliona ni vyema nikatumia usaidizi wa wanamuziki ambao waliwahi kufanya kazi katika nyimbo kadhaa za wanamuziki kama vile, Quincy Jones pamoja na Michael Jackson. Tulitumia muda mwingi kupiga vyombo vya muziki ili tu kupata mtiririko sahihi wa ala ya muziki, wakati mmoja tulitumia zaidi ya masaa 19 tukia studio.
_131637414_a1343eb487e4419e21e9545c997d7d249e63f981-1.jpg

Mwaka 2017, Mika alifanya mahojiano na katika kipindi chake cha Stasera Casa Mika kilichokuwa kikiruka katika kituo cha Rai 2 kutoka Italia, Mika alielezea kuwa akiwa mtoto mdogo alikuwa akiogopa sana kwenye kituo cha London Underground, kwa sababu ya sauti kubwa paoja na umati mkubwa wa wasafiri, na wakati mmoja akia ndani ya treni akitoka studio, treni yao ilisimama ghafla, taa ndani ya usafiri wao zilizima zote na taa ziliporudi, abiria wote walipewa maelekezo kwa watoke ndani ya treni na Mika pamoja na abiria wengine walipofika nje ya kituo, walikutana na maafisa polisi na usalama wengi, siku hiyo ilikuwa ni Julai 7 2005 na inatambulika kuwa ni siku ya mashambulizi ya London au London bombings. Mika akiwa na hofu alitembea akiwa anatetemeka sana na alipofika nyumbani alianza kuandika wazo la wimbo wa "Relax, Take It Easy" ndani ya dakika 20 tu, moja ya sehemu ya wimbo huu inasema "It's as if I'm scared/It's as if I'm terrified/It's as if I scared/It's as if I'm playing with fire". London Bombing ndo ilipelekea kutokea kwa wimbo huu wa Relax ikiwa ni sehemu ya Mika kuvaa ujasiri kuwa nyakati mbaya zinapit tu na zinatuandaa kutufanya imara mbeleni.
maxresdefaulta.jpg

Katika chart za Billboard European Hot 100, wimbo huu wa "Relax, Take It Easy" ulishika nafasi ya 12 katika wiki iliyoisha Juni 30 2007, kisha ilipanda na kufika namba 8 katika wiki iliyofuata, na wiki ya tatu "Relax, Take It Easy" ilishika nambari 4 na wiki ya nne wimbo huu ukakwea mpaka kufika nafasi ya 2. Uhispania wimbo huu ulifikia kiwango kikubwa mpaka kupewa double platinum certification ukiwa umepakuliwa zaidi ya mara elfu 40, Ubeligiji ilishika nambari moja kwa muda wa wiki mbili mfululizo kwenye chart ya Ultratop, Relax, Take It Easy ilikaa nambari moja kwa muda wa wiki 7 Uholanzi katika chart ya nyimbo 40 bora, huku ikikamata nambari moja kwa wiki 15 huko Ufaransa, Relax, Take It Easy ikiwa Urusi ilipata gold certification ikiwa na copy zaidi ya elfu 50 zilizouzwa.​

maxresdefaultaqe.jpg

Dunia inamfahamu kwa jina la Mika ila kiuhalisia majina yake ya ubatizo anaitwa Michael Holbrook Penniman Jr, alizaliwa Agosti 18 1983 huko Beirut Lebanon na majiji mawili ya Paris Ufaransa pamoja na London Uingereza ndipo Mika alipopata nafasi ya kulelewa zaidi. huyu ndo ametupatia wimbo huu mtamu sana ambao umepata kufanyiwa remix zaidi ya mara 20 huku akipata umaarufu mkubwa hata baada ya miaka 17 ila kwa sasa wimbo wake huu una watazamaji zaidi ya Milioni 161 huku video nyingine ya new version ikiwa na watazamaji zaidi ya milioni 17.
Mika12.jpg

Ukiachana na Relax kuna nyimbo zingine ambazo zinaonesha ufundi wa Mika, mfano, Grace Kelly, Lollipop, My Interpretation, Love Today, Any Other World, Billy Brown, Big Girl (You Are Beautiful), Stuck in the Middle, Happy Ending, pamoja na Over My Shoulder. Mika alikuwa mwimbaji kiongozi huku mara kadhaa akipiga gitaa, kinanda, ngoma yaani kifupi alikuwa ni kiraka kila chombo cha muziki alikuwa anafahamu ufundi wa kutengeneza ala ya muziki. Pia alikuwa akifanya ziara za kimuziki akiwa pamoja na Greg Wells ambaye ni mwandishi mzuri sana wa nyimbo haswa za wasanii wakubwa kama vile, John Legend ambaye aliandikiwa wimbo wa Never Break, pamoja na Katy Perry ambaye alipata kuandikiwa wimbo wa By the Grace of God.
Mika-by-Paolo-De-Francesco-11.jpg

Katika matamasha ya Mika aliongozana pia na watu kama Tim Pierce, Dylan Schiavone, Lyle Workman, Dan Rothchild ambao walikuwa wanafahamu kucheza na nyuzi sita vyema ili kutengeneza utamu wa muziki. Ukisikiliza wimbo wa Relax au Lollipop utaona kuna sauti kwa nyuma za waitikiaji basi hiyo ilikuwa ni kazi safi kutoka kwa ndugu watatu wa Mika ambao ni Zuleika Penniman, Paloma Penniman, pamoja na Fortuné Penniman, lakini pia alikuwepo mwanadada mrembo sana Audrey Moukataff, Alexander Millar pamoja na Ida Falk Winland.

Wazungu wana msemo wao "After the storm, the wind calms down, and everything gets quiet again. In every area of life, after the turmoil and mess, there comes a period when things start to return to normal."
Good music never expires ✨ “Do Better​
 
Hatari sana MIKA moja ya wakali sana wa mashairi
Mwaka jana alitamba na kibao cha C'est la vie
Ngoma bado inasumbua kwenye chart za ufaransa hasa RFM na M!
 
Radio ebony fm ya Iringa ilitumia sana huu wimbo wake kama Jingle kwenye kipindi chake cha vuta pumzi utasikia
"Vuta pumzi... Relax take it easy!!!!
 
Hatari sana MIKA moja ya wakali sana wa mashairi
Mwaka jana alitamba na kibao cha C'est la vie
Ngoma bado inasumbua kwenye chart za ufaransa hasa RFM na M!
C'est la vie, c'est la vie, la vie, dam-dam
C'est la vie, c'est la vie, la vie, dam-dam
C'est la vie, c'est la vie, la vie, dam-dam
Mika
anajua mpaka basi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom