Kwa ujumla suala la vita ya DR Congo dhidi ya waasi ambao kwa mshangao mkubwa wameweza kuiteka miji muhimu katika nchi hiyo bila kupata upinzani wowote toka kwa majeshi ya Serikali na yale ya UN, inatufanya tulitafakali kwa undani zaidi.
Binafsi napenda kujiaminisha kuwa yawezekana majeshi ya serikali yaliweka imani kubwa sana kwenye jeshi la UN na kuliona kuwa kwao jeshi hilo ni sawa na ukuta wa shaba, lakini ikumbukwe kuwa watu haohao wanaweza kugeuka na kuwa ndumila kuwili kwa kuwapumbaza wanajeshi wa serikali ili sehemu hiyo itwaliwe na waasi kwa minajili ya kuzifaidisha nchi za wenzetu ukizingatia kuwa eneo hilo ndilo eneo lenye utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu na shaba.
Kwa picha hii, vita ya Congo inaweza isiishe mapema kutokana na baadhi ya nchi za wenzetu kuangalia maslahi zaidi kuliko kuleta amani katika eneo hilo.
Je, ni kweli tuendelee kuyategemea haya majeshi ya UN (hasa kutoka nje ya africa) ili kuleta amani katika nchi zetu za africa?
Sioni tofauti yako na hawa wanaong'ang'ana kwenye katiba yao kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa. Ni uimara gani unaouzungumzia wa jeshi lililosheheni vifaa tulivyonunua vikiwa chakavu. Unapoongelea jeshi lililomtoa Amin, unaongelea jeshi tofauti kabisa na hili la leo. Nani kati ya makamanda wa jeshi kipindi hicho aangefikiria kupiga dili apate vijisenti vya kuficha Uswisi? Use yor brain man / woman.
Thubutu yako wewe unafikiri Idd Amin tulimpiga peke yetu?