Wilaya zenye baridi sana Tanzania

Wilaya zenye baridi sana Tanzania

Ngorongoro nayo Ni noma miezi hii. Hasa Loliondo.
Wakuu bila shaka ni wazima,

Mimi ni mtu naye penda sana kitu inaitwa hali ya hewa. Kuna jamaa anatoka Makete aliwahi nisimulia baridi ya huko. Nikasema isiwe kesi nikatinga msimu wa baridi mwaka jana. Aisee ni noma. Ila jamaa wamelizoea. Kama mgeni hutakaa urudi tena. So far nimetembelea.

1. MAKETE
2. NJOMBE
3. MAKAMBAKO.
Bado MUFINDI NASIKIA NAKO SI HABA.
Hii ni nyanda za juu kusini.

Hebu tupeane update wilaya zenye baridi na linakuwa msimu upi sana.

Nawasilisha.
R
 
Nadhani Njombe inaongoza aisee, ile wilaya karibia kila mahali unapogusa ni baridi hatariii

Halafu inafuatia Mufindi, bwana we kule ndio unakunywa chai ya moto bila kujua, muda wote kuna maukungu hata wakati mwingine huoni mita 5 mbele...

Kuna wilaya ya Rungwe, haswa maeneo ya Uporoto kwa Wasafwa, noma sana kule

Halafu kuna Arumeru, kule juu juu kule kama unaukaribia mlima, kuna vijiji vina baridi kule hatari...

Mwisho kuna Lushoto na Muheza, hizi baridi zake nimeweza kuzivumilia walau hata kwa kuvaa tshirt inawezekana...

Huwa nasikia na Rombo inasifiwa lakini sijawahi fika huko

Hizo sehemu tatu za juu ni kawaida sana asubuhi kukuta umande wa theluji
Nenda Marangu-Arisi,Ashira,Kitowo,Kyala,,,,,Kibosho
 
Watanzania huwa mnanishangaza sana 😃 hapa mleta mada amesema tupeane update wilaya zenye baridi na linakuwa msimu upi sana.. lakini mwelekeo navyouona kila mtu atatetea wilaya zake hata kama imezidiwa na wilaya from nowhere 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Lushoto maeneo ya mbelei km unaenda Bumbuli baridi lake si mchezo, nilikaa siku 3 bila kuoga!!!!
 
Hili eneo zamani miaka ya 2000 mwanzoni nikiwa mdogo muda wote ukipita hapo haijalishi ni majira yapi kuna ukungu na baridi tu.

Maeneo kama Njombe yanakuwa na baridi kali msimu majira ya baridi zaidi ila hapo Uporoto ni mwaka mzima palikuwa panakuwa na baridi. Sina hakika kwa sasa pakoje.

Binafsi napenda sana kuishi maeneo yenye baridi.

Uporoto hadi sasa ipo hivyo hivyo, ikichagizwa na vimvua mvua vyepesi vile visivyo na ratiba...
 
Mimi nimefika Njombe, Makambako na Mafinga/Mufindi, bila kupepesa macho wala kujifikiria Mara mbili nakueleza wazi kwamba Mafinga/Mufindi inabaridi kuliko Njombe na Makambako
Hii nakuunga mkono mkuu
Nilipita na basi asubuhi pale kwenda Songea tukitokea Iringa. Basi lilisinama pale ili watu wakachimbe dawa. Aisee ile baridi sitakuja kuisahau,unaona kabisa baridi inapiga kwenye mfupa ndani tena hapo gari imefungwa vioo na nimevaa sweta zito
Sikuweza kutoka kwenda kuchimba dawa ingawa dereva alipiga mkwara hasimami mpaka Njombe
 
Kimsingi baridi linafanyika kitaifa hapa Makambako mwaka huu kiongozi hahahahhaah
Wakuu bila shaka ni wazima,

Mimi ni mtu naye penda sana kitu inaitwa hali ya hewa. Kuna jamaa anatoka Makete aliwahi nisimulia baridi ya huko. Nikasema isiwe kesi nikatinga msimu wa baridi mwaka jana. Aisee ni noma. Ila jamaa wamelizoea. Kama mgeni hutakaa urudi tena. So far nimetembelea.

1. MAKETE
2. NJOMBE
3. MAKAMBAKO.
Bado MUFINDI NASIKIA NAKO SI HABA.
Hii ni nyanda za juu kusini.

Hebu tupeane update wilaya zenye baridi na linakuwa msimu upi sana.

Nawasilisha.
 
Hii ni hali niliokutana nayo leo asubuh wakati natoka wilaya ya babati kuja hanangView attachment 1850662
Jorodomu au? Kindabi,Mwagitu,Balangda Lalu walau walau baridi inapungua kidogo. Ila ukanda wote wa barabara inayoelekea Singida mpaka Gehandu hadi Njiapanda Makiungu ni shidaaa. Nangwa,Endasaki mpaka kule Mureru ni tabu tupu. Huko Secheti,Gidagamond,Mulubadow n. k ni taabu tupu mpaka Gawal hadi Singida Vijijini ni tabu tupu. Naishi hapa Nangwa baridi lake sio la kitoto.

Saitaaaa khaigeeee[emoji13][emoji13][emoji13]
 
Back
Top Bottom