Eneo linalokua kwa kasi kibiashara mkoa wa Njombe

Mk boy

JF-Expert Member
Nov 3, 2020
2,293
1,706
HONGERA KWA MKOA WA NJOMBE KUBORESHA ENEO LA KIBIASHARA MAKAMBAKO ZONE Kwa kuweka centre zote taa za barabarani yaani makambako CBD ,wangingombe ,mtwango, igwachanya na ilembula hii zone ya biashara inayojumuisha Makambako tc, Wangingombe DC, na Njombe DC yaani kata ya Mtwango, Ikuna, Kichiwa, Ninga na Igongolo eneo hili lina tarafa nne Yani Makambako, Wang'ing'ombe, Imalinyi na Mdandu.Moja ya eneo linalokua kwa Kasi Sana makazi yameungana

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 ni eneo lenye watu 447000 plus zaidi ya nusu ya mkoa wa njombe kwa maana Hiyo ndo eneo lenye watu wengi zaidi mkoa wa njombe, jiografia ni eneo tambarare, hali ya hewa Lina ukanda wa joto na baridi kitovu chao ni makambako ukiwa makambako round about makambako mtwango ni km 24.

Na makambako to ilembula km 30 na makambako igwachanya via ikwete km 30 na ni eneo ambalo asilimia kubwa linatawaliwa na makazi na hii imechangiwa kuwa na main road tatu ambazo ni mbeya road ,iringa road ,na Songea road nini kifanyike kuliboresha zaidi ni kuongeza miundombinu kama vile Barabara mfano kuweka lami Barabara ya ikwete inayounganisha makambako, Ilembula na igwachanya pia itasaidia kuiunganisha na makete road kupitia igosi ambapo km zita pungua Sana.Itakuwa makambako igosi via igwachanya km 137 wakati kupitia njombe 167

Pia Kuna makambako mlowa hadi mgololo nayo itasaidia Sana hili eneo ikijengwa miundombinu hii kwa lami litaongeza Sana idadi ya watu pia kukamilika kwa mradi wa maji unaounganisha miji ya makambako na wangingombe utachochea zaidi ukuaji, pia mradi wa bandari kavu makambako, soko la mazao la kimataifa, viwanda, uwanja wa ndege ukikarabatiwa wa ilembula utachochea Sana ukuaji wa zone hii katika mkoa wa njombe na miradi yote ikitekelezwa utakuwa ni mji mkubwa Sana ukanda wa nyanda za juu kusini kulingana na jiografia.MAENEO mengi ya nyanda za juu kusini yameathiriwa na milima na mabonde na hifadhi za taifa na misitu ila eneo hili linatmbalale ya kutosha ime cover Halmashauri tatu makambako tc ,njombe dc na Wangingombe hii imepelekea kuungana kwa kihistoria ilikuwa wilaya moja zamani

Hongera kwa tanroad na TARURA naona tayari wameliona Hilo kwa kuweka street light taa za barabarani wangingombe ,ilembula ,igwachanya ,mtwango na makambako CBD pia na CRDB BANK kufungua matawi ilembula, igwachanya, mtwango hizo ni moja ya fursa na mashirika ya dini Yana fungua vyuo na hospitali za kutosha eneo hili Mfano hospitali ya ilembula ,ikelu na inuka zote zipo eneo hili na hii imefanya katikati ya mji wa makambako kuchangamka zaidi maana ndo soko linalo supply mahitaji kwenye masoko hayo madogo.
Makazi yanazidi kuwa well organised kutokana na Kasi ya ukuaji
IMG-20230416-WA0004~2.jpg
IMG-20230416-WA0004.jpg
FB_IMG_16728517915595809.jpg
FB_IMG_16755156315245458.jpg
thumb_584_1130x480_0_0_auto.jpg
FB_IMG_16765236115613910.jpg
 
Kitu pekee kinachokuwa kwa kasi njombe ni maambukizi ya VVU na kushindana na Geita kujibu matukio
NJOMBE: MKOA UNAOKUWA KWA KASI ZAIDI KIUCHUMI TANZANIA

Mkoa wa Njombe Unaweza kuuita Duma wa Tanzania, kutokana na Kasi kubwa ya ukuaji unaofananishwa na nchi za Kusini mashariki ya mbali ya Asia kama Malaysia, Singapore na Taiwan.

Mkoa wa Njombe uchumi umekuwa ukikuwa kwa asilimia 63 katika kipindi Cha miaka minne iliyopita. Sekta zinazokuwa kwa Kasi zaidi ni kilimo Cha Asili Cha mkoa huo kinachohusisha mazao makuu kama Chai, Mahindi, Maharage na Viazi kimekuwa kwa asilimia 15. Pia kilimo Cha misitu na biashara ya mazao ya misitu hasa nguzo na mbao ni mhimili wa uchumi wa mkoa na umeajiri watu wengi.

Biashara ndogo ndogo na za Kati (SMEs) zinaongezeka Sana katika miji ya Njombe, Makambako na Halmashauri ya Njombe DC. Kilimo bustani Cha mboga mboga na matunda kimepata mwamko Mpya na kushuhudia ukuaji wa hali ya juu hasa kilimo Cha matunda aina ya Parachichi ambacho kinawaingizia mamilioni wakulima wa Njombe.

Pato la Njombe (GDP) limefikia shilingi trioni 2.66 na Pato la mtu mmoja mmoja ni Tsh. Milioni 3.3 kwa mwaka. Halmashauri zenye wananchi wenye vipato vya juu ni Makambako (7m), Njombe Mjini (5.6m) na Njombe DC (3.2m). Njombe ndio mkoa wenye maskini wachache zaidi, idadi yao ni watu 110,000 tu.

Hata hivyo Kasi ya ukuaji inatarajia Kuongezeka zaidi kutokana na uwekezaji katika kilimo bustani, chuma, umeme wa Maji, Barabara za lami na reli ya kisasa (SGR) kwenda Mtwara.

Mikoa mingine inayokuwa kwa Kasi ni Pwani, Dodoma, Katavi na Mwanza. Pwani imekuwa kitovu Cha viwanda na Utalii pamoja na biashara na ukuaji wa miji. Dodoma, makao makuu yameongeza idadi ya watu, uwekezaji katika makazi, shughuli za kiserikali, mahoteli na burudani. Katavi, imekuwa kitovu kipya Cha Utalii na biashara katika ukanda wa Ziwa Tanganyika. Ukaribu wake na nchi za DRC na Zambia zimeongeza fursa ya kibiashara. Mwanza inarudi kuwa kitovu Cha biashara katika eneo la maziwa makuu. Pamoja na mambo mengine imechochewa na uwekezaji katika miundombinu hasa uwanja wa ndege, ujenzi wa meli Mpya na ujenzi wa reli ya kisasa, ukuaji wa idadi ya watu na uwekezaji katika viwanda na mahoteli ambapo Pato la mkoa wa Mwanza limefikia takribani trioni 11 kutoka trioni 2.5 miaka michache iliyopita.
 
Hii ni kutokana na ukongwe wa hospitali hii pia ongezeko la watu kwenye zone ya makambako imepelekea kuanza kuikarabati zaidi hii hospitali ili iwe ya rufaa
FB_IMG_16798543723498106.jpg
FB_IMG_16800052212294279.jpg
FB_IMG_16822408321742322.jpg
FB_IMG_16822413082025307.jpg
FB_IMG_16822409511827903.jpg
 
Maeneo ya starehe Yanazidi kuongezeka watu wanatumia fursa ya ongezeko la watu
FB_IMG_16710685737414787.jpg
FB_IMG_16710685398166314.jpg

FB_IMG_16721148802993430.jpg

FB_IMG_16721148704611080.jpg

FB_IMG_16765221828150145.jpg
FB_IMG_16720411105198959.jpg
FB_IMG_16720411392622736.jpg
FB_IMG_16718394361224932.jpg
FB_IMG_16720410736656070.jpg
FB_IMG_16718081492893228.jpg
FB_IMG_16721134174282919.jpg

FB_IMG_16724044258288294.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_16765221828150145.jpg
    FB_IMG_16765221828150145.jpg
    34 KB · Views: 24
Makampuni ya vifaa vya ujenzi nk yanatumia fursa ya eneo hili ujenzi upo Kasi sana
FB_IMG_16727495359454879.jpg
 
Ujenzi wa vyuo vya afya hospitali za ilembula kinafanya kazi ikelu hospitali kazi inaendelea fursa
FB_IMG_16822413082025307.jpg
istituto_03.jpg
istituto_04.jpg
istituto_02.jpg
 
Back
Top Bottom