Wilaya zenye baridi sana Tanzania

Wilaya zenye baridi sana Tanzania

Nadhani Njombe inaongoza aisee, ile wilaya karibia kila mahali unapogusa ni baridi hatariii

Halafu inafuatia Mufindi, bwana we kule ndio unakunywa chai ya moto bila kujua, muda wote kuna maukungu hata wakati mwingine huoni mita 5 mbele...

Kuna wilaya ya Rungwe, haswa maeneo ya Uporoto kwa Wasafwa, noma sana kule

Halafu kuna Arumeru, kule juu juu kule kama unaukaribia mlima, kuna vijiji vina baridi kule hatari...

Mwisho kuna Lushoto na Muheza, hizi baridi zake nimeweza kuzivumilia walau hata kwa kuvaa tshirt inawezekana...

Huwa nasikia na Rombo inasifiwa lakini sijawahi fika huko

Hizo sehemu tatu za juu ni kawaida sana asubuhi kukuta umande wa theluji
Good observation mkuu. Lushoto nako naona kunapata credit
 
Wakuu bila shaka ni wazima,

Mimi ni mtu naye penda sana kitu inaitwa hali ya hewa. Kuna jamaa anatoka Makete aliwahi nisimulia baridi ya huko. Nikasema isiwe kesi nikatinga msimu wa baridi mwaka jana. Aisee ni noma. Ila jamaa wamelizoea. Kama mgeni hutakaa urudi tena. So far nimetembelea.

1. MAKETE
2. NJOMBE
3. MAKAMBAKO.
Bado MUFINDI NASIKIA NAKO SI HABA.
Hii ni nyanda za juu kusini.

Hebu tupeane update wilaya zenye baridi na linakuwa msimu upi sana.

Nawasilisha.
Mimi nimefika Njombe, Makambako na Mafinga/Mufindi, bila kupepesa macho wala kujifikiria Mara mbili nakueleza wazi kwamba Mafinga/Mufindi inabaridi kuliko Njombe na Makambako
 
Back
Top Bottom