Wilaya zenye baridi sana Tanzania

Wilaya zenye baridi sana Tanzania

Wakuu bila shaka ni wazima,

Mimi ni mtu naye penda sana kitu inaitwa hali ya hewa. Kuna jamaa anatoka Makete aliwahi nisimulia baridi ya huko. Nikasema isiwe kesi nikatinga msimu wa baridi mwaka jana. Aisee ni noma. Ila jamaa wamelizoea. Kama mgeni hutakaa urudi tena. So far nimetembelea.

1. MAKETE
2. NJOMBE
3. MAKAMBAKO.
Bado MUFINDI NASIKIA NAKO SI HABA.
Hii ni nyanda za juu kusini.

Hebu tupeane update wilaya zenye baridi na linakuwa msimu upi sana.

Nawasilisha.
Mufundi kuna mwaka nilienda kuna baridi mpaka barafu inakuwepo sijui kwa siku hizi halafu kuna
Kateshi
Karatu
Machame sehemu moja inaitwa kialya kule ni balaa
 
Kuna wilaya ya Rungwe, haswa maeneo ya Uporoto kwa Wasafwa, noma sana kule
Hili eneo zamani miaka ya 2000 mwanzoni nikiwa mdogo muda wote ukipita hapo haijalishi ni majira yapi kuna ukungu na baridi tu.

Maeneo kama Njombe yanakuwa na baridi kali msimu majira ya baridi zaidi ila hapo Uporoto ni mwaka mzima palikuwa panakuwa na baridi. Sina hakika kwa sasa pakoje.

Binafsi napenda sana kuishi maeneo yenye baridi.
 
Ww kama mm. Nataka nitafute chimbo zuri hata katesh huko.
 
Back
Top Bottom