Wilaya zenye baridi sana Tanzania

Wilaya zenye baridi sana Tanzania

Nadhani Njombe inaongoza aisee, ile wilaya karibia kila mahali unapogusa ni baridi hatariii

Halafu inafuatia Mufindi, bwana we kule ndio unakunywa chai ya moto bila kujua, muda wote kuna maukungu hata wakati mwingine huoni mita 5 mbele...

Kuna wilaya ya Rungwe, haswa maeneo ya Uporoto kwa Wasafwa, noma sana kule

Halafu kuna Arumeru, kule juu juu kule kama unaukaribia mlima, kuna vijiji vina baridi kule hatari...

Mwisho kuna Lushoto na Muheza, hizi baridi zake nimeweza kuzivumilia walau hata kwa kuvaa tshirt inawezekana...

Huwa nasikia na Rombo inasifiwa lakini sijawahi fika huko

Hizo sehemu tatu za juu ni kawaida sana asubuhi kukuta umande wa theluji
 
Back
Top Bottom