Wilaya zenye baridi sana Tanzania

MKOA WA KILIMANJARO BARIDI LIMESIMAMA. Yaani upepo/hewa haitembei kubabake ukipanda pikipiki au gari au ukitembea wewe ndiye unaukata upepo. Ni balaa kuanzia mwezi mei hadi septemba. Ngara, mafinga, njombe kuna baridi kali ila hewa inatembea. Lushoto napo ni balaa. Arusha na kilimanjaro kuna baridi nadhani 60% ya tanzania. Kigali napo si haba.
 
Korogwe...msambiazi...unaenda juuu unapita lutindi..kna sehem inaitwa masange huko si mchezo

Ova
 
Wakuu bila shaka ni wazima,

Mimi ni mtu naye penda sana kitu inaitwa hali ya hewa. Kuna jamaa anatoka Makete aliwahi nisimulia baridi ya huko. Nikasema isiwe kesi nikatinga msimu wa baridi mwaka jana. Aisee ni noma. Ila jamaa wamelizoea. Kama mgeni hutakaa urudi tena. So far nimetembelea.

1. MAKETE
2. NJOMBE
3. MAKAMBAKO.
Bado MUFINDI NASIKIA NAKO SI HABA.
Hii ni nyanda za juu kusini.

Hebu tupeane update wilaya zenye baridi na linakuwa msimu upi sana.

Nawasilisha.
Umeisahau wilaya ya ILALA kuna nyahenge ya kufa mtu kunguru haruki
 
Back
Top Bottom