Josephine
JF-Expert Member
- Sep 5, 2010
- 786
- 812
sikujua first lady wa CDM ulikuwa unasurpote ile mada ya Exaud Mamuya na kuchochea mgogoro ndani ya Chama?
kwanza nimekosea neno moja nakubali makosa,japo kwakuwa na majukumu hata kiswahili naweza kosea.
siyokwamba ninaunga mkono au kutokuunga mkono,japo napitia nakusoma mambo mengi yaliyopo humu.
shida yangu ni moja tu siwezi kuchangia.
nimenena hivyo kwakuwa najua kunapokuwa na jambo mwisho mashambulizi yatakuwa kwa Dr.
Japo inawapaasa kujua tunafurahia,na ninafurahi mnapomkosoa.kwangu mimi mnanipa nini na wapi natakiwa kumsihi Mungu amtengeneze na kumfinyanga ili aifanye kazi yake vema.
Ndugu zangu kuongoza Watu wenye upeo tofauti,na mawazo ambayo bado yanakuwa si kazi rahisi.ndani na nje ya mazingira aliyomo.
Lakini pamoja na yote hayo,yeye ni mwanadamu,yote aliyoyafanya ni kwa uwezo wa Mungu.
Naomba muendelee na mjadala,Josephine ataendelea kusoma yote yanayoandikwa.
Kila mmoja yuko sahihi kwakuwa anaandika kile kilichomo moyoni mwake.
Ndugu yangu yuko sawa.