Who really killed Prof. Mwaikusa?

Who really killed Prof. Mwaikusa?

Mkuu,

Mie siwahukumu hao jamaa na wala sijasoma makala nzima maana naona Kidhungudhungu leo.

Point yangu ilikuwa ni kwamba, Wakatoliki ni kama watu wengine. Kwenye kundi la Kondoo, na Chui wamo. Na kwenye kundi la Chui, na Kondoo pia wamo. Wewe maelezo yako yanawapa hawa jamaa 100% kuwa ni watakatifu na unaweka sheria na mistari kibao kuwa HAWAWEZI.

Narudia tena, mie siwahukumu na hakuna sehemu nimesema kuwa JAMAA WANA MAKOSA. Ila kama Papa mwenyewe alikuwa akishirikiana na Hitler, itakuwa hao wengine? Point yangu ni moja, LOLOTE LILIWEZA KUTOKEA. Wanaweza kuwa ni MAFIA kweli au WAMESINGIZIWA.

Usalama wa Taifa upi unaoongelea? Na mwanasheria mwenyewe ndiyo huyo WEREMA kila siku anapewa shule na Tundu Lissu. Vyombo vyote vya usalama wa Taifa, maboss wake wameteuliwa na yule mwenye jina gani sijui? Ngoja nimuulize John Mnyika........

Kama ungesoma mabandiko yangu hapa utakuja kuelewa kwamba sijajenga utetezi wo wote, ila nimesimama kwenye ukweli kwamba kwa tuhuma na maelezo ya makala ya gazeti, hali kadhalika walio karibu na shirika hilo na kujua yanayojilia wameeleza bayana hapa kwamba:

Kuna mwanashirika mmoja mtajwa katika makala ile alikuwa anafanya mambo kwa siri katika mgodi huo na alipokuja gundulika na shirika na pia kugundulia ameliibia shirika pesa, alishtakiwa na kuwa rejected shirikani kwa kufukuzwa.

Aliposhtakiwa alifungwa, baada ya kutumikia kifungo cha ndani, sasa anatumikia kifungo cha nje. Kwa maana hiyo hawezi tena kurudi shirikani na hata mipango yake ya siri aliyokuwa anaifanya kwenye migodi ile imeshaota mbawa kwa vile alikuwa anafanya kwa kutumia kivuli cha shirika.

Inasemekana baada ya kumpata hayo aliapa kuliadabisha shirika lake kwa kulichafua kama kulipiza kisasi kwa kufukuzwa utawa, na ndicho alichokifanya.

Nimekua nashikilia msimano wangu tangu awali kutokana na uelewa wangu wa mashirika haya na taasisi zake katika kanisa hili, utaratibu unaosemwa katu hauwezi kufanywa na shirika kisheria kwa sababu mradi mkubwa kama ule huasisiwa na kukubaliwa na makao makuu na ndiyo yenye kuuendesha na kugharimia.

Mikataba katika shughuli za uchumi kama hizi haiwezi kufanya tu na kila mwanashirika, ila hufanywa na procurator wa shirika mwenye mamlaka katika mambo ya mikataba na mambo ya uchumi wa monasteri. Hata ingekuwa jimboni kuna procurator wa jimbo anayeshughulikia mambo ya mikataba na matumizi ya pesa, si kila mwanashirika au muumini, na hili walijua na linafahamika si katika mashirika ya dini tu hata taasisi ye yote.

Makala ya gazeti la Raia mwema halijaonyesha waliotia sahihi wadhifa wao, na kwa kuulizia wahusika sisi wengine tunaowafahamu hao wawili hawana nyadhifa za uprocurator wala ukubwa wa shirika, hivyo kwa hoja hiyo na kadiri ya sheria zao shirika halihusiki ila hao wawili personally ndio wanaotakiwa kubeba mzigo na shirika lilishamtema mmojawapo baada ya kugundua madudu aliyoyafanya.

Kwamba mipango ya kumwua Mwaikusa ilifanyika ndani ya Abatia ya Peramiho, hilo jambo zito, maana kama ni kweli Abasia ilifanya hayo dondoo za mikutano yao ya shirika itaonyesha lini na kwa namna gani walifanya kikao chao na theluthi mbili ya wajumbe wa mkutano kurithia kupanga na kutekeleza mauaji hayo. Je, hilo lawezekana?

Kwa taratibu zao za kishirika wana mikutano ifuatayo katika kutekeleza majukumu mazito katika shirika kama ifutatavyo:

  • Senioratus (halmashauri kuu/kamati kuu ya shirika)
  • Mkutano mkuu wa shirika unaowakutanisha wanashirka wote.
  • Mikutano yote huwa na dondoo za mikutano na kumbukumbu za mikutano na mada zilizojadiliwa hutunzwa.
Kwa siyejua mfumo wa shughuli za mashirika haya rahisi sana kuingia kichwa kichwa kufikiria hivyo, lakini kwa sisi tunaofahamu na ambao tumekuwa karibu zaidi katika maisha yao kila siku jambo hilo haliwezekani, labda mtu fulani binafsi kwa siri afanye hivyo kwa sababu zake binafsi au kuingiliwa na yule mwovu kama Yuda Ikariote alivyomwuza Yesu kwa vipande thelathini vya fedha haikuwa jopo la mitume wote, ila Yuda alitoroka kwenda kufanya mipango kwa siri na wauaji.

Mimi sijatetea hilo, ila kwa mapungufu kadhaa yaliyojitokeza katika gazeti hilo kwa ujumla inaonekana ni mtu fulani binafsi ambaye alikuwa mwanashirika amehusika na ndiye anayetakiwa kuwajibishwa, la sivyo kama ni shirika limehusika uchunguzi wa wazi ufanyike na hata gazeti litume mwandishi wake kwenda kupata ukweli, si kuandika kitu bila uthibitisho wa pande zote zinazohusika. Huu ndio msimamo wangu mdau
Sikonge.
 
Kila siku watu wanasuka habari mpya ili biashara inogeeeee..
 
Kwanza kabisa nikuambie unajua kidogo sana kuhusu Kanisa Katoliki licha ya kuwa wewe ni muumini walo. Pili unachokiongea hapo juu ni "ideal situation" tu, eti mpaka sijui theluthi mbili ikae ndio itoe maamuzi. Hiyo hai-apply pale ambapo kuna uhalifu wa aina yoyote ile unapotendeka. Maamuzi yanakuwa ni angalau kwa mtu mmoja au watu wachache sana "inner circle". Bado hujasema kwa nini unaamini kwa uhakika kabisa kwamba wao jamaa watawa hawawezi kuhusika na kifo cha Prof. Nimekwambia usome tu hicho kitabu cha David Yallop kuhusu tuhuma za Vatican kuhusika na kifo cha Papa John Paul I ambaye alikuwa amedhamiria kuisafisha Vatican dhidi ya uchafu uliokuwa umekithiri.

Candid Scope, bado unahitaji kulijua na kulifahamu zaidi Kanisa Katoliki, nje ya maswala ya ibada/misa, liturjia na mambo ya sala kanisani.

wengine wamo kazini hao kutetea uhalifu lakini bahati mbaya ni karne nyengine hii
 
wengine wamo kazini hao kutetea uhalifu lakini bahati mbaya ni karne nyengine hii

100_2148.jpg

Uwongo mwingine wa Gazeti la Raia mwema ni huu hapa.
Katika makala yake limesema mkuu wa shirila hilo la Peramiho ni Atabe Lambert Dorr OSB, ni wongo na hili ni uhakikisho kwamba hawafanyi uchunguzi wa kina katika mada zao kabla ya publication.

Wakati anafariki Mwaikusa, Abate Lambert Dorr OSB alishastaafu, ni mzee wa kutunza tu shirikani. Mkubwa wa sasa katika shirika hilo ni Abate Anastas OSB ambaye picha yake ipo hapo juu mwenye kofia ya kiaskofu, ila yeye si askofu bali wadhifa wake ni kama wa askofu ndio maana anavaa nguo kama hizo awapo katika maadhimisho ya liturjia.

A%2Bformer%2Bpresident%2BBenjamin%2BWilliam%2BMkapa%252C%2BArchbishop%2BNorbert%2BMtega%252C%2BAbbot%2BThadeus%2BMhagama%2Band%2BPrior%2BOddo%2BNanyanje%2BOSB%255B1%255D..JPG

Askofu Mkuu Mtega akiwa kushoto kwa Ben Mkapa
Hanga - Songea, Mkoani Ruvuma

Labda Askofu Mkuu wa Songea, Mhashamu Askofu Mkuu Norbert Mtega ataweza kutolea ufafanuzi kwa vile na watu walio katika himaya ya jimbo lake.
 
ABASIA YA PERAMIHO YAKANUSHA KUHUSIKA KATIKA MAUAJI YA PROFESA JWAN MWAIKUSA

Na Mwandishi Wetu, Songea

Shirika la Wabenediktini la Peramiho limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti la Raia mwema la tarehe 7 mwezi Novemba mwaka huu kuhusiana na tuhuma za kifo cha Profesa Jwan Mwaikusa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alhamisi ya wiki iliyopita , Msaidizi wa Abate P.Fidelis Mligo OSB, ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria(LLB), alisema kuwa Abasia ya Peramiho imesikitishwa sana na taarifa hizo ambazo ni za uzushi,uongo, na zisizo na ukweli, zinazoleta uchochezi na fitina katika jamii, ambazo zimeandikwa na gazeti hilo la kila wiki nchini, lenye kichwa cha habari kilichosomeka "Mapya yaibuka mauaji ya Profesa Jwan Mwaikusa".

"Kuhusu Abasia kuhusika na mauaji ya Mwaikusa ni jambo la kijinai, ambalo sisi kama Abasia hatuna mamlaka ya kulisemea na hatulijui. Tujuavyo, huo ni uzushi na uwongo usio na chembe ya ukweli. Lengo msingi hapa ni kutaka kuipaka taasisi yetu ya kidini matope ya bandia mbele ya jamii. Huu ni mkakati wa mtoa habari hiyo wa kulipa kisasi dhidi ya jamii yetu ya Abasia, baada ya kufukuzwa utawa na kufungwa gerezani kwa sababu ya wizi wa mamilioni ya fedha za Abasia ya Peramiho na udanganyifu mwingine," alisema P.Fidelis Mligo OSB. Pamoja na mambo mengine, P. Mligo alishangaa: Je ni kwanini mwandishi wa habari hii ameficha jina lake (identity)?

Ni kwanini pia mtoa habari naye ameficha jina lake? Maana yake hawa wote wawili wanajua toka mwanzoni kuwa wanaandika uzushi na uongo, ndiyo maana wanaficha identity zao. Lakini tutakapolifikisha gazeti hili mahakamani lazima watajitokeza kwa hiari yao. Hili lazima lifanyike. Pia nashangaa sana kama kweli chanzo cha habari hizi kina ushahidi wa jinai hiyo, kwanini kisiupeleke polisi ambao ndio wenye mamlaka kisheria ya kufanya upelelezi? Je ni kuanzia lini gazeti ni kituo cha polisi? Je ni kuanzia lini gazeti ni mahakama yenye uwezo wa kumtia mtu hatiani? Wacha waendelea kuandika ili gazeti liuzike".

Kwa mujibu wa Pd. Mligo ni kwamba mtoaji wa habari hiyo kwa namana yoyote ile ni Bw. Nestory Mhuwa(kwasababu alishawatangazia watu kuwa atahakikisha anaichafua Abasia Peramiho ili kulipa kisasi) ambaye aliwahi kuwa mtawa wa shirika hilo, akijulikana kwa jina la Br. Aidan OSB ambapo baadaye aliachishwa utawa kwa kuwa alikwenda kinyume na taratibu, kanuni,sheria na maadili ya kitawa ya shirika husika ambapo baadaye alishtakiwa kwa kosa la wizi la mamilioni ya shilingi ambazo ni mali ya shirika hilo. Hatimaye akatiwa hatiani na mahakama ya hakimu mkazi ya Songea.

"Niseme machache juu ya kuhusika kwa Abasia Peramiho katika kampuni ya UMICO Ltd: Abasia ya Peramiho kuanzia miaka ya 1990 ilikuwa ni mwanahisa katika kampuni ya UMICO Ltd.

Kampuni hii ilikuwa ikijihusisha na uchimbaji madini huko Lukarasi wilayani Mbinga mkoani Ruvuma. Abasia ilikuwa na hisa kubwa (majority shareholder). Wanahisa wengine walikuwa ni Bw. Johnson Nchimbi, Bw.Mathew , Barnabas na wengine."

Alisema kuwa mwanzoni kabisa, hisa zao zilishikiliwa na Bw.Johnson (in trust). Baadaye hisa hizo zikahamishiwa kwa baadhi ya watawa wenzao kama wadhamini (in trust), mmojawapo alikuwa ni Nestory Mhuwa(ex bro. Aidan). Huyu ndiye aliyekuwa Mkurugenzi na baadaye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo. Mara zote Nestory Mhuwa (ex Br.Aidan) alitoa sababu mbalimbali za visingizio vya kutoleta ripoti hiyo kwa Abasia(principal owner of shares).

"Mara moja aliwahi kuleta taarifa kwenye mkutano wetu kwa maneno tu (kiblabla), alipobanwa na wajumbe wa mkutano huo juu ya mradi huo na matatizo yake, alisema matatizo ya mradi huu yataisha ndani ya miezi miwili. Baada ya kupita miezi hiyo miwili hakuleta ripoti yoyote mpaka leo. Muda mwingi alikuwa hapatikani utawani hapa Abasiani kwa kisingizio cha kushughulika na UMICO," alifanunua Pd. Fidelis OSB.

Alisema baada ya kuona hatujui kinachoendelea katika kampuni hiyo na huyu mdhamini (trustee) wetu katika kampuni hii Mr. Nestory Mhuwa (ex bro.Aidan) haaminiki na siyo muwazi katika utendaji wake; kwa mkutano rasmi wa Baraza letu, pamoja na mambo mengine tuliamua kuwa lazima tujitoe katika kampuni hiyo kwa kuuza hisa(shares)kwa sababu hatuoni faida yake na hatupati ripoti.

Pili, hisa(shares) alizokuwa akizimiliki ex Br. Aidan kwa niaba ya Abasia katika kampuni hiyo zihamishiwe kwa watawa wengine ili kukamilisha mpango wetu msingi wa kujitoa katika kampuni hiyo. Kazi hiyo ilitekelezwa vizuri kwa kuhamisha hisa hizo toka kwa Nestory Mhuwa(ex br.Aidan) kwa mujibu wa sheria.

Mwaka 2010 Abasia ya Peramiho ilijitoa rasmi katika kampuni hiyo kwa kuuza hiza zake zote kwa mujibu wa taratibu na sheria za makapuni. Hivyo basi, kwa tendo hilo la kisheria, Abasia ya Peramiho siyo mwanahisa wa kampuni ya UMICO, na haina maslahi ya aina yoyote ile katika kampuni hiyo.

P. Mligo alizidi kusisitiza kuwa taarifa nyingi za UMICO zilizomo katika gazeti ni za zamani, na nyingine ni za kupikwa. Huyu Nestory (ex Br.Aidan) kipindi hicho alishika(mdhamini) hisa hizo kama mtawa. Kwa mujibu wa sheria ya Kanisa mtawa haruhusiwi kuwa na mali binafsi. Hivyo umiliki wa Abasia ya Peramiho wa hisa hizo kupitia kwa watawa hao na watu wengine haukuwa wa siri, haikuwapo sababu ya msingi ya uwepo wa siri hizo, ndiyo maana yeye ana nyaraka za kuhamisha hisa mbalimbali.

"Hakuna mtu aliyewahi kuja hapa Abasia Peramiho na kudai kupewa maelezo juu ya Abasia kuwa na hisa katika kampuni ya UMICO, na akanyimwa haki hiyo ya kupata habari. Vinginevyo hiyo inabaki ni tafsiri yake mgando na umbumbumbu wa sheria za makampuni. Abasia ya Peramiho kama mtu asiye wa kawaida(legal entity- Artificial person) anafanya kazi kupitia watu halisia(natural persons). Watu halisia hao ndio walioshika hisa kwa udhamini(in trust) kwa niaba ya Abasia Peramiho, akiwemo Nestory mhuwa (ex Br.Aidan). Basi, tuseme siri hiyo anayoisemea imewekwa na sheria.

Pamoja na hayo, Mr.Nestory Mhuwa(ex Bro.Aidan) kwa udanganyifu wake, na kukosa fadhila ya uaminifu aliweza kuiibia Abasia ya Peramiho mamilioni ya fedha, ambazo zililenga kutumika katika huduma mbalimbali za kijamii hapa Peramiho.

Hivyo, Mwezi Januari 2012, Mr. Nestory Mhuwa (ex br. Aidan) alitiwa hatiani(convicted) na mahakama ya hakimu makazi Songea kwa kosa la wizi wa mamilioni hayo ya fedha za Abasia Peramiho(Benedictine Fathers of Peramiho). Mpaka sasa bado anatumikia adhabu hiyo ya kifungo".

Aidha Pd. Mligo alihitimisha kusema kuwa Bw. Nestory(ex Bro.Aidan) ameshaachishwa utawa kwa mujibu wa sheria na taratibu za kanisa. Hivyo, si mtawa tena wa Abasia Peramiho, hana uhusiano wa kimaslahi na Abasia ya Peramiho.
 
Ninaona mnajaribu kutuondoa kwenye ukweli na kutuaminisha ya kuwa watu hawa hawawezi kukosea. Kanisani pia kuna mbwa mwitu wamejipenyeza. Jana nimekuwepo Peramiho kupima upepo watawa wengi wamefurahia habari hii kuanikwa ijapokuwa hawapendi kujionyesha maana boss msaidizi wa shirika buluda fr fidelis mligo akijua anakuwajibisha kwa kukutafutia sababu ya kufukuzwa, au anakuhamisha makazi au hata kukumwang..i kwa kumtumia Kamh...a. ndiyo maana katoa mil 5 kwa press club baada tu ya kuua prof na gazeti la raia mwema lilipoandikamajuzi kawapa zingine mil5. watawa wamalalamika hali kiuchumi imekuwa ngumu kisa anahonga hela kuwamaliza wenzie wenye uadilifu.

Baadhi ya wenzetu ktk kanisa jirani, kila anapokuja buluda fidelis mulugo kusalisha wanaondoka kurudi makwao kwa kuwa tunaona chui katuingilia asije akameza na wasiohusika. mtu huyu anatisha eti. Kamtesa buluda mhuwa na watu wa songea hasa peramiho tuna hasila naye. Amemhonga mil 30 hakimu ili atimize, tumekaa kumlilia mungu, si bola angewapa watoto yatima apate thawabu kulikokumwonea mnyonge na mtetezi wa watu.

Watawa wamenieleza kuwa bado wanamlilia buluda mhuwa maana ndiye aliyekuwa mtetezi wao na alikuwa bosi msaidizi nafasi ambayo inaonekana ndiyo kaifanyia vituko na kwa sasa kaikalia yeye. tunaomba gazeti hili lije kutuhoji sisi watu majirani zao, tutawambia mengi maana watu hawa wanapotezwa mwelekeo na buluda fidelis mligo. wale mlioko dar na mliopata nakala ya leo tujulisheni kumewekwa nini na raia mwema. ngoja nipige simu kwa walioko bongo. Buluda fidelis kama utwa umekushinda waachie wenzio kuliko kuleta umafia kanisani, hadi unapokuja kutusalisha tunashindwa kufuatilia ibada, maana chui na kondoo wapi na wapi.
 
kamajuzi

Moja ya mafanikio ya habari ni kuibua mjadala wenye kufichua kilichofichika na katika hili Raia Mwema imefanikiwa sana, sasa tunapata mengi yaliyofichika huko.

Kuna mchangiaji hapa kazi kubwa ni kurudia majibu yake katika kila hoja zinazotolewa na wachangiaji wengine, hatukatai kuwatetea lakini sio kutonyesha kuwa hao jamaa ni wasafi 100pc.

Nashangaa maelezo ya watetezi wakipindisha maelezo, hakuna sehemu ambayo huyo Mzungu ametuhumiwa kwenye hiyo article, bali ameonyeshwa kuwa akiwa kiongozi aliwaelekeza bodi ya wakurugenzi kutofanya lolote lile linalohusu huo mgodi bila kushauriana na Marehemu Prof Mwaikusa ambaye alikuwa mwanasheria wao.

Tunashukuru wengine mnatupa yaliyopo huko ndani ambayo jamii haikuyafahamu..
 
Last edited by a moderator:
100_2148.jpg

Uwongo mwingine wa Gazeti la Raia mwema ni huu hapa.
Katika makala yake limesema mkuu wa shirila hilo la Peramiho ni Atabe Lambert Dorr OSB, ni wongo na hili ni uhakikisho kwamba hawafanyi uchunguzi wa kina katika mada zao kabla ya publication.

Wakati anafariki Mwaikusa, Abate Lambert Dorr OSB alishastaafu, ni mzee wa kutunza tu shirikani. Mkubwa wa sasa katika shirika hilo ni Abate Anastas OSB ambaye picha yake ipo hapo juu mwenye kofia ya kiaskofu, ila yeye si askofu bali wadhifa wake ni kama wa askofu ndio maana anavaa nguo kama hizo awapo katika maadhimisho ya liturjia.

A%2Bformer%2Bpresident%2BBenjamin%2BWilliam%2BMkapa%252C%2BArchbishop%2BNorbert%2BMtega%252C%2BAbbot%2BThadeus%2BMhagama%2Band%2BPrior%2BOddo%2BNanyanje%2BOSB%255B1%255D..JPG

Askofu Mkuu Mtega akiwa kushoto kwa Ben Mkapa
Hanga - Songea, Mkoani Ruvuma

Labda Askofu Mkuu wa Songea, Mhashamu Askofu Mkuu Norbert Mtega ataweza kutolea ufafanuzi kwa vile na watu walio katika himaya ya jimbo lake.

KAMAJUZI KATUMWAGIA VITU HIVI , WEWE ENDELEA KUTETEA

Ninaona mnajaribu kutuondoa kwenye ukweli na kutuaminisha ya kuwa watu hawa hawawezi kukosea.

kanisani pia kuna mbwa mwitu wamejipenyeza.

jana nimekuwepo Peramiho kupima upepo watawa wengi wamefurahia habari hii kuanikwa ijapokuwa hawapendi kujionyesha maana boss msaidizi wa shirika buluda fr fidelis mligo akijua anakuwajibisha kwa kukutafutia sababu ya kufukuzwa, au anakuhamisha makazi au hata kukumwang..i kwa kumtumia Kamh...a. ndiyo maana katoa mil 5 kwa press club baada tu ya kuua prof na gazeti la raia mwema lilipoandikamajuzi kawapa zingine mil5. watawa wamalalamika hali kiuchumi imekuwa ngumu kisa anahonga hela kuwamaliza wenzie wenye uadilifu.

baadhi ya wenzetu ktk kanisa jirani, kila anapokuja buluda fidelis mulugo kusalisha wanaondoka kurudi makwao kwa kuwa tunaona chui katuingilia asije akameza na wasiohusika. mtu huyu anatisha eti.

Kamtesa buluda mhuwa na watu wa songea hasa peramiho tuna hasila naye. Amemhonga mil 30 hakimu ili atimize, tumekaa kumlilia mungu, si bola angewapa watoto yatima apate thawabu kulikokumwonea mnyonge na mtetezi wa watu. watawa wamenieleza kuwa bado wanamlilia buluda mhuwa maana ndiye aliyekuwa mtetezi wao na alikuwa bosi msaidizi nafasi ambayo inaonekana ndiyo kaifanyia vituko na kwa sasa kaikalia yeye.

tunaomba gazeti hili lije kutuhoji sisi watu majirani zao, tutawambia mengi maana watu hawa wanapotezwa mwelekeo na buluda fidelis mligo. wale mlioko dar na mliopata nakala ya leo tujulisheni kumewekwa nini na raia mwema.

ngoja nipige simu kwa walioko bongo. Buluda fidelis kama utwa umekushinda waachie wenzio kuliko kuleta umafia kanisani, hadi unapokuja kutusalisha tunashindwa kufuatilia ibada, maana chui na kondoo wapi na wapi.
 
Nawe Ibambasi nikupe pole kwani unajadiliana na mtu unayefahamu kwa jina hapa JF bila kumjua upeo wake. Ndio maana hata Zawadi ameongea uwongo kuhusu Dr. Ansgar OSB kumbe mie najua hata wadhifa alio nao na kwamba aliletwa Peramiho na shirika kuzoea mazingira ya nchi za misioni ili napokabidhiwa jukumu zito la management ya uchumi wa shirika katika ulimwengu mzima awe anajua mazingira ya nchi hizo yalivyo.

Labda nikuambie kuchukua nukuru ya kitabu fulani na kuwa kielelezo ni sawa na haya ya Gazeti la Raia mwema lisilofanya utafiti wa kina wala kuwahusisha watu waliowatuhumu ilivyo kawaida ya uhakiki wa wahariri, na katika toleo lao hilo katika habari hii hawakueleza cho chote kuwauliza wahusika ilivyo ada ya uandishi hapo ndipo unapoweza kuona udhaifu unaoukingia kifua katika fani ya habari na uhariri uliotukuka katika kutoa publication zenye kupata heshima stahiki.

Jaribu kusoma historia ya kanisa kuanzia Mtume Petro alipokabidhiwa funguo, jaribu kuelewa teologia, sheria (Canon Law) na kanuni nyingine. Sitaki nikueleze kiwango nichokifahamu, ila umeonyesha ulipofikia kulitafsiri kanisa badala ya kulielewa. Hapo inatosha, nimekuelewa, sinahaja ya kukuuliza zaidi.

Naomba tujadili vielelezo ambavyo Raia mwema anatakiwa atuhakikishie kuhusika kwao badala ya kupoteza muda kwamba wewe walifahamu kanisa au la, hatupo chumba cha mitihani hapa.

Jambo la msingi asiyekuwepo ndani ya uzio huwa na mawazo na fikra nyingi za kufikirika kwa vile hajui mfumo, maisha na sheria zao. Anachoweza kutumia ni nukuru fulani bila kujua mwandishi alimaanisha nini na nini msukumo wa kuandika kitabu au makala gazetini. Huu ni udhaifu wa wengi wetu.

Kama mimi naufahamu Ubudha, ninachojua tu kwamba ni watu wa kutafakari sana na kwa walioendelea katika tafakuri ni kufikia kiwango cha
Nirvana (Nirvana - hatua ya juu anapofanya tafakuri kuhusu suprime being anashtukia ameangama angani), nimesoma na kujifunza hayo katika historia ya dini mbalimbali hata Mtume SAW alipofikia, lakini siwezi kusema najua kwa ufasaha kupita hata mwenye maisha hayo au mwenye kuishi maisha hayo. Hata nilipofundishwa na Maalimu na Shehe tuition ya mambo mbalimbali ya dini yao ingawa naweza hata kukariri baadhi ya miezi kamaRabie awal, Thur Kaadat, Ramadhan, nk nilichoambulia ni kile nilichotaka kukijua nilichohitaji lakini siwezi kujivunia kwamba nayafahamu mambo yao ni kujidanganya, na ndivyo wengi tunavyodanganyika kwa kusoma habari za maandishi ya fulani kwamba tunafahamu kuliko wenyewe wenye maisha yao.

Hao watawa kama picha unayoona hapo juu wakisali vipindi sita kwa siku, mikesha (Matutinum), Misa (Holy Mass), Masifu ya asubuhi (Laudes), sala ya saa tatu (Tersya), sala ya adhuhuri (Noon), sala ya saa tisa, masifu ya jioni (Vesper), na sala ya mwisho kabla ya kulala (Completo). Haya ndiyo majukumu yao ya kila siku, sasa kuwaongezea shutuma za kufanya mikutano ya kupanga mauaji muda wanaposali sala hizo tunahitaji uthibitisho legally si mambo ya kufikirika.

Candid Scope,

Mambo ya kusali sala mara tano au sita kwa siku siyo hoja hapa. Mi pia sidai kujua undani wa Kanisa Katoliki ila kiwango ninachofahamu kinatosha kabisa kunipa picha kwamba hao watawa sio wasafi kama vile unavyotaka kutuaminisha. Mambo ya sala hata mie nimesali sana wakati bado tukiwa seminarini, masifu ya siku nzima (asubuhi, mchana na jioni kwenye "Breviarum Romanum").

Hoja hapa ni uhusika au kutohusika kwa Abasia katika mauaji ya Prof. katika mambo yanayohusiana na biashara ya Abasia (ingawa imefichwa kwa kutumia"trustee share holding"). Najaribu tu kukurejesha katika ile kashfa ya benki ya Vatican (Papal banking scandal 1981-2) mabayo ilihusisha nadhani money laundering kati ya Vatican na Italian Mafia mabpo ilihusishwa na kifo cha Papa John Paul I inayesemekana alitaka kusafisha hali hiyo. Unaweza pia kutazama sinema "The Godfather III" ambamo wamefanya reference ya scandal hiyo katika deal la "Immobiliare".

Kanisa lia watu wachafu na wasafi, ila mambo machafu ya kihalifu yanapofanyika ndani ya Kanisa/Abasia yanapaswa kukemewa na wahusika kuletwa kwenye sheria na sio kutetea kama vile waso ni wasafi 100%. Ukiisoma historia ya kanisa kuanzi kwa huyo Mtume Petro utagundua kuna machafu sana ambayo yamefanywa na Kanisa, uzinzi, uporaji, mauaji, kuhukumu "wazushi", n.k.
 
Banco Ambrosiano was an Italian bank which collapsed in 1982. At the centre of the bank's failure was its chairman,
Candid Scope tazama hii:-

Roberto Calvi
and his membership in the illegal Masonic Lodge Propaganda Due (aka P2). Vatican Bank was Banco Ambrosiano's main shareholder, and the death of Pope John Paul I in 1978 is rumored to be linked to the Ambrosiano scandal, giving one of the subplots of The Godfather Part III. Vatican Bank was also accused of funneling covert United States funds to Solidarity and the Contras through Banco Ambrosiano.

Unaweza kusoma zaidi katika Banco Ambrosiano - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Candid Scope yaelekea una ufahamu mzuri kuhusu kanisa katoliki. Wengine ni wadandiaji.

Binafsi abasia Peramiho naifahamu vizuri. Maelezo ya Fr Fidelis ndio ukweli wenyewe.
 
Candid Scope,

Nimeishi sana nchi ya Kikatoliki na nikuambie tu jambo moja:

Kuna Watawa watu wema sana na Mungu awazidishie kwa wema wao huo. Wamesaidia sana kanisa na watu wengine kwa jumla bila kutaka malipo yoyote kutoka kwao.

Ila katika hao watawa, baadhi ni MBWA MWITU. Nilishawahi kumuona kijana wa Ki-Islaam akiwa kachukizwa na matendo ya Padre fulani ingawa yeye si Mkristo. Na kibaya zaidi ambacho nilikuja kufahamu ni kuwa Padre akifanya kosa au kuwaudhi Wakubwa, basi adhabu yake ni kumpeleka AFRICA, ASIA au Latin America.

Pana wakati niliandika kidogo story za Mapadre ambazo habari zenyewe nilizipata kutoka kwa Watawa wenyewe wakati nikiishi kwa wenzetu. Amini usiamini, jamaa mmoja hapa JF ambaye nampa sana heshima, aliniomba nisiandike habari kama hizo. Nilizifuta na nikaahidi kutoandika tena maana sikutegemea zitamtibua Muumini.

Anyway, endelea kushika sana ulichonacho asije Sikonge, Ibambasi au wengine na wakakunyang'anya. Ni heri uendelee kuamini kuwa dunia ni BLACK or WHITE na siye ngoja tubaki na imani zetu kuwa dunia ni COLOURED.

Mwisho wa siku, ni MANENO yako against MANENO YA GAZETI. Mmoja wenu LAZIMA anadanganya ingawa wajuvi wa mambo wanasema kuwa SIKU ZOTE, UKWELI UPO KATIKATI.
 
Last edited by a moderator:
@Candid Scope,

Sikonge,

Anachoogopa Candid Scope, ambaye naamini ni muumini wa dhati wa ukatoliki, ni kujua ukweli kwamba kuna uhalifu ndani ya Kanisa na vyombo vyalo. Kwa maana nyingine hataki kuukubali ukweli mchungu kwamba hata Kanisa na mashirika ya Kanisa hutenda uhalifu. Ni sawasawa na mtoto ambaye miaka yote amekuwa akifahamu kwamba A ni baba yake, only kuja kufahamu baadaye kuwa baba yake ni B. Ni wazi hatakubali ukweli huo na ataishia katika depression. Hivyo ulichomshauri ni kizuri, aendelee kuamini kuwa Kanisa na mashirika yalo ni masafi, kwa afya ya imani na amani yake ya moyo.
 
Candid Scope,

Mambo ya kusali sala mara tano au sita kwa siku siyo hoja hapa. Mi pia sidai kujua undani wa Kanisa Katoliki ila kiwango ninachofahamu kinatosha kabisa kunipa picha kwamba hao watawa sio wasafi kama vile unavyotaka kutuaminisha. Mambo ya sala hata mie nimesali sana wakati bado tukiwa seminarini, masifu ya siku nzima (asubuhi, mchana na jioni kwenye "Breviarum Romanum").

Hoja hapa ni uhusika au kutohusika kwa Abasia katika mauaji ya Prof. katika mambo yanayohusiana na biashara ya Abasia (ingawa imefichwa kwa kutumia"trustee share holding"). Najaribu tu kukurejesha katika ile kashfa ya benki ya Vatican (Papal banking scandal 1981-2) mabayo ilihusisha nadhani money laundering kati ya Vatican na Italian Mafia mabpo ilihusishwa na kifo cha Papa John Paul I inayesemekana alitaka kusafisha hali hiyo. Unaweza pia kutazama sinema "The Godfather III" ambamo wamefanya reference ya scandal hiyo katika deal la "Immobiliare".

Kanisa lia watu wachafu na wasafi, ila mambo machafu ya kihalifu yanapofanyika ndani ya Kanisa/Abasia yanapaswa kukemewa na wahusika kuletwa kwenye sheria na sio kutetea kama vile waso ni wasafi 100%. Ukiisoma historia ya kanisa kuanzi kwa huyo Mtume Petro utagundua kuna machafu sana ambayo yamefanywa na Kanisa, uzinzi, uporaji, mauaji, kuhukumu "wazushi", n.k.

Mkuu wangu, ukitaka undani wa ile scandal ya mauaji ya Papa tafuta kitabu kinaitwa 'In God's name' by David Yallop
 
Punguza jazba ndugu yangu, andika hoja ndio great thinker tulivyo.
Uchafu wa kanisa hapo ni upi kama mradi huo waliufanya kisheria na kwa taratibu za wanasheria kufuata sheria za nchi? Gazeti limetuhumu Peramiho kupanga ndani ya Abatia mauaji ya Mwaikusa ndio hoja ya tuhuma tunayojadili bado gazeti halijatoa vielelezo na wahusika wameamu kulipeleka Gazeti mahakamani.
 
KAMAJUZI KATUMWAGIA VITU HIVI , WEWE ENDELEA KUTETEA

Ninaona mnajaribu kutuondoa kwenye ukweli na kutuaminisha ya kuwa watu hawa hawawezi kukosea.

kanisani pia kuna mbwa mwitu wamejipenyeza.

jana nimekuwepo Peramiho kupima upepo watawa wengi wamefurahia habari hii kuanikwa ijapokuwa hawapendi kujionyesha maana boss msaidizi wa shirika buluda fr fidelis mligo akijua anakuwajibisha kwa kukutafutia sababu ya kufukuzwa, au anakuhamisha makazi au hata kukumwang..i kwa kumtumia Kamh...a. ndiyo maana katoa mil 5 kwa press club baada tu ya kuua prof na gazeti la raia mwema lilipoandikamajuzi kawapa zingine mil5. watawa wamalalamika hali kiuchumi imekuwa ngumu kisa anahonga hela kuwamaliza wenzie wenye uadilifu.

baadhi ya wenzetu ktk kanisa jirani, kila anapokuja buluda fidelis mulugo kusalisha wanaondoka kurudi makwao kwa kuwa tunaona chui katuingilia asije akameza na wasiohusika. mtu huyu anatisha eti.

Kamtesa buluda mhuwa na watu wa songea hasa peramiho tuna hasila naye. Amemhonga mil 30 hakimu ili atimize, tumekaa kumlilia mungu, si bola angewapa watoto yatima apate thawabu kulikokumwonea mnyonge na mtetezi wa watu. watawa wamenieleza kuwa bado wanamlilia buluda mhuwa maana ndiye aliyekuwa mtetezi wao na alikuwa bosi msaidizi nafasi ambayo inaonekana ndiyo kaifanyia vituko na kwa sasa kaikalia yeye.

tunaomba gazeti hili lije kutuhoji sisi watu majirani zao, tutawambia mengi maana watu hawa wanapotezwa mwelekeo na buluda fidelis mligo. wale mlioko dar na mliopata nakala ya leo tujulisheni kumewekwa nini na raia mwema.

ngoja nipige simu kwa walioko bongo. Buluda fidelis kama utwa umekushinda waachie wenzio kuliko kuleta umafia kanisani, hadi unapokuja kutusalisha tunashindwa kufuatilia ibada, maana chui na kondoo wapi na wapi.

Taratibu, kama ulikuwako Peramiho, nipe majiya ya watawa ulioongea nao ambao walilalamika, mimi nitawasioliana nao na watakuja hapa JF kuhakikisha kauli yako, mimi ni hoja tu si maneno ya kupanga. Niambie majina ya watawa hao kutoka pala St Benedict Abbey.
 
monks.jpg

Mkuu wa Shirika la Peramiho Benedictine Fathers (OSB) Abate Lambert kwenye picha hiyo aliyeko mbele mstari wa nyuma mpenda watu, mleta maendeleo na usitawi wa wananchi wengi ukanda wa Ruvuma na Kusini nyanda za juu kwa wengi wanashangazwa na habari hiyo toka Raia Mwema yenye taswira ya kuchafua badala ya ukweli halisi.

Bahati nzuri siku za nyuma nilipokuwa mwanahabari nilifanikiwa kuwepo kikazi maeneo hayo mwenyeji wangu akiwa Ahmed Jongo. Baadhi ya watajwa nawafahamu si kitu cha kawaida kufanya jambo kama hilo ukitilia maanani ninavyomfahamu Abate Lambert Dor na anavyoheshimika katika Jimbo la Songea na majimbo yandokando na naendeleo kwa wananchi. Hospitali ya St. Joseph Peramiho ndio kimbilio kubwa ukanda huo. Shule ya sekondari Peramiho imetoa wasomi wengi wa kike nchini. Kuna mengi naona wasioijua Peramiho ndio wanaoweza kuzusha mambo yasiyo na kichwa wala miguu, flagment.

Hata Yuda alipomsaliti YESU WATU HAWAKUAMINI KAMA WEWE NA YESU ALIKUFA.
 
Nestory(ex br.Aidan-mfungwa)Mhuwa,Kwirinus Mapunda,Masumbuko(baba yake hajulikani) leteni habari mpya na kwa mbinu mpya. Hiyo ya Mwakusa haijawatoa! Tumeichoka sasa. tumegundua kuwa ninyi ni wahuni na wapuuzi, munaojifisha chini ya uvungu wa gazeti. Kama munayoyasema ni kweli, kwanini munaogopa kupeleka ushahidi huo mzuri polisi?
Mbinu zenu ni duni kama mavi ya kale.
 
kwa nini unatukana na mapovu yanakutoka. Tupe vielelezo vya watu unaowatuhumu badala ya kutoka mapovu. nilikuwa pera leo habari ni kwamba kumbe buluda muhuwa ndiye alikuwa proculator na buluda fides muligo akamfanyia kitu mbaya kwa kumwondoa na akakalia kiti yeye, upande wa mgodi akashika pia, wote waliohoji akahamisha, na ili kufuta nyayo akaanza kuwashugulikia akiua prof na buluda muhuwa akamfunga kwa kuhonga fedha mil 30. anna tofauti gani na yuda aliyemsaliti asiye na hatia? tutajua mengi safari hii, uchamungu wenu, na umafia wenu pia kwa upande mwengine. walio wacha Mungu watajulikana, na wasio watajulikana kwa matendo yao, na siyo kwa maneno yao kuwa mengi.
 
Back
Top Bottom