Who really killed Prof. Mwaikusa?

Candid Scope,

..waliofanya mauaji hayo ni WAHUNI.

..watawa wa ukweli hawawezi kujihusisha na ukatili.
monks.jpg

Mkuu wa Shirika la Peramiho Benedictine Fathers (OSB) Abate Lambert kwenye picha hiyo aliyeko mbele mstari wa nyuma mpenda watu, mleta maendeleo na usitawi wa wananchi wengi ukanda wa Ruvuma na Kusini nyanda za juu kwa wengi wanashangazwa na habari hiyo toka Raia Mwema yenye taswira ya kuchafua badala ya ukweli halisi.

Bahati nzuri siku za nyuma nilipokuwa mwanahabari nilifanikiwa kuwepo kikazi maeneo hayo mwenyeji wangu akiwa Ahmed Jongo. Baadhi ya watajwa nawafahamu si kitu cha kawaida kufanya jambo kama hilo ukitilia maanani ninavyomfahamu Abate Lambert Dor na anavyoheshimika katika Jimbo la Songea na majimbo yandokando na naendeleo kwa wananchi. Hospitali ya St. Joseph Peramiho ndio kimbilio kubwa ukanda huo. Shule ya sekondari Peramiho imetoa wasomi wengi wa kike nchini. Kuna mengi naona wasioijua Peramiho ndio wanaoweza kuzusha mambo yasiyo na kichwa wala miguu, flagment.
 
wala sishangai wafanya maovu wanajifichaga nyuma ya mwamvuli wa dini

Siwezi kuwa kinyume chako kabisa, lakini dhana hii si kuihusisha na shirika wakati labda mmoja binafsi kwa masilahi binafsi amefanya kwa usiri, kinachotakiwa ni mtu huyu mhusika badala ya kulihusisha shirika zima ambalo halijui from A-Z ya kinachoendelea, kwao inaweza kuwa usiku wa kiza kinene tu. Kumbuka hao wazungu unaoona kwenye picha ni raia wa Ujerumani na Uswis wako nchini kwa minajili ya kueneza dini tangu miaka ya 1884, kwa nini hawakujihusisha na mambo hayo miaka hiyo wakati nchi ikiwa chini ya wajerumani na waingereza halafu waanza kuhangaikia hilo leo wakati hata umri wao tu ni vigumu kufikiria hata upandaji wa maua milangoni mwa majengo yao? Picha hiyo ni ya zamani kidogo, hao wazungu ni wazee sana sasa hivi.
 
Mafia hawa ulikuwa hujui? They make money in the name of God. They cheat everybody including themselves.

Afadhali hela zao zinaonekana zinafanya nini. Mashule (Seminary zote za Katoliki ziko juu katika Elimu) Hospital za Katoliki huwezi kulinganisha na za Serikali.
Sitaki kusema haiwezekani kwani hata Papa ni Mwanadamu ila kama ni kweli nadhani issue ni individual na si Shirika
 
Inafahamika kuwa prof Mwaikusa aliuwawa na serikali ya kagame nd hili linahusishwa sana na yeye kujiingiza na siasa za mauaji ya kimbarik nchini Rwanda...Raia mwema chini ya uenyekiti wa Jeneral Ulimwengu wana interest na ukaribu na rwanda na hapa wanajaribu kupotosha
 
Nijuacho ni kuwa prof aliuawa na watu wanaozaniwa ni toka burundi na rwanda nse prof alikuwa anasimamia baadhi ya kesi
Hii ya leo ndo nashangaa ila kama wanahusika hao watawa mbona wangetumia mbinu zingine kutekeleza hayo bse prof aloshindiliwa risasi za kutosha na mpaka leo kimya
 
Nijuacho ni kuwa prof aliuawa na watu wanaozaniwa ni toka burundi na rwanda nse prof alikuwa anasimamia baadhi ya kesi
Hii ya leo ndo nashangaa ila kama wanahusika hao watawa mbona wangetumia mbinu zingine kutekeleza hayo bse prof aloshindiliwa risasi za kutosha na mpaka leo kimya
Na serikali yetu kimya. Alafu Mwema na wenzake wanapeta tu.
 
Mafia hawa ulikuwa hujui? They make money in the name of God. They cheat everybody including themselves.

Inafaa kuwa na jicho la kuona zaidi katika hili badala ya kutoa comment ya jumla jumla. Hatuwezi kusema hata siku moja kwamba serikali ya Tanzania ni ya rushwa, inavuja mali ya umma hilo si kweli. Serikali inabaki kama ilivyo na sheria zake, ila baadhi ya wau walioko ndani ya serikali baadhi wanaweza kuwa na tabia hizo. Hivyo katika hili inawezekana waliotia sahihi katika document za hisa kwenye machimbo ni watu binafsi si shirika.

Upeo wa ufahamu wangu Document zinazohusu shirika mwenye dhamana si Abate Lambert Dor, bali ni mchumi wa Shirika ambaye ni Procurator. Hawa waliotajwa si Procurator wa Abatia, nianyemfahamu nadhani ni mzungu, na baadhi wako Pale Dar Es Salaam Benediction Fathers Kilwa road, Kurasini karibu na Mivinjeni, au bendera tatu ni wale wale.

Shirika hilo ni kubwa sana kama ujuavyo wale wa Ndanda Abbey kule Masasi ni wale wale walijenga Ndanda Hospial, Ndanda Sekondari, Peramiho Hospital, Peramiho sekondari. Ndio walio jenga vyuo vingi vya ualimu nchini ambavyo leo vimekuwa vyuo vikuu kama Kigurunyembe, Matogoro Songera, nk. Pugu pale ndipo yalipokuwa maskani yao ya awali.
 
Hizi taarifa hazina ukweli wowote.

perajubi.jpg


Ukitaka kujua historia ya watu hawa walivyovunja pori la Tanzania na kuleta maendeleo angalia Askofu wa kwanza kama CV yake inavyoonekana hapa chini kenye jedwali.

Bishop Cassian (Franz Anton) Spiß (Spiss), O.S.B. †

Deceased

Vicar Apostolic of Southern Zanguebar {Zanguebar Meridionale}

Titular Bishop of Ostracine


Events

DateAgeEventTitle
12 Jul 1866BornSt. Jakob am Arlberg, Italy
24 Apr 188922.8Ordained PriestPriest
15 Aug 189226.1ProfessedPriest of Order of Saint Benedict
15 Sep 190236.2AppointedPrefect of Southern Zanguebar {Zanguebar Meridionale}, Tanzania
17 Sep 190236.2AppointedVicar Apostolic of Southern Zanguebar {Zanguebar Meridionale}, Tanzania
17 Sep 190236.2AppointedTitular Bishop of Ostracine
16 Nov 190236.3Ordained BishopTitular Bishop of Ostracine
14 Mar 190538.7DiedVicar Apostolic of Southern Zanguebar {Zanguebar Meridionale}, Tanzania
 
Ukimya wa serikali ndo unanifanya niwaze kuwa ilo ni deal la inchi na inchi ingekuwa na kanisa serikali hii ilivyo mbona wangekomaa
 
Leo ndo nimetoka kifungoni, ngoja nikae kimya kidogo

PhD, pesa zilitumiwa kumuuza Yesu...ukweli pekee ndio utatuweka huru na si vinginevyo. Kama kuna ukweli lazima uwekwe vile ulivyo ingawa unaumiza sana roho...tutafanyaje sasa.
 
Ukimya wa serikali ndo unanifanya niwaze kuwa ilo ni deal la inchi na inchi ingekuwa na kanisa serikali hii ilivyo mbona wangekomaa

Ushuhuda wangu ni huu, katika kesi kadhaa ambazo vyombo vya dola vinapofanya uchunguzi, inapotokea kugusa vihiyo katika ngazi za juu serikalini hufanya usanii wa kuyumbisha kutafuta pakujishikiza kama ilivyotokea kwa Mwenyekiti wa Madaktari Tanzania kumsingizia mwenye matatizo ya akili kuwa ndiye aliyempeleka Dr. kule msituni. Wakishaona kuna penye unyonge hujishikiza hapo.
 
Ushuhuda wangu ni huu, katika kesi kadhaa ambazo vyombo vya dola vinapofanya uchunguzi, inapotokea kugusa vihiyo katika ngazi za juu serikalini hufanya usanii wa kuyumbisha kutafuta pakujishikiza kama ilivyotokea kwa Mwenyekiti wa Madaktari Tanzania kumsingizia mwenye matatizo ya akili kuwa ndiye aliyempeleka Dr. kule msituni. Wakishaona kuna penye unyonge hujishikiza hapo.

Ndio maana ukweli lazima utafutwe kwa nguvu zote hata kama unaumiza kiasi gani. Binafsi siamini kama watawa hao wanaweza kufanya hivyo na kama wamefanya hayo hatua za kisheria lazima zichukuliwe juu yao....
 
PICHA kulia ni Kanisa Kuu la Abatia Peramiho
mkuu mbona hiyo picha inaonyesha kama hapo ni TOSAMAGANGA IRINGA? au macho yangu? ama mazingira yanafanana?
 
Ndio maana ukweli lazima utafutwe kwa nguvu zote hata kama unaumiza kiasi gani. Binafsi siamini kama watawa hao wanaweza kufanya hivyo na kama wamefanya hayo hatua za kisheria lazima zichukuliwe juu yao....

Binafsi sipingi kama mtawa binafsi akaweza kufanya kitu kama hicho, inawezakana tu, kwani tumeshuhudia mengi katika kesi kadhaa zinawoweza kufananishwa na hii. Lakini kesi hizo zimekuwa zikimhusu mwanashirika binafsi si shirika. Shirika lina katiba na taratibu katika mikataba, ndio maana utaona miaka yote hii tangu mwaka 1884 hawajaenda kinyume cha sheria za nchi na wako makini sana tu.

Shirika lina mtaalamu wa uchumi na mwenye kubobea mambo ya sheria, na kama hawana hujitahidi kumsomesha mmojawapo afanya kazi kwa umahiri kwa kufuata sheria za nchi. Hivyo katika kesi hii naona mwandishi wa gazeti amerukia kulihusisha shirika badala ya watu binafsi ambao sahihi zao zinaonekana kwenye documents za mikataba ya machimo hayo ya madini.

Shirika la Peramiho halina procurator wawili, ni mmoja tu mwenye dhamana na kutia sahihi mikataba mbalimbali, hapa kuna majina mawili ya Aidan na Edmond na hawajaeleza wana wadhifa gani katika shirila lao. Kwangu wanaonekana tu ni wau wa kawaida wasio na madaraka ya juu katika shirika lao.
 
Back
Top Bottom