Who really killed Prof. Mwaikusa?

Who really killed Prof. Mwaikusa?

Aliyepeleka taarifa hii ya UWONGO NA UZUSHI kwa mhariri mkuu wa Raia Mwema ni NESTORY MHUWA(Ex Br.Aidan Mhuwa). Huyu alikuwa mtawa wa Abasia Peramiho. Amefukuzwa utawa mwaka huu 2012 baada ya kutiwa hatiani na mahakama ya hakimu mkazi Songea january 2012 na kupata adhabu ya kifungo cha mika 3 jela. Kuanzaia mwezi September 2012 ameanza kutumikia kifungo cha nje. Ex mtawa huyo aliiba mamilioni ya fedha ya Abasia Peramiho, ambayo yanafikia zaidi ya Tsh.500,000,000.-(milioni 500). Amezusha uongo huo ili kulipa kisasi kwa sababu yeye bado anaamini alionewa kwakutia hatiani. Pia, aliutegemea sana mgodi huo wa UMICO, asijue kuwa hakuwa na hisa hata mmoja. Kabla ya kutoa habari hii kwenye gazeti husika alijigamba kuwa Abasia imenifukuza utawa na kusababisha kufungwa, hivyo watanikoma. Nitahakikisha nawakomoa. Ni kweli amewakomoa haswa!
Lakini yote ni uongo mtupu na yatapita kama upepo.Yeye aendelee kumtumika shetani!
Ukweli utapatikana mahakamani!
Br. Aidan, ambaye alijaribu kuizunguka Abasia ya Peramiho kwa kuingia ubia na mtu mmoja aishiye Kibaha ili hawa wawili kwa pamoja waumiliki mgodi wa Lukarasi anaitwa Nestory?
Unasema amehukumiwa kifungo na Mahakama ya Hakimi Mkazi Songea?
Kweli, dunia hadaa, ulimwengu shujaa!
 
Hatimaye mmeanza kutajana, mtasema yote. Mara uongo, mara abate, sisi wa kunyumba tunajua kwa ukweli jinsi mtajwa wa hapo juu mlivyomtesa kwa kumfungulia mashtaka ya uongo na kesi ipo mahakama ya rufaa kupinga umafia wako buluda fidelis na abate annastu. wewe buluda unatumia madalaka vibaya, wenzako wazungu wametafuta hela kwa uhalali kwa muda mlefu, wewe unakuja kutapanya kwa kuwafungulia wenzako mambo ya uongo. uongo huwa unafunikwa mala nyingi, lakini infikia maali ukifunika uku, uku unafunuka. aliiba hela ipi, maana naona ktk sakata hili tutasikia mengi, kumbe hata kuwafunga wenzenu mmeshawafunga kwa kitu gani walichowaibia. hukumu ni hapa hapa.
tunawaona wewe buluda hata hapa shilikani unatumia vibaya hela ya shilika kwanza umekuwa unahonga sana, kwani kanisani kuna kuhonga. ma dogo wale wa press club wamekuwa wanaponea kwako, uliwapa mil 5 wakati ule prof alipofariki, lengo lilikuwa nini. zmjuzi tena umetoa mil 5 kuwasaidia hao waandishi. niya yako ni nini kama siyo kukufichia mambo yako. rudi kwenye mada, buluda aidan ulimsingizia na ukahonga sana mahakamani hadi leo hii hatuamini tena abasia. ndiyo maana hata jumuia zetu hatupendi kushiriki na nyie kama zamani.
 
Pia usitutoe kwenye mada, yaani mauaji ya prof, mambo ya huyu mwenzenu mliyeamua kumtesa pasipo sababu na hela yote ya abasia ikaishia mahakamani, mzimu huu ndiyo unawatesa wala siyo kisasi, mnajihisi. na nahisi huyu anayejaribu kuturubuni hapa kama siyo buluda fidelis atakuwa mbia wake jonson nchembe.
 
Aliyepeleka taarifa hii ya UWONGO NA UZUSHI kwa mhariri mkuu wa Raia Mwema ni NESTORY MHUWA(Ex Br.Aidan Mhuwa). Huyu alikuwa mtawa wa Abasia Peramiho. Amefukuzwa utawa mwaka huu 2012 baada ya kutiwa hatiani na mahakama ya hakimu mkazi Songea january 2012 na kupata adhabu ya kifungo cha mika 3 jela. Kuanzaia mwezi September 2012 ameanza kutumikia kifungo cha nje. Ex mtawa huyo aliiba mamilioni ya fedha ya Abasia Peramiho, ambayo yanafikia zaidi ya Tsh.500,000,000.-(milioni 500). Amezusha uongo huo ili kulipa kisasi kwa sababu yeye bado anaamini alionewa kwakutia hatiani. Pia, aliutegemea sana mgodi huo wa UMICO, asijue kuwa hakuwa na hisa hata mmoja. Kabla ya kutoa habari hii kwenye gazeti husika alijigamba kuwa Abasia imenifukuza utawa na kusababisha kufungwa, hivyo watanikoma. Nitahakikisha nawakomoa. Ni kweli amewakomoa haswa!
Lakini yote ni uongo mtupu na yatapita kama upepo.Yeye aendelee kumtumika shetani!
Ukweli utapatikana mahakamani!

Wewe unajua mengi, lakini unaficha mengi. Nashukuru, kwani msomaji yeyote wa taarifa yako atajua kuwa kuna walakini katika safu hiyo ya watawa. Kama wewe unahakikisha kuwa huyo mtawa ameiba mil 500, basi hakuwa peke yake isitoshe umeweka wazi kuwa huyo mtu alikuwa anategemea pesa ya migodi.

By the way, unaandika kuwa alisema watamkoma. Unajua kwanini alisema hivyo? Ni kwa sababu anajua mengi ya siri kuhusu mgodi husika.

Asante kwa kutufafanulia juu ya NESTORY MHUWA(Ex Br.Aidan Mhuwa) , nakusifu maana yeye ndio alikuwa chambo akitumiwa kama jitu lisilokuwa na akili. Mambo yanakuja kidogo kidogo, na ninawaambieni si madogo haya na wala hayataisha leo. Wahusika wote watashughulikiwa, sijui kama CHADEMA ikishinda 2015.
 
Kama ungesoma vizuri maelezo yangu tangu awali ungenielewa kwamba huko mbali sana na mtazamo wangu. Nilieleza wazi kuwa:
Sahihi za watawa hao wawili hazionyeshi majukumu yao katika shirika kwa vile mwenye wajibu wa mikataba ni Procurator wa shirika, hao wawili hakuna hata mmoja ambaye ni procurator wa shirika. Hivyo ingekuwa ni shauri inayowahusu hao waliotia sahihi badala ya kulihusisha shirika.

Mimi ni Mkatoliki najua vema sana taratibu za kanisa na mashirika yake kadiri zilivyoainishwa na katiba za mashirika, Canon Law ya Kanisa Katoliki na taratibu nyingine zinazowahusu.
Shirika la Wamisionari Wabenediktini wa Peramiho kama nilivyoainisha hapo juu ni tawi kutoka Shirika mama la St Ottilien taratibu za shughuli zao lazima

  • Kiroho Mkutano wa shirika uridhie kwa kura za theluthi mbili
  • Kiuchumi Mkutano wa shirika lazima uridhie kura kiwango cha theluthi mbili
  • Mkuu wa shirika arithie maamuzi ya kura za wanashirika kutilia sahihi

Suala linalohusu uchumi hata kiroho kama kuanzisha tawi au nyumba nyingine, kuanzisha mradi mkubwa kama huo wa machimbo ya madini lazima uidhinishwe na mkutano mkuu wa Shirika mama la St. Otilieni pamoja na halmashauri yake inayoundwa na wakubwa kutoka nyumba kadhaa zenye uwakilishi. Mradi kama huo unatakiwa uwe chini ya uangalizi wa procurator mkuu wa shirika. Mfano Procura ya Benedictine Fathers pale Kurasini si ya Peramiho au Ndanda, bali ni ya shirika chini ya usimamizi wa nyumba zilizoka Tanzania.

Kwa hoja hizo maana yake Mkutano Mkuu wa Shirika ulirithia Machimbo ya Madini na hali kadhalika kupanga mauaji ya Mwaikusa kwa theluthi mbili za wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu ya shirika katika ya katiba yao kadiri ya utashi wa gazeti la Raia Mwema? Je, kwa tuhuma hizi ambazo gazeti la Raia Mwema ina maana Abatia ya Peramiho ilifanya mkutano wake wa kikatiba na kupata idhini ya theluthi mbili kupanga mkakati wa kumwua Mwaikusa?

Uzoefu wa watu walio karibu na wamisionari hawa wana kawaida sana ya kuwasaidia watu kwa njia mbalimbali, hivyo yawezekana machimbo hayo ambayo watu walikuwa wanatumia zana duni, waliona kuna umuhimu wa kuwasaidia zana bora. Kwa vile zana hizo ni ghali sishangai kama watumiaji walitakiwa kuzinunua na kama uwezo haukuwaruhusu walihitaji ushauri wa wanasheria namna ya kufanya kama ilivyozoeleka wao kuomba mwanasheria mzalendo kuwasaidia masuala ya kisheria. Kwa vile ni mfumo wa kiuchumi kuna taratibu zake kama kuzitumia kwa mfumo wa ubia kadiri ya maelekezo ya mwanashria wao.

Peramiho licha ya kuwa na wanasheria wao, wana kawaida ya kuajiri mwanasheria mahiri mzalendo ili kuwasaidia kuweka mambo sawa yahusuyo sheria zinazoingiliana na sheria za serikali. Hilo halina shaka, na ndivyo ninavyoelewa walivyomtumia Mwaikusa.

Tatizo wengi wetu tunakuwa na tafsiri potovu kwa kufanya tafsiri tunavyoona sisi bila kufanya utafiti au kuwaulizia wahusika watufafanulie hili ndilo linalotufanya tuonekane tuko watu wenye upeo wa kiwango cha masafa mafupi.

Rais Kikwete miezi michache iliyopita alifungua umeme jimboni Njombe katika Tarafa ya Mawengi umeme ambao umesambazwa vijijini. Mradi huo kwa mtazamo wa wenye upeo wa kiwango cha masafa mafupi watafikiria ni wa kanisa, kumbe ni mpango wa maendeleo wa kanisa kwa wananchi, ni jambo linalohusu wananchi na kwa manufaa ya maendeleo ya wananchi si kanisa lenyewe. Mpango wa Peramiho kuingiza vifaa hivyo huko mimi ningekuwa na mtazamo huo, vinginevyo kuwepo na vielelezo vya wazi vinavyoonyesha umiliki na document za Shirika na Procura kuthibitisha.

Majuzi Speaker makinda amemrudi waziri na wabunge kuibua kashfa za rushwa bila vielelezo vya wazi na bila uthibitisho, hata ikiundwa tume bila uthibitisho nini kitaendelea? Wanamsakama Makinda, lakini ukweli ndio huo kamati haikukuta evidence, sasa itawatia hatiani kwa mambo ya kufirikika? Mwenye evedence apeleke wafungwe, hakuna aliyethubuti ila naneno mengi, kisheria mambo hayaendi hivyo. Ndio haya sasa ya kufikirika hadi kufikia kulituhumu shirika la watawa kuhusika na mauaji bila evidence kama
Lokissa alivyoainisha kwa nukuru ifuatayo:

Kandid Scope, nakusifu kwa kulitetea Shirika kwa nguvu na moyo wote. Maana hata pale penye makosa wewe unalitetea tu. Pole sana.

Unaeleza uzoefu wako juu ya utendaji kazi wa shirika, lakini unachosahau ni kuwa muandishi wa Gazeti kaweka wazi kabisa kuwa shughuli nzima ya umiliki wa mgodi ilikuwa siri au ukipenda ni shughuli ya KIMAFYA. Shughuli kama hizo huwa haziendi katika utaratibu ulioueleza ili kusiwepo nua kuhisiwa kwa jambo lolote lile.

Uchambuzi uliofanyika na Gazeti ni wa kupongezwa, na ulilinga shughuli nzima jinsi ilivyoendeshwa na kuhusika au kuwa na Taarifa kwa wazito wengi wa shirika. Hebu rudia kwa upole nukuuu hapa chini toka gazetini.
"Kwanza napåenda kukutaarifu kuwa shu
Hisa za shirika hilo kwenye ndani ya UMICO hazikuandikwa kwa jina la Peramiho. Hata hivyo, kumbukumbu za kununua hisa zinalifichua shirika hilo pale zinapoonyesha kuwa Peramiho ni mwanahisa ambazo ameaminishwa Johnson Nchimbi, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya UMICO Ltd azishikilie kwa niaba ya shirika."

"Utaratibu uliotumiwa na shirika hilo kumiliki mgodi huo wa dhahabu wa Lukarasi, ndio unaowapa nguvu watawa hao pamoja na washirika wao kuwaelekeza wachunguzi wa kadhia hii kwenda Brela wakifahamu fika kuwa kule shirika halipo, lakini wakati huo huo wakisahau kuwa kuna nyaraka nyingine zinazowahusisha moja kwa moja na umiliki wa mgodi huo"

"Profesa Mwaikusa alikuwa mhimili mkuu wa Kampuni ya UMICO na mmoja wa wawakilishi wa Shirika ndani ya UMICO. Baada ya mauaji yake, wakurugenzi waliobaki nao walijikuta katika wakati mgumu, wakilazimishwa kuachia nafasi zao"

Kwa hiyo maelezo yako ya kisheria ya shirika kama uandikavyo, "kuanzisha mradi mkubwa kama huo wa machimbo ya madini lazima uidhinishwe na mkutano mkuu wa Shirika mama la St. Otilieni pamoja na halmashauri yake inayoundwa na wakubwa kutoka nyumba kadhaa zenye uwakilishi. Mradi kama huo unatakiwa uwe chini ya uangalizi wa procurator mkuu wa shirika." Hapa maelezo kama hayo hayana nafasi kwani shughuli nzima ni ya kimafya. Na kama yasemwayo si ya kweli kwanini wahusika wanashindwa kuzungumza na waandishi wa Gazeti. Hapa ndipo tunapokuwa na wasiwasi.

Hata kama ukidai kuwa Gazeti halijatoa ushahidi wa kuhusika kwao aidha katika mpango wa kumuua Prof au kuhusika shirika katika umiliki wa Mgodi, hata nawe huna ushahidi wa wao kutoshiriki katika tuhuma hizo. Kwanini unasimama kidete na kudai kwa asilimia 100% kuwa hawakuhusika?
 
Zawadi Ngoda
Kwanza ujue mleta mada huwa na msimamo wake na ana haki ya kusimamia mjadala kwa kutetea hoja yake. Mwisho wa mjadala nitatoa hitimisho langu kuhusu majumuisho ya mjadala huu ndivyo watu wenye upeo katika majadiliano tunavyofanya, la sivyo nikiwa mtu ninayeyumba kama bendera inayofuata upepo itaniwia vigumu kusimamia mjadala niliouanzisha. Nifanyavyo ndivyo great thinkers tunavyotakiwa kufanya.

Zawadi Ngoda
jambo la msingi unachanganya mambo uhusika wa shirika na mwanashirika binafsi kujihusisha katika shughuli kama hiyo kwa siri. Hapo ndipo tunaposhindwa kukutana kwa sababu wewe unavyolichukulia jambo hata pale inatokea vielelezo kuonyesha mhusika kajihusisha bila ridhaa au kwa niaba ya shirika ndipo tunapokuja kuelewa tatizo ni la mtu fulani si shirika. Mratibu na mhusika Mkuu wa shirika katika masuala ya uchumi haonekani kwenye document hizo hapo ndipo tunapoamua kung'ang'ania dhana ya umafya ya kufikirika kwa malengo ya kutetea kitu kisichoakisi ukweli. Tunapojadili tusiingize mambo ya kufikirika ambayo hayana uthibitisho wala taratibu walizo nazo katika maisha na shughuli zao za kila siku. Kama mfano niliosema bunge limeaibishwa kwa kutuhumu wabunge kuwa wala rushwa bila evidence na Speaker kuwatolea nje, wengi wataongea kinyume lakini ukweli ndio huo, wengi wetu hapa tupo na mawazo tata ya kufikirika zaidi kuliko ukweli, mfano mzuri katika mada hii watu wanapozusha umafya kitu ambacho hawawezi kuthibisha hata jambo moja ambalo limefanyika kimafya.

Rejeja mabandiko haya mawili hapa chini:
moma2k
Aliyepeleka taarifa hii ya UWONGO NA UZUSHI kwa mhariri mkuu wa Raia Mwema ni NESTORY MHUWA(Ex Br.Aidan Mhuwa). Huyu alikuwa mtawa wa Abasia Peramiho. Amefukuzwa utawa mwaka huu 2012 baada ya kutiwa hatiani na mahakama ya hakimu mkazi Songea january 2012 na kupata adhabu ya kifungo cha mika 3 jela. Kuanzaia mwezi September 2012 ameanza kutumikia kifungo cha nje. Ex mtawa huyo aliiba mamilioni ya fedha ya Abasia Peramiho, ambayo yanafikia zaidi ya Tsh.500,000,000.-(milioni 500). Amezusha uongo huo ili kulipa kisasi kwa sababu yeye bado anaamini alionewa kwakutia hatiani. Pia, aliutegemea sana mgodi huo wa UMICO, asijue kuwa hakuwa na hisa hata mmoja. Kabla ya kutoa habari hii kwenye gazeti husika alijigamba kuwa Abasia imenifukuza utawa na kusababisha kufungwa, hivyo watanikoma. Nitahakikisha nawakomoa. Ni kweli amewakomoa haswa!
Lakini yote ni uongo mtupu na yatapita kama upepo.Yeye aendelee kumtumika shetani!
Ukweli utapatikana mahakamani!

fundimchundo
Br. Aidan, ambaye alijaribu kuizunguka Abasia ya Peramiho kwa kuingia ubia na mtu mmoja aishiye Kibaha ili hawa wawili kwa pamoja waumiliki mgodi wa Lukarasi anaitwa Nestory?
Unasema amehukumiwa kifungo na Mahakama ya Hakimi Mkazi Songea?
Kweli, dunia hadaa, ulimwengu shujaa!

Nilisema toka awali haya mambo hayaendi kwa utaratibu huu tunaoona kwa sababu mfumo wao wa kiutawala na hierarikia ni wa mfumo kama wa serikali, sasa ukweli kwa nukuru hizi unaanza kujitokeza kama nilivyosema ni mtu au watu wawili binafsi ndio waliokuwa wanafanya mambo kwa malengo yao binafsi.
Ushahidi kwamba wamefanya isivyo na wana matatizo mengine ndiyo hilo la mtajwa mmoja wapo katika Gazeti amefukuzwa shirika kwa kufanya mambo kinyume cha utaratibu na sheria na ndiye aliyeamua kulichafua shirila lake kama kulipiza kisasi.

Tuweke jazba kando, tuweke hisia zisizo na uthibitisho eti umafya, unaweza kuthibitisha huo umafya au ni jambo lililopokichwani mwako ambalo ni la kufikirika? Kama una ushahidi wa shirika hilo kufanya umafya tunahitaji evedence si mambo ya kuhisi kwani JF tuko wako wawazi sana, na kile ninachotetema mimi nimeleta mifano na mfumo wa taratibu za uendeshaji shirika na katiba zao zinavyofanya kazi, ukitaka kufanya uhakiki uko huru kuwauliza uone wongo wangu au ukweli wangu, lakini unachokazania umafya tunahitaji uthibitisho hapa, la sivyo utakuwa katika kundi la watu wenye kuleta mabandiko ya mambo ya kufikirika na hivyo kuchafua hali ya hewa.

Kwa taarifa yako shirika la kitawa mtu ukifanya mambo kinyume cha katiba na maadili utakuwa umejihakikishia ticket ya kuwa rejected shirikani na ndicho kilichompata huyo Aidan, mbaya zaidi kushtakiwa mahakamani na hiyo ni revenge kwa shirika lake lililomlea na kumfikisha alivyo anaamua kulichafua ati kwa lkulipiza kisasi cha kufukuzwa.

Maana yake alizoea kufanya mambo yake kwa kivuli cha shirika, na hivyo shirika lilipogundua na kumpa kibano na kupata rejection kwa kumfukuza shirikani anaamua kuchaufa shirika ndivyo hali ilivyo duniani hata vyama vya siasa tumeyashuhudia hayo kwa sana tu.
 
Kwanza nikupe pole kwa kutojadili hoja husika katika mada gazetini ambayo maudhui yake ni mauaji ya Maikusa, kwamba yalipangwa ndani ya Abatia ya Peramiho na kuatibiwa na Abate Lambert Dorr OSB akiwa ndiye kiongozi wa juu pale kama mkuu wa Abatia. Ningekushauri anzisha mada nyingine inayohusu moral itajadilika vizuri. Hapo utatuletea vielelezo na viambatanisho vya kutujuza uhusika wao na mradi huo kama walimiliki au walitumika kama washauri kwa wachimbaji au waliwekeza vifaa vilivyotumika katika mradi huo vikiwa kama ndio sehemu ya hisa. Hilo twalisubiri uanzishe mada linajadilika.

Kwa uelewa wako sahihi za Brother Edmond ambaye kama sijachanganya ni Br Edmond Kimario mtaalamu wa umeme anayeendesha kitengo cha hicho katika abatia hiyo pamoja na mwenzake Brother Aidan vinathibitisha kuhusika katika mauaji au ni kwa vile tu ni watawa kufanya usichotegemea kiuchumi basi ndio wahusika na mauaji?

Tunacho kijadili hapa ni kesi nzito ya mauaji. Suala kama walihujumu uchumi wa madini au maadili yao kidhamiri kadiri ya mwenendo wa maisha yao ni kesi nyingine ijadilike kwa namna ya uhujumu uchumi si mauaji kwani ni vitu viwili tofauti. Cha ajabu unachohangaika kujibu umejichanganya kwamba la mauaji ya Maikusa hulijui, unawezaje kulijadili jambo usilolijua wakati maudhui ya mada ni kuhusu mauaji hayo?

Nakushauri sana anzisha mada nyingine ya kujadili hilo, kwani mimi mleta mada nililenga maudhui ya mauaji yalivyoripotiwa na gazeti. Natumaini umenipata na kunielewa vizuri. Jazba tuweke kando tunapo jadili mada kama hizi, kwani kama unavyosema wawajua hao ni wengi sana hapa wanawajua sana tu kama nilivyokufafanulia hata mmoja ya majina na kazi anayofanya sijui kama unafahamu hata hilo.

Nilishtushwa na hoja zako katika post #57 . Uliandika kama ifuatavyo: " Huo uchafu wa mgodi ni nini ukilinganisha na makubwa yalifanywa miaka nenda rudi kujenga mashule, hospitali, zahanati, vituo vya afya, na mengineyo, ni mgodi gani waliouendesha kupata pesa za kujenga hayo kama si misaada ya waumini na serikali ya Ujerumani na Uswiss kufadhili hayo yote?"

Na hii ndio iliyonishtua jinsi unavyofikiri. Hata hivyo ujumbe umeupata na natarajia utafuta kauliyako hii kabla hatujaendelea kujadili Mauaji ya Prof.

jambo la msingi unachanganya mambo uhusika wa shirika na mwanashirika binafsi kujihusisha katika shughuli kama hiyo kwa siri. Hapo ndipo tunaposhindwa kukutana kwa sababu wewe unavyolichukulia jambo hata pale inatokea vielelezo kuonyesha mhusika hakujihisisha kwa kutumwa au kwa niaba ya shirika ndipo tunapokuja kuelewa tatizo ni la mtu fulani si shirika.

Kama Kikwete kaunda jeshi binafsi na kaenda kuvamia Burundi, hakuna mrundi atayekubali kuwa Tanzania haijaivamia Burundi.

Hatuelewani kwa hilo kwa vile Shirika la Peramiho si la kwanza kutumia ujanja huo. NNaweza kukupa mifano zaidi ya 100.

Kama umeangalia kipindi cha Al jazeera leo juu ya Mashirika yanayofunguliwa nje ya nchi (nje ya Afrika)kwa kutumia majina ya watu wengine ili kukwepa uhusika wao ndio utajua nini mimi ninachokiongelea.

Na katika point hii ndio tunasigana. Utapolielewa hili tunaweza kuendelea na mjadala.
 
Ningekushauri ungeanzisha mada nyingine kuhusu haya ya umafya na yale uliyosema jana kuhusu morals, kwa vile mada hii tunakoenda tunatoka nje kwa vile maudhui ni mauaji ya Mwaikusa ambayo shirika limethumumiwa. Tujaribu kuwa concentrated kwenye main subject la sivyo kuruka huku na kule itaonekana tunacheza mpira uwanjani bila mfumo wa kueleweka na hivyo kutoleta mvuto stahiki.
 
Hii habari itasaidia sana gazeti na Raia Mwema kuuzika. Hivi hili gazeti ndio kipaaza sauti cha Usalama wa Taifa???? Kwani Usalama wa Taifa ndio waliotoa habari hii kwa gazeti hili ili wawape wananchi ukweli wa mwenendo mzima au? Mimi naona kama vile huu ni uzushi tu na kuhisi pengine kuna agenda ya siri ya kulichafua Kanisa Katoliki kwa minajili ya kisiasa na ole wao wahusika.
 
Nakupa tano zawadi Ngoda. Buluda Aidani alifanyika kafara ili kuendelea kuficha umafia wa watu hawa. Imeripotiwa kuwa baada ya kifo cha Prof ndipo na hawa wakawekwa katika msukosuko na mwendeshaji mkuu akiwa buluda fidelis akisaidiwa na watu wake. hela nyingi imepotelea mahakamani na polisi kuhonga mapolisi na hakimu. Jibuni hoja kuwa mmehusishwa na mauaji. Huyu Buluda mliyeamua kumtesa mlivyoweza, mlijua mmemaliza lakini naanza kuona kuwa Mungu kawaumbua. Maana Buluda Fidelis ambaye aliongoza zoezi hili la kumsweka akafie jela, imekuwa tofauti. Mahusiano yetu majirani na Pera yamehalibika siyo kama zamani lakini baada ya wewe Fidelis kushika uongozi umehalibu kila kitu pamoja na mahusiano.

Sisi tunawaangalia tu mwende ki vyenuvyenu na sisi waumini na majilani tumegeukia njia zetu. mabuluda hawana nguvu ya neno la Mungu kama zamani.
waandishi wanalituhumu shilika, na washilika wao yaani jonson nchembe na swahiba wake mkuu shilikani ni buluda fidelis. Ninavyoona, buluda huyu anajua kitu ktk haya, japokuwa ktk simu kwa wandishi alikana kuelewa, ngoja tuvute subira, yatazidi kufumuka tu. Muda huu ngoja niende hukohuko Abasia nikaongee na baadhi ya watawa ili kujua upepo kwa sababu wao wenyewe wamemchoka huyu Buluda wanasema anaendesha Abasia Kimafia.

Naenda.
 
Tunaelezwa kuwa Baraka Mwaikusa, Mtoto mkubwa wa marehemu aliwapeleka chumbani kwa marehemu lakini hawakuchukua chochote, kulikuwa na haja gani ya kuingia chumbani kama lengo lao lilikuwa ni kumuuwa tu Prof? Je hawakuweza kuchukua chochote kwa sababu walizikosa nyaraka hitajiwa? Wauwaji walimweleza Baraka kuwa wasingefikia hatua ya kumuuwa baba yake kama angeacha ukaidi wake, Je, ni ukaidi gani huo? Je Kwanini Prof alikuwa mkaidi hadi kupelekea kifo chake?

Tutafakari!
 
Candid Scope

Kwanza kabisa nikuambie unajua kidogo sana kuhusu Kanisa Katoliki licha ya kuwa wewe ni muumini walo. Pili unachokiongea hapo juu ni "ideal situation" tu, eti mpaka sijui theluthi mbili ikae ndio itoe maamuzi. Hiyo hai-apply pale ambapo kuna uhalifu wa aina yoyote ile unapotendeka. Maamuzi yanakuwa ni angalau kwa mtu mmoja au watu wachache sana "inner circle".

Bado hujasema kwa nini unaamini kwa uhakika kabisa kwamba wao jamaa watawa hawawezi kuhusika na kifo cha Prof. Nimekwambia usome tu hicho kitabu cha David Yallop kuhusu tuhuma za Vatican kuhusika na kifo cha Papa John Paul I ambaye alikuwa amedhamiria kuisafisha Vatican dhidi ya uchafu uliokuwa umekithiri.

Candid Scope, bado unahitaji kulijua na kulifahamu zaidi Kanisa Katoliki, nje ya maswala ya ibada/misa, liturjia na mambo ya sala kanisani.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza kabisa nikuambie unajua kidogo sana kuhusu Kanisa Katoliki licha ya kuwa wewe ni muumini walo. Pili unachokiongea hapo juu ni "ideal situation" tu, eti mpaka sijui theluthi mbili ikae ndio itoe maamuzi. Hiyo hai-apply pale ambapo kuna uhalifu wa aina yoyote ile unapotendeka. Maamuzi yanakuwa ni angalau kwa mtu mmoja au watu wachache sana "inner circle". Bado hujasema kwa nini unaamini kwa uhakika kabisa kwamba wao jamaa watawa hawawezi kuhusika na kifo cha Prof. Nimekwambia usome tu hicho kitabu cha David Yallop kuhusu tuhuma za Vatican kuhusika na kifo cha Papa John Paul I ambaye alikuwa amedhamiria kuisafisha Vatican dhidi ya uchafu uliokuwa umekithiri.

Candid Scope, bado unahitaji kulijua na kulifahamu zaidi Kanisa Katoliki, nje ya maswala ya ibada/misa, liturjia na mambo ya sala kanisani.

Nawe Ibambasi nikupe pole kwani unajadiliana na mtu unayefahamu kwa jina hapa JF bila kumjua upeo wake. Ndio maana hata Zawadi ameongea uwongo kuhusu Dr. Ansgar OSB kumbe mie najua hata wadhifa alio nao na kwamba aliletwa Peramiho na shirika kuzoea mazingira ya nchi za misioni ili napokabidhiwa jukumu zito la management ya uchumi wa shirika katika ulimwengu mzima awe anajua mazingira ya nchi hizo yalivyo.

Labda nikuambie kuchukua nukuru ya kitabu fulani na kuwa kielelezo ni sawa na haya ya Gazeti la Raia mwema lisilofanya utafiti wa kina wala kuwahusisha watu waliowatuhumu ilivyo kawaida ya uhakiki wa wahariri, na katika toleo lao hilo katika habari hii hawakueleza cho chote kuwauliza wahusika ilivyo ada ya uandishi hapo ndipo unapoweza kuona udhaifu unaoukingia kifua katika fani ya habari na uhariri uliotukuka katika kutoa publication zenye kupata heshima stahiki.

Jaribu kusoma historia ya kanisa kuanzia Mtume Petro alipokabidhiwa funguo, jaribu kuelewa teologia, sheria (Canon Law) na kanuni nyingine. Sitaki nikueleze kiwango nichokifahamu, ila umeonyesha ulipofikia kulitafsiri kanisa badala ya kulielewa. Hapo inatosha, nimekuelewa, sinahaja ya kukuuliza zaidi.

Naomba tujadili vielelezo ambavyo Raia mwema anatakiwa atuhakikishie kuhusika kwao badala ya kupoteza muda kwamba wewe walifahamu kanisa au la, hatupo chumba cha mitihani hapa.

Jambo la msingi asiyekuwepo ndani ya uzio huwa na mawazo na fikra nyingi za kufikirika kwa vile hajui mfumo, maisha na sheria zao. Anachoweza kutumia ni nukuru fulani bila kujua mwandishi alimaanisha nini na nini msukumo wa kuandika kitabu au makala gazetini. Huu ni udhaifu wa wengi wetu.

Kama mimi naufahamu Ubudha, ninachojua tu kwamba ni watu wa kutafakari sana na kwa walioendelea katika tafakuri ni kufikia kiwango cha
Nirvana (Nirvana - hatua ya juu anapofanya tafakuri kuhusu suprime being anashtukia ameangama angani), nimesoma na kujifunza hayo katika historia ya dini mbalimbali hata Mtume SAW alipofikia, lakini siwezi kusema najua kwa ufasaha kupita hata mwenye maisha hayo au mwenye kuishi maisha hayo. Hata nilipofundishwa na Maalimu na Shehe tuition ya mambo mbalimbali ya dini yao ingawa naweza hata kukariri baadhi ya miezi kamaRabie awal, Thur Kaadat, Ramadhan, nk nilichoambulia ni kile nilichotaka kukijua nilichohitaji lakini siwezi kujivunia kwamba nayafahamu mambo yao ni kujidanganya, na ndivyo wengi tunavyodanganyika kwa kusoma habari za maandishi ya fulani kwamba tunafahamu kuliko wenyewe wenye maisha yao.

Hao watawa kama picha unayoona hapo juu wakisali vipindi sita kwa siku, mikesha (Matutinum), Misa (Holy Mass), Masifu ya asubuhi (Laudes), sala ya saa tatu (Tersya), sala ya adhuhuri (Noon), sala ya saa tisa, masifu ya jioni (Vesper), na sala ya mwisho kabla ya kulala (Completo). Haya ndiyo majukumu yao ya kila siku, sasa kuwaongezea shutuma za kufanya mikutano ya kupanga mauaji muda wanaposali sala hizo tunahitaji uthibitisho legally si mambo ya kufikirika.
 
Candid Scope

Yawezekana unasoma gazeti tofauti na lile tusomalo wengine, kwani Bruda Fidelis nimemsoma kwenye hiyo article akijibu kimkato kuzuia kuendelea na mahojiano. Pili utetezi wako unasimamia zaidi katika kazi ya utawa kama ni malaika wakati ni binadamu kama wengine.

Lakini nililolifurahia katika mjadala wa hoja hii, ni hatua ya kufunguka kwa baadhi ya siri, kumbe ni kweli kuna mgogoro pale miongoni mwa watawa kuhusu mali za shirika, kwa nini tukuamini wewe kwamba Fr Muhuwa ndiye mkosaji na isiwe Fr Fidelis au wengine hapo shirikani.

Kama ilivyoelezwa kwenye hiyo article, kwamba huo ni mtazamo mpya kuhusu mauaji ya Prof Mwaikusa, lakini hapa unajitahidi kwa nguvu kubwa kutuaminisha kuwa ule mtazamo unaohusisha Burundi ndio sahihi kabisa na sio hao watawa, unathibitishaje, na jee kwa nini pia tusiamini kuwa nanyi ndio wenye kuupotosha umma uangalie mgogoro wa Burundi kwa sababu ilikuwa ushiriki wake kule ulifahamika zaidi na umma!!

Umechokoza ya Br Muhuwa ambaye naye inaonekana anawindwa kuangamizwa, inaonekana huyu ana siri nyingi za hapo, sasa mengi yanafichuliwa, sisi yetu macho na masikio.

Unayazungumziaje madai ya kuhonga katika kuficha ukweli!!!!
 
Last edited by a moderator:
Hawa watawa nao ni MAFIA sana. Mafia wa Italy wamekuwa wakishirikiana na Vatican kwa miaka mingi sana. Wengi wanaamini yule Papa aliyedumu miezi 3 tu, alianza kuwakalia kooni Mafia na wakaamua kumfunga mdomo.

Kutoka hapo, Papa amebaki kushughulikia mambo ya Kidini na mambo ya Serikali ya Vatican, kawapisha Watoto wa Mujini.

200px-Hitlerspope.jpg
hitler-pope-pius.jpg

bishops_salute_hitler.jpg
 
Candiki,

Yawezekana unasoma gazeti tofautina lile tusomalo wengine, kwani Bruda Fidelis nimemsomakwenye hiyo article akijibu kimkato kuzuia kuendelea na ahojiano. Pili utetezi wako unasimamia zaidi katika kazi ya utawa kamani malaika wakati ni binadamu kama wengie.

Lakininililolifurahia katikamjadala wa hoja hii, ni hatua ya kufunguka kwa baadhi ya siri, kumbe ni kweli kuna mgogoro pale miongoni mwa watawa kuhusu mali za shirika, kwa nini tukuamini wewe kwamba Fr Muhuwa ndiye mkosaji na isiwe Fr Fidelis au wengine hapo shirikani.

Kama ilivyoelezwa kwenye hiyo artcile, kwamba huo ni mtazamo mpya kuhusu mauaji ya Prof Mwaikusa, lakini hapa unajitahidi kwa nguvu kubwa kutuaminisha kuwa ule mtazamo unaohusisha Burundi ndio sahihi kabisa na sio hao watawa, unathibitishaje, na jee kwa nini pia tusiamini kuwa nanyi ndio wenye kuupotosha umma uangalie mgogoro wa Burundi kwa sababu ilikuwa ushiriki wake kule ulifahamika zaidi na umma!!

Umechokoza ya Br Muhuwa ambaye naye inaonekana anawindwa kuangamizwa, inaonekana huyu ana siri nyingi za hapo, sasa mengi yanafichuliwa, sisi yetu macho na masikio.

Unayazungumziaje madai ya kuhonga katika kuficha ukweli!!!!

Siri ya umiliki wa mgodi ni kwamba kuna sahihi za watu wawili ambao inasemwa ni watawa, lakini hawa wawili si viongozi wa Abatia Peramiho wenye majukumu ya kufanya mikataba kisheria kama alivyo procurator, ni sawa na kusema wajanja wameiba pesa serikarini na kuzificha nje au mipango ile ya account za nje zilizowaingiza wajanja serikalini katika awamu hii. Tuhuma kama hizo huwezi kuzihusisha moja kwa moja na uongozi wa vyombo vya bank au serikali kwa vile pesa hizo hazikuchotwa kwa utaratibu wa kimfumo na wala serikali haikuhusika kwa vile ni kinyume cha sheria na utaratibu, ila wajanja wachache ndani ya serikali kwa jeuri yao walifanikisha mpango huo wakati wengi ndani ya mfumo mzima wa serikali wasijue. Hayo ndiyo yaliyomfikisha mhusika katika jeuri hiyo kunasa kwenye mtego na kuwa rejected na shirika lake, na yalipomkuta hayo na kuona aliyokuwa anayafanya kwa mgongo wa shirika hawezi tena hapo ndipo anapoumia na kuamua kulichafua shirika lake.

Shirika lake limefanya jambo muhimu so far kwa kumtoa shirikani na kumstaki kwa vile amekuwa akifanya mambo yaliyo kinyume cha katiba, maadili na taratibu ya wito wake wa kitawa na hivyo wasingefanya hayo leo hii kusingekuwa na haya tunayojadili. Hizi ni dalili wazi za jeuri aliyokuwa anafanya shirikani kumtokea puani na sasa kachanganyikiwa na kufikia hatua ya kushika shoka kukata tawi alilolikalia.

Kama shirika lingekuwa linahusika na mradi huo kwa vyo vyote lisingeweza kumlipua huyo mhusika kwani kwa kufanya hivyo ni kujikoroga, hata haiingii akilini hilo kufanyika. Hali kadhalika kuhusika kwa shirika hilo procurator angehusika katika kutia sahihi kwenye documents.

Raia mwema haijaambatanisha katika makala yake kielelezo cha document kinachochukuliwa kama uthibitisho wa uhusika wa shirika hilo katika tuhuma za mauaji hayo, la sivyo article yenyewe inaonekana kuwa fragment. Hapo ndio unapoona mhariri mkuu kupwaya kwa kiwango kikubwa katika jukumu lake la kuhakikisha habari kama hizi zinakuwa na uchunguzi wa kina wenye kutoleta mashaka wala udhaifu katika mada ileyowekwa gazetini mwake ukitilia maanani ni tuhuma nzito kuhusu mauaji.

Udhaifu mkubwa kwenye article hiyo ni:
  • kutoonyesha jitihada zo zote kuongea na upande wa watuhumiwa ilivyo kawaida, jambo ambalo wachangiaji wengi ukiwa wewe mmoja wapo mnakwepa kujibu. Magazeti mara zote yanandika mada kama hizi kwa hufanya kila liwezekanalo kupata kauli pande zote, utakuta tumemtafuta kwa simu mhusika kasema hiki, au jitihada zetu ziligonga mwamba katika kumpata fulani, kwanini katika hili hatusikii tijihada za gazeti hili kuwasiliana na upande husika na hata kumtuma mwandishi kwenda kukutana nao ili kupata habari yenye kuakisi ukweli kamili?
  • Kutoweka kiambatanisho cha kivuli cha document ambayo mada imeegemea kulituhumu shirika kuhusika na mauaji, kwani katika kesi nzito kama hii huwezi kujenga utetezi hewa usiokuwa na vielelezo vyenye kusaidia vyombo vya dola kuchukua hatua.
  • Kama tuhuma hizo zingekuwa na uthibitisho wa uzito stahiki sina shaka vyombo vya dola vingeshachukua hatua mapema kwani tuhuma za mauaji si kitu lele mama.

Tatizo linepowashinda kupata ukweli, sasa ndipo unapozuka usanii wa kuchepusha ukweli kwa kusingizia oh ni umafya, huu ndio uswahili wetu badala ya kutafuta ukweli kwa utafiti unaotakiwa na haya magazeti yetu na sisi tunaingia kichwa kichwa tu.

Tunachohitaji Gazeti hili lifanya mahojiano na wahusika na kupata ukweli ili washikwe na kushitakiwa katika sakata la Kupanga na Kumwua Mwaikusa, si oh umafya hiyo haitatusaidia katika ukweli wa mauaji bali ni uswahili wa watu wasio great thinker. Kama umafya tunacho chombo cha kiserikali cha kimafya usalama wa taifa wanaoweza kufanya utafiti kama uhalifu umefanyika kimafya.

Sipendi hoja za kufikirika hata siku moja,
Ukweli huwa katika uchambuzi na uchunguzi wa kina.
Ukweli utatuweka huru.

Hawa watawa nao ni MAFIA sana. Mafia wa Italy wamekuwa wakishirikiana na Vatican kwa miaka mingi sana. Wengi wanaamini yule Papa aliyedumu miezi 3 tu, alianza kuwakalia kooni Mafia na wakaamua kumfunga mdomo.

Kutoka hapo, Papa amebaki kushughulikia mambo ya Kidini na mambo ya Serikali ya Vatican, kawapisha Watoto wa Mujini.

200px-Hitlerspope.jpg
hitler-pope-pius.jpg

bishops_salute_hitler.jpg

Ukweli hujitenga na wongo. Tunacho chombo cha kiserikali ambacho ni Usalama wa Taifa ambao ndio wenye kuchukua jukumu la kuchunguza mambo ya kimafya, je, wamewatuhumu hawa kuwa ni mafya? Usalama wa Taifa wametawanyika kila kona ya nchi, hili la umafya lingefanyika kwa njia ipi wakati hao ni wengi wao ni raia wa nje ambao jicho la serikali kupitia usalama wa taifa wako muda wote kuwaangalia mienendo yao?

Tunahitaji kujadili kama great thinker, na naweza kusema sifikirii greater thinker kama
Sikonge anaweza kuchuku hoja laini ya kufikirika kirahisi hivi bila uthibitisho, uchunguzi wa kina.

Lets be fair.
 
Mkuu,

Mie siwahukumu hao jamaa na wala sijasoma makala nzima maana naona Kidhungudhungu leo.

Point yangu ilikuwa ni kwamba, Wakatoliki ni kama watu wengine. Kwenye kundi la Kondoo, na Chui wamo. Na kwenye kundi la Chui, na Kondoo pia wamo. Wewe maelezo yako yanawapa hawa jamaa 100% kuwa ni watakatifu na unaweka sheria na mistari kibao kuwa HAWAWEZI.

Narudia tena, mie siwahukumu na hakuna sehemu nimesema kuwa JAMAA WANA MAKOSA. Ila kama Papa mwenyewe alikuwa akishirikiana na Hitler, itakuwa hao wengine? Point yangu ni moja, LOLOTE LILIWEZA KUTOKEA. Wanaweza kuwa ni MAFIA kweli au WAMESINGIZIWA.

Usalama wa Taifa upi unaoongelea? Na mwanasheria mwenyewe ndiyo huyo WEREMA kila siku anapewa shule na Tundu Lissu. Vyombo vyote vya usalama wa Taifa, maboss wake wameteuliwa na yule mwenye jina gani sijui? Ngoja nimuulize John Mnyika........

Back
Top Bottom