Who really killed Prof. Mwaikusa?

Kusema ukweli, this issue inaniuma sana kwasababu mwaikusa alinifundisha administrative law pale UDSM, ni mtu ambaye alikuwa fit sana. Lakini cha ajabu, siamini kama kweli kesi yake ya ugombea binafsi ndo itakuwa imemuua, kwa sababu kama issue ndo ingekuwa hiyo, Mch. Mtikila tungeshampoteza muda mwingi sana. Zaidi ya yote, Tanzania hatuna historia ya kuua watu hivyo kama anavyofanya Kagame....

Hapo ndo napenda Tz ihakikishe inafanya investigation na kama Rwanda watakuwa wamehusika, kwa kweli hatua nzito za kidiplomasia zinatakiwa kuchukuliwa.
 
It still does not fit the puzzle. What did the killers have to gain if the real reason behind his killing was that he had defended genocide suspects?
What threat did he pose, if Rwanda was behind it, to the Rwandan government? Let us hope those arrrested for his murder will talk.
 
ha hha ahaha chunguza kwanza hiyo San francisco bay view ndio utaelewa unachoongea.
 
Damu nzito kuliko maji. Hivi nyinyi mlitegemea Banyamulenge Salva aache kutoa siri kwa Kagame ili iwe nini? Subirini akina Koba waje kutetea ndugu zao hapa.
 
It still does not fit the puzzle. What did the killers have to gain if the real reason behind his killing was that he had defended genocide suspects?
What threat did he pose, if Rwanda was behind it, to the Rwandan government? Let us hope those arrrested for his murder will talk.

Mkuu Jasusi, kuna tetesi kuwa kuna faili wauaji walikuwa wakilitafuta na alikuwa na mazoea ya kwenda nalo nyumbani kulifanyia kazi. Faili lenyewe lilikuwa na bomu lililowahusu wazito wa Tz - hiyo theory ya defence of genocide suspects ni kile kilichopangwa kitumike kama red herring kufunika wingu zito linalofunika hicho kifo. Kama nilivyosema mwanzo ingawa mpaka sasa ni tetesi lakini ni dalili ya mambo ambayo tutegemee kuyashuhudia tunavyokaribia uchaguzi wa mwaka huu.
 
kwakweli kama hawa wauaji watakuwa ni wauaji toka Rwanda, Selikali inatakiwa kuchukua uamzi wa kueleweka kabisa, na ikiwezekana, watupiliwe mbali kabisa hata kwenye east africa community, fukuza kabisa hata balozi wao...kwasababu kama mauaji yatakuwa ndo ya aina hiyo ya ICTR tribunal issue, basi selikali ya kagame lazima itakuwa inahusika....kwa visirani vyao na wahutu.

....nasikia hata yale mabomu ya Temeke kuna mkono wa Kagame pale,kweli huyu inabidi tumkomeshe la sivyo atatuchafulia amani yetu
 
Boy I tell you, conspiracy theorists are hard at it (at work, that is)

With due respect, inaelekea hii cospiracy is alive. Kila ambaye kwa namna yoyote hakubaliani na msimamo wa serikari ya Rwanda anauawa. Inatakiwa wafe wangapi ndipo isiwe conspiracy?
 
Damu nzito kuliko maji. Hivi nyinyi mlitegemea Banyamulenge Salva aache kutoa siri kwa Kagame ili iwe nini? Subirini akina Koba waje kutetea ndugu zao hapa.

Kitu cha kwanza unachotakiwa kuelewa ni kwamba, BANYAMULENGE ni watusi wanaoishi Congo. Hili ni kabila la watusi waishio nchini Congo ambao Kagame amekuwa akiwasapoti kupitia Laora Nkunda aliyekimbilia uhamishoni Rwanda kwa sasa hivi. hivyo unapoongelea RPF chama cha kagame kilichotoka msituni hadi kusababisha mlipuko wa genocide uanze, usichanganye na Banyamulenge..

Banyamulenge ni watu wanaoongea kitusi na ni watusi wa kikongo si wa Rwanda OK. Hebu tuongeage kisomi sometimes....watu wengi wanatusome watz humu na wanaweza kuona kama sio watafiti na wasomaji wa habari.

Pili , Hivi Salva ni Mtusi? Hadi unamwita Banyamulenge? Najua Salva yuko Ikulu, lakini nilikuwa sijui kama ni Mtusi. Yeye hajatoka Bukoba kweli yule? Kama ni Mtusi wekeni wazi na mtusi mwenyewe asiwe mtusi wa Kitanzania...Kama ni mtusi raia halali wa Tanzania, hatutakiwi kumbagua...

Kwa sababu hata makabila mengine, kuna wanyasa wanaoshare nchi mbili Tanzania na Malawi, Kigoma kule unashare watu wengi tu, na Burundi na Rwanda, Bukoba nako unashare na Waganda etc.. Msumbuji unashare na makabila ya kina mkapa na huwezi kuwaita hao ni alien.. inauma sana kubaguliwa...racism is poisonous unajua...
 
Nadhani wanadamu ( i mean any citizen of the world) wanapaswa kujua kuwa mtusi ni mtusi tu, awe wa Kongo(banyamulenge) wa unganda(mnyankole), wa Tz au hata wa Ulaya. Juhudi za Prof Mwaikusa zilikuwa zinalenga kuanika ukweli juu ya uongo wa kuwa Rwanda kulikuwa na mauaji ya kibali wakati hayakuwepo.

1. Alitetea kuwe na uwezo wa ICTR kujiridhisha kwa kutemebelea eneo la tukio ili kujionea ukweli. hii ingeepusha ushahidi wa kufundishwa unaotolewa mahakamani na mashahidi wengi.

2. Alitetea wafungwa wa ICTR watumikie adhabu zao mahali pengine na siyo Rwanda kwani wakienda Rwanda ni Kifo. Kwa watutsi ilikuwa lazima wahakikishe wamemuondoa.
 
kwakweli kama hawa wauaji watakuwa ni wauaji toka Rwanda, Selikali inatakiwa kuchukua uamzi wa kueleweka kabisa, na ikiwezekana, watupiliwe mbali kabisa hata kwenye east africa community, fukuza kabisa hata balozi wao...kwasababu kama mauaji yatakuwa ndo ya aina hiyo ya ICTR tribunal issue, basi selikali ya kagame lazima itakuwa inahusika....kwa visirani vyao na wahutu.

mh!
 
Shirika la Wabenedition Tanzania ambalo ni tawi toka shirika la Mt. Otilia kutoka Ujerumani kuingizwa kwenye tetesi ya kashfa ya mauaji ya Mwanasheria Mwaikusa, ni jambo la kushtua na si la kawaida, pengine ni mbinu ya kuyumbisha ukweli wa kilichojilia, huku wakihusishwa Br. Aidan OSB na Br. Edmond OSB kwa kile kinachoelezwa sahihi za hao wanashirika la Benediction Fathers Peramiho kukutwa kwenye document ya Mwaka 2003 inayoonyesha wanahisa katika machimbo yamgodi wa Lukarasi.

Jambo linalonishangaza ni kuhusushwa Abate Lambert Dor OSB ambaye ni mkuu wa shirika hilo huko Peramiho, wakati wahusika ni hawa wawili pengine walifanya mikataba binafsi na si shirika.

Ninavyoelewa kuna upungufu mkubwa kuhusu habari hiyo kwa maana kwamba wenye mamlaka katika shirika lao kufanya mikataba si kila mwanashirika, ila ni Procurator wa shirika mwenye dhamana na mambo ya uchumi wa shirika, na udadisi wangu bado sina hakika kama hawa ni wako katika kitengo cha procurator ya Peramiho Abbey, huenda ni miradi binafsi inayofanywa na hao mabradha wawili na hivyo kulitia aibu na miskusuko shirika. Pengine uchunguzi ufanyike kwa kiwango cha kisheria, maana kama habari ilivyoletwa inatoa mswali ambayo kuna upungufu mkubwa wa kulihusisha shirika hilo ambalo makazi yake yako St. Otillien, nchini Ujerumani.

Habari hiyo ni kama ifuatavyo hapo chini nukuru kutoka gazeti la Raia Mwema.

Profesa Mwaikusa alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sheria. Aliuawa na watu wasiojulikana usiku wa Julai 13, mwaka 2010 wakati akirejea nyumbani.

Mengi yamezungumzwa kuhusu mauaji ya gwiji huyo wa sheria nchini, kila kundi likiibuka na nadharia yake kuhusu wahusika wa mauaji hayo, baadhi wakiyahusisha na kesi za watuhumiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda aliokuwa akiwatetea katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda Jijini Arusha.

Wapo pia waliohusisha mauaji hayo na kifo cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Daudi Balali, hao ni walioamini kuwa Gavana huyo alipata kukutana na Profesa Mwaikusa na inawezekana kuwa walizungumza kuhusu kashfa za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).


Hayo yakiendelea, sasa taarifa za kichunguzi ambazo Raia Mwema imefanikiwa kuzipata, zimeongeza utata zaidi katika sababu za mauaji hayo, zikieleza kwamba mauaji ya Profesa Mwaikusa yanaweza kuwa yalifanywa kwa maelekezo ya baadhi ya watawa wa Shirika la Wabenedikti wa Peramiho, wafanyabiashara, wahalifu na viongozi ndani ya Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma.

Habari zaidi zinasema wahusika kwa mujibu wa taarifa hizo mpya, wamekuwa wakijichimbia Peramiho, Songea, mkoani Ruvuma na Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mauaji ya Profesa Mwaikusa yalipangwa na kuratibiwa ndani ya Shirika la Watawa la Peramiho mkoani Ruvuma ambako inaelezwa ndimo walimo wahusika wakuu wa mauaji hayo kutokana na ugomvi wa umiliki wa mgodi wa dhahabu wa Lukarasi ulioko wilayani Mbinga, uliokuwa unamilikiwa na Shirika la Benedikti la Peramiho.

Taarifa zinasema kwamba Profesa Mwaikusa alikuwa akihifadhi nyaraka za umiliki wa mgodi huo na yalikuwapo maagizo kutoka kwa mkubwa wa Shirika, anayetajwa kwa jina la Fr. Lambert, akiwaagiza wakurugenzi walioteuliwa kusimamia hisa za shirika hilo kwenye mgodi huo kutofanya jambo lolote pasipo kumshirikisha Profesa Mwaikusa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Profesa Mwaikusa naye alikuwa ameteuliwa kuwa mmoja wa wawakilishi wa shirika hilo kwenye mgodi huo wa dhahabu, kwa barua ya Agosti 12, 2003 iliyowekwa sahihi na Buruda Aidan na Buruda Edmund wote wakionyeshwa kuwa na hisa 2000.

Wawakilishi hao wawili waliteuliwa na Mkubwa wa Jumuiya hiyo ya watawa wa Peramiho wakiwa watawa na kuongezewa mtu mwingine, mkazi mmoja wa Songea Mjini anayetajwa kwa jina la Steven Haule ambaye hakuwa mtawa.

Uteuzi wa wawakilishi hao uliibua uhasama mkubwa miongoni mwa watawa wenzao likiibuka kundi la watawa waliotaka wakabidhiwe jukumu la kuwakilisha shirika hilo huko mgodini. Inaelezwa kuwa ni kundi hili lililopanga njama za kupora nyaraka hizo kwa gharama yoyote hata ikiwa ni kutoa uhai wa wawakilishi halali wa shirika hilo.

Taarifa zinasema akiwa mwakilishi wa Shirika la watawa hao, Profesa Mwaikusa alisimamia sheria akiwataka watawa hao kufuata sheria katika kuuchukua mgodi huo wa Lukarasi, msimamo ambao hawakukubaliana nao kutokana na mazingira ya usiri katika umiliki wa mgodi wenyewe, usiri uliowanufaisha zaidi watawa hao.

Vielelezo mbalimbali, ambavyo Raia Mwema imefanikiwa kuvipata, vinawaonyesha baadhi ya viongozi wa zamani wa shirika hilo kuwa nyuma ya kundi hilo la watawa na washirika wao waliopanga mipango ya kupora nyaraka hizo za siri kutoka kwa Profesa Mwaikusa, na wanatajwa kuanzisha uhasama mkubwa na viongozi wapya walioteuliwa na aliyekuwa Mkubwa wa Shirika hilo la Peramiho, Fr. Lambert.

Siri katika umiliki wa Mgodi wa Lukarasi

Nyaraka zinaonyesha kuwa shirika hilo linamiliki mali mbalimbali zikiwamo nyumba, magari, bunduki, viwanja na mgodi wa dhahabu wa Lukarasi huko Mbinga mkoani Ruvuma.

Hata hivyo, nyaraka hizo zinaonyesha kuwa shirika hilo limekuwa likimiliki mgodi huo kwa siri ambapo hutumia wawakilishi wanaojitokeza kwenye nyaraka za shirika hilo.

Shirika hilo la watawa wa Peramiho, lilinunua hisa kwenye Kampuni ya UMICO, inayomiliki mgodi huo wa dhahabu wa Lukarasi, kwa dola zinazoelezwa kuwa zaidi ya laki tatu, na vyanzo ndani ya Shirika hilo la "Roman Catholic Benedict's Abbey of Peramiho" vinabaisha kuwa lilitoa shilingi bilioni mbili na kusimamia uendeshaji wa mgodi huo kwa siri.

Kwa mujibu wa nyaraka za kampuni hiyo kwa mwaka 1997, wanahisa wa Kampuni ya UMICO, wanaonyeshwa kuwa ni Barnabas Mathew, Dismas Ndunguru, Johnson Nchimbi, Francis Kayombo, Kenneth Nchimbi na Karim Hassanali Teja Kanji.

Hisa za shirika hilo kwenye ndani ya UMICO hazikuandikwa kwa jina la Peramiho. Hata hivyo, kumbukumbu za kununua hisa zinalifichua shirika hilo pale zinapoonyesha kuwa Peramiho ni mwanahisa ambazo ameaminishwa Johnson Nchimbi, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya UMICO Ltd azishikilie kwa niaba ya shirika.

Miongoni mwa nyaraka hizo, ni zile za ununuzi wa hisa kutoka kwa mwanahisa Karim Kanji, mawasiliano ya shirika na Kanji kuhusu malipo ya hisa hizo na nyaraka za kisheria kuhusu uteuzi wa wawakilishi wa shirika hilo katika Kampuni ya UMICO, na kila mmoja alisaini nyaraka zake pamoja na mwanasheria wao, Profesa Mwaikusa, Juni 17, 2003.

Nyaraka hizo za uteuzi zilikuwa ni za pamoja na Buruda Mhuwa, Buruda Kimario na Haule, ambapo ni katika nyaraka hizo pia zinatajwa hisa 4,250 za shirika hilo kwenye mgodi wa Lukarasi, mgawanyo ukiwa wawakilishi watawa wawili hisa 2000 kila mmoja na Haule hisa 250.

Katika nyaraka hizo pia ndimo inamobainishwa ushiriki wa Nchimbi katika kulifichia siri shirika hilo hizo hisa 4250.

Utaratibu uliotumiwa na shirika hilo kumiliki mgodi huo wa dhahabu wa Lukarasi, ndio unaowapa nguvu watawa hao pamoja na washirika wao kuwaelekeza wachunguzi wa kadhia hii kwenda Brela wakifahamu fika kuwa kule shirika halipo, lakini wakati huo huo wakisahau kuwa kuna nyaraka nyingine zinazowahusisha moja kwa moja na umiliki wa mgodi huo.

"Sifahamu chochote, hatuhusiki na mgodi wa Lukarasi, I know nothing about it, nenda Brela upate members wa mgodi, sawa? bye," alijibu Buruda Fidelis Mligo alipotakiwa kuelezea anachofahamu kuhusu mgodi huo.

Jibu la aina hiyo hiyo lilitolewa na Johnson Nchimbi katika mahojiano yake na Raia Mwema kwa simu akisema: "Mimi siko authorized (siruhusiwi) kutoa taarifa za kampuni. Ni vema ukaenda Brela." Hata hivyo, baadaye alizungumza kuonyesha yamekuwepo mawasiliano na Buruda Mligo akisema: " Jana Br (Buruda) Fidelis alipigiwa simu kutoka Raia Mwema, hakufurahishwa na maswali, nikamwambia wakikupigia tena waambie waende Brela."

Nchimbi alisema tena baaaye: "Si vema mtu kukupa taarifa, mimi si msemaji wa kampuni, ukitaka taarifa zaidi tuwasiliane."Vyanzo vya ndani ya shirika hilo vinaashiria kwamba mauaji ya Profesa Mwaikusa yana mkono wa baadhi ya watawa ndan i ya shirika hilo.

Aidha, taarifa nyingine zinamtaja mtu ambaye alikuwa karibu kabisa na Profesa Mwaikusa kusaidia kufanikisha mpango huo kama Profesa Mwaikusa asingekubali kutoa nyaraka za shirika.

Vyanzo ndani ya familia ya marehemu pamoja na taarifa za maandishi zinaibua mazingira ya mashaka kuhusu mahusiano ya mtu huyo na marehemu, siku chache kuelekea mauaji hayo. Familia ya marehemu Mwaikusa inathibitisha kupotea kwa mtu huyo tangu ilipohamia Salasala kutoka Kunduchi jambo lililowashangaza kwani haikuwa kawaida yake.

Maelezo hayo yanaoana na ya vyanzo ndani ya shirika hilo vinavyoeleza kuwa marehemu akiwa na mkurugenzi mmoja wa watawa waliokuwa wakisimamia mgodi huo, walikubaliana na mtu huyo wakutane nyumbani kuzungumzia ujumbe uliokuwapo kuhusu kundi la watawa waliotaka kuchukua mgodi kwa nguvu, lakini katika hali iliyowashangaza, rafiki huyo wa marehemu hakufika na hawakuonana naye tena hadi Profesa Mwaikusa anauawa.

Taarifa zinasema wakati wa msiba mtu huyo alifika nyumbani kwa marehemu eneo la Salasala, ikiwa ndiyo mara yake ya kwanza tangu familia hiyo ihamie huko.Mawasiliano ya watawa hao na Profesa Mwaikusa kabla ya mauaji yake, vinaonyesha kuwa mbali ya yeye, kulikuwa na watu wengine watatu zaidi waliokuwa kwenye orodha ya kuuawa, na kwamba tayari walishahisi kuwapo kwa njama hizo.

Profesa Mwaikusa alikuwa mhimili mkuu wa Kampuni ya UMICO na mmoja wa wawakilishi wa Shirika ndani ya UMICO. Baada ya mauaji yake, wakurugenzi waliobaki nao walijikuta katika wakati mgumu, wakilazimishwa kuachia nafasi zao.

Source: Raia Mwema
 
Jwani Mwaikusa...........Kenneth Nchimbi.........Johnson Nchimbi.....Any relation to Emmanuel Nchimbi???
 
Candid Scope,

..waliofanya mauaji hayo ni WAHUNI.

..watawa wa ukweli hawawezi kujihusisha na ukatili.
 
Last edited by a moderator:
bado nina majonzi ya msiba wa baba askofu Aloysius balina, sitachangia uzi huu leo.

Msiba huo wa Askofu Aloysius Balina umenigusa sana, namkumbuka alivyokuwa so social kwa kila mtu, hakuwa na makuu, mpenda watu. Unajisikia huru kabisa kuongea naye kama mwenzako. Namkumbuka nimekutana naye mara kadhaa wakati angali askofu wa Jimbo la Geita na hata kabla hajawa askofu alipokuwa anafanya kazi TEC. Askofu ambaye unaweza kumwalika kifamilia kaja kushiriki, si jambo la kawaida kwa maaskofu walio wengi. Basi kazi ya Mungu haina makosa, ndio ukamilifu.
 
Back
Top Bottom