jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Tarehe 27/4/2001, Raisi Benjamin William Mkapa alimteua Bwana John Tendwa kuwa Msajili mpya wa Vyama vya Siasa akichukua nafasi ya George Christopher Liundi ambaye muda wake ulimalizika.
Kabla ya hapo John Tendwa alikuwa wapi na alikuwa anafanya nini - wana JF mpo? - msaada unatakiwa kwani giza lililotanda kuhusu historia yake linaleta wasi wasi.
Je ni Mtanzania? Alizaliwa wapi? Alisomea wapi?
Good question, i mean thread imechelewa lakini si sana,kama tungefanya hivyo kwa Balali ambaye alikuwa maybe raia wa marekani, maybe tungesave ufisadi mwingi sana...
Hatuna utaratibu wa vetting kwenye nafasi muhimu zinazohusisha demokrasia ya kweli, zenye kuhusisha kuwatumikia wananchi wote kama watanzania na si wana ccm,chadema ama CCJ, nafasi zenye ku deal na usalama wa Taifa ie mkurugenzi wake, waziri wa mabo ya ndani nk,jeshi nk...
Ni muhimu bunge liwe linawapitisha watu kama hawa, naona siasa za vyama vingi ni maneno tu lakini mazingira hayaruhusu ama yana ukiritimba!
Ni kama CCM wanavyopractice ufisadi wa kibepari na wakati itikadi zao ni za kijamaa...Tufumbue macho!