Tanzania hii John ni Mmoja tu

Tanzania hii John ni Mmoja tu

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,499
Reaction score
139,724
Anaandika John Heche.

Kazi ya msajili ni kusajili vyama, kuvilea ili vikuze ushindani bora wa kisiasa ili Nchi yetu ipate maendeleo ya haraka ..

Kwa kupata sera mbadala na kuwapa wananchi nafasi ya kuchagua mtu wanemtaka.

Huyu bwana Mtungi kinyume chake ni kushambulia chama chetu kila siku.

Bwana Mtungi na ofisi yake kila mara amekua anaiandikia Chadema barua za vitisho, maonyo na kuzuia sisi kufanya wajibu wetu.

Bwana Mtungi na ofisi yake walikua nyuma ya kesi ya Saidi Issa kwa msajili Msaidizi kwenda kwa marehemu mama Komu kumshawishi na kufanikiwa kufungua kesi.

Bwana Mtungi na ofisi yake walikua nyuma ya yule bwana aliesema hamtambui katibu mkuu wa chama, manaibu katibu wakuu wote, wajumbe wa kamati kuu na mwanasheria mkuu.

Bwana Mtungi na ofisi yake wameshiriki kuwafuata baadhi ya wanachama na viongozi kuwashawishi kuchafua chama chetu na taswira ya viongozi wetu..

Kwahiyo bwana Mtungi anachotaka ni Nchi yenye vyama aina hiyo aliyonayo, vyama vya mfukoni ambavyo haviwezi kusimamisha hata wagombea kwenye mitaa kumi Nchi nzima..

Mtungi anataka sisi pia tuwe kama chui au nyoka wa maonesho awe anatuswaga na kutupeleka kwenye vikao na mikutano ya kuonesha dunia kwamba kuna vuma vingi wakati hakuna.

Mtungi Chadema ni chama serious cha wananchi kitakacholeta ukombozi wa kiuchumi, kukomesha rushwa, uzembe, upendeleo, uchawa na kurejesha heshima kwenye ofisi za umma.. Chadema ni chama cha kulinda utajiri wa Nchi na kuusimamia kuinua maisha ya wananchi .. kwahiyo hangaika na vyama vyako vya mfukoni..

Shame on you, wewe ni sehemu ya uchochezi na kujaza hasira umma dhidi ya utawala huu wa kidkteta, ofisi yako inachochea machafuko migawanyiko kwenye jamii.

My Take
Nchi hii John ni mmoja tu, majoni wewe ni Joni-shikizi
 
Ingekuwa video ingeenda viral zaidi na ingependeza mshaurini afanye hivyo mtu wenu wa chadema
 
Back
Top Bottom