Who is John Tendwa?

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wakuu,

Nasikitika zaidi ya kujua kuwa John Tendwa ni Msajili wa Vyama vya Siasa (Registrar of Political Parties) nchini lakini nashindwa kupata background yake kabisa.

Kama kuna wadau wanaweza kunisaidia (naamini itawasaidia wengine) kuweza kumjua vema ni nani, ametoka wapi, na hapa alipo tutarajie wapi ataelekea... (I doubt anaweza kuingia kwenye siasa na akawa upande wa chama 'flani').

Natanguliza shukrani kwa watakaonipa ushirikiano katika hili na huenda ikawasaidia wengi

==========
FROM HIMSELF (Tendwa):

Ametokea Mahakama ya Kazi ambapo alikuwa akifanya kazi kama Incharge alikotokea kuwa Msajili wa vyama vya siasa.

Amefanya kazi ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kwa muda wa miaka 23 (yeye ni mwanasheria, hakutoa details kwa kirefu; mwandishi wetu atahojiana naye na kutupa kwa undani)
 
Dah jamaa naona inawezekana HAJULIKANI kwa wengi... Yawezekana yakitolewa 'madudu' yake wengi watadhani ni kupakaziana na kuchafuliana majina!
 
Asante sana Invisible - na mimi nimewahi kujiuliza sana hili swali kuhusu John Tendwa. Nakumbuka siku akiteuliwa kuwa msajili wa vyama vya siasa wengi wetu tulipigwa na butwaa na tukabaki tukijiuliza katokea tena wapi huyu ?

Hebu wote wana JF tushirikiane tuweze kumfahamu huyu Tendwa kabla ya kupewa hiyo tenda alikuwa nani na alikuwa na sifa gani ?
 
Mkuu Masanilo,

Naona unaishia kwenye kugonga ukuta kama wengi tulivyojikuta tunaambulia patupu. Huyu jamaa inavyoelekea wengi wanaona anafanya kazi na hata wapinzani kuna uwezekano wamemwamini kiasi kwamba hakuna hata wa kuweza kutufahamisha who is he? Tukijua alikotokea mpaka akafikia alipo ni rahisi kuweza kujua huyu anatupeleka wapi.

Ni mtumishi wetu na ni vyema sisi tunaotumikiwa na bwana huyu tumfahamu vema.

Kilicho kwenye link yako ni hiki:

2u7lz4x.jpg

Asante sana Invisible - na mimi nimewahi kujiuliza sana hili swali kuhusu John Tendwa. Nakumbuka siku akiteuliwa kuwa msajili wa vyama vya siasa wengi wetu tulipigwa na butwaa na tukabaki tukijiuliza katokea tena wapi huyu ?

Hebu wote wana JF tushirikiane tuweze kumfahamu huyu Tendwa kabla ya kupewa hiyo tenda alikuwa nani na alikuwa na sifa gani ?
Mkuu Mag3,

Nimetafakari sana, lakini naamini kuna wadau kadhaa wanaweza kutupa kwa undani mtu huyu ni nani haswa kwa undani ili tuwe na imani naye na kujiridhisha kuwa tuna msajili wa vyama asokuwa na mawaa kabisa na mwisho wa utumishi wake tutaendelea kumuenzi kama mtanzania aliyetutumikia bila 'kutumiwa' ama vinginevyo.
 
Kipindi fulani alikuwa State Attorney kule Tabora.

Ila nasikia katika tukio moja kubwa wakati akiwa katika nafasi hiyo ni pale ambapo alichukua mke wa mtuhumiwa ambaye kesi yake alikuwa anaisimamia upande wa Jamhuri na hatimaye kufikia kumweka kinyumba na baya zaidi siku mojawapo ya usikilizaji wa shauri ilo eti Tendwa aliingia mahakamani akiwa na suti ya mtuhumiwa na kupelekea mtuhumiwa kuanzisha fujo mahakamani kwa kumwambia; mke wangu umenichukulia na suti yangu pia umeivaa tena kuja kwenye shauri la kuja kunifunga?

Mwenye stori kamili juu ya hii skendo amwage hapa jamvini... mi nimeipata mtaani
 
Jamaaa hana school mates, wa secondary, university ama kama alipitia JKT? Maana hata elimu yake haiko wazi, ni Mwanasheria sawa....alisoma wapi na alisomea kitu gani? LL.B ama LL.M
 
Yaani mawazo yenu yoote, Tendwa kawahujumu CCJ. Tukubalini tu jamani, CCJ wamejimaliza wenyewe, after all sijaona kitu special kwa CCJ mpaka eti kihujumiwe.
 
Yaani mawazo yenu yoote, Tendwa kawahujumu CCJ. Tukubalini tu jamani, CCJ wamejimaliza wenyewe, after all sijaona kitu special kwa CCJ mpaka eti kihujumiwe.
MKUU umechanganya madesa!!!

hapa watu wanatafuta kumjua huyu mtendaji "mahiri" wa tume ya uchaguzi, wewe unakuja na theories zako... kwenye kazi tunayo watanzania
 
Yaani mawazo yenu yoote, Tendwa kawahujumu CCJ. Tukubalini tu jamani, CCJ wamejimaliza wenyewe, after all sijaona kitu special kwa CCJ mpaka eti kihujumiwe.

"It is bad intelligent people make too bad error in judgement so late in their lives" Mario Puzo's Godfather
 
Yaani mawazo yenu yoote, Tendwa kawahujumu CCJ. Tukubalini tu jamani, CCJ wamejimaliza wenyewe, after all sijaona kitu special kwa CCJ mpaka eti kihujumiwe.
Ngoja na mimi nishangae why today? what happened?
 
Jamaaa hana school mates, wa secondary, university ama kama alipitia JKT? Maana hata elimu yake haiko wazi, ni Mwanasheria sawa....alisoma wapi na alisomea kitu gani? LL.B ama LL.M
Unaona eh? Yani inapokuja suala la Tendwa ni ngumu kupata mtu anayemwongelea kwa undani!

Ilulu walau katupa kidogo, aliwahi kuwa 'State Attorney' huko Tabora, we can now start connecting dots, hizo skandali zake mimi sintopenda kuziingilia, suala hapa ni elimu yake kaipatia wapi, kivipi na kapitia nafasi zipi kufikia aliyo nayo.

Yaani mawazo yenu yoote, Tendwa kawahujumu CCJ. Tukubalini tu jamani, CCJ wamejimaliza wenyewe, after all sijaona kitu special kwa CCJ mpaka eti kihujumiwe.
Hayo mambo ya CCJ wala hayapo kwenye hii issue mkuu, usije ukachanganya madesa kabisaa, tena tunapoenda mbele ningependa issue ya CCJ et all ikae pembeni, ni mtumishi wetu (na wako pia) hivyo kuweza kujua undani wake kielimu na kiutumishi ni jambo jema kabisa.

Endapo tutakumbana na mambo ambayo si ya kawaida haina budi kuyaangalia pia na kujua kwanini aliyafanya na athari yake kwa taifa ni ipi.

Nafikiri hili ni swali zuri sana maana JF huwa watu hawakurupuki tu katika mambo mengi...kuna lililojificha pengine hatulijui
Mkuu, tuna kitu tunatakiwa tukiweke sawa kabla ya 'Jambo' kuja kwenye kadamnasi... Naamini tukishamfahamu hasa CV yake itasaidia soon likiibuka lolote aidha la kumzushia au la uhakika kabisa juu yake tuweze kulihukumu bila kuegemea upande usio sahihi.

Mpaka sasa Elimu ya Tendwa na alikotokea mpaka afikie alipo ni kitendawili isipokuwa kwamba aliwahi kuwa 'State Attorney' huko Tabora (kwa mujibu wa Ilulu wa hapa JF).

Nothing personal!
 
one may ask... why now? yes its a good question lakini nadhani he was just very lucky not to be put under the microscope siku zote hizi... i think its a good policy sisi wana JF na wapenda nchi wote kuweka wazi wasifu wa all public figures ili tuwe comfortable na hata kuomba technical advices!! wako wachache wanafahamika na nimependa sana mtu kama Dr. Kafumu anavyohandle public demand for infomration bila kusema niandikie barua kwa ofisi

we need to know tendwa na kumjua haswaaaa...WHO IS JOHN TENDWA?
 
MKUU umechanganya madesa!!!

hapa watu wanatafuta kumjua huyu mtendaji "mahiri" wa tume ya uchaguzi, wewe unakuja na theories zako... kwenye kazi tunayo watanzania

Wala sijachanganya madesa, hicho ndo watu wanachokitafuta humu, just think of the timing
 
Tarehe 27/4/2001, Raisi Benjamin William Mkapa alimteua Bwana John Tendwa kuwa Msajili mpya wa Vyama vya Siasa akichukua nafasi ya George Christopher Liundi ambaye muda wake ulimalizika.

Kabla ya hapo John Tendwa alikuwa wapi na alikuwa anafanya nini - wana JF mpo? - msaada unatakiwa kwani giza lililotanda kuhusu historia yake linaleta wasi wasi.

Je ni Mtanzania? Alizaliwa wapi? Alisomea wapi?
 
Wala sijachanganya madesa, hicho ndo watu wanachokitafuta humu, just think of the timing

I beg to differ!!! I though ni ile issue ya rai kutania kila wakati ndio maana watu wakawa na interest ya kumjua the 'self proclaimed msemaji wa rais' wakati ana kazi ngumu ya kuandaa nchi kuelekea uchaguzi.

Lakini kama ilivyo ada, you are entitled to your opinion... maybe ni double timing
 
John tendwa mi nimewahi kusikia ni mhehe,halafu nikasikia ni mngoni.......
 
John tendwa mi nimewahi kusikia ni mhehe,halafu nikasikia ni mngoni.......
Walau tunaanza kupata japo kidogo kujua mkuu huyu kwa mbali, lakini inakuwaje hafahamiki kiasi hiki? Nawashukuru mnaoendelea kutufungua macho, nimetoa credit kwa kila anayeleta info yoyote katika kuutafuta ukweli juu ya mkuu huyu (on the first post)
 
Mkuu Invisible, i know you're still "Invisible" to some of us, but i wish we could know you, or if you're Kiyabo or Muhabi, mambo yangebadilika hapa, we need yu mkuu!
 
Back
Top Bottom