WhatsApp Status yangu

WhatsApp Status yangu

Nimecheka sana
Hawapost status ila kazi yao kubwa ni ku view 😅😅
Na hiyo ndio kazi yao sasa

Sioni tatizo mtu akipost
Sioni tatizo mtu asipo post pia

Ila wasio post kabisa wanajipaga ka umuhimu 😆😆🙌
Basi wanajipa umuhimu wa kijinga jinga sana. Wakati nje ya mambo ya watsap wote wanapitia changamoto zilezile tu.
 
Hivi ndivyo ilivyo Whatsapp status yangu kimaudhui

Dini (Mahubiri, nyimbo, Aya za biblia n.k)-50%
Mpira-20%

Matukio(ndoa, birthdays, misiba n.k)-20%
Fursa za uchumi,biashara-5%
Memes, Quotes-5%
Mkuu na wewe unakimbizana na kina dada kuweka status? Hiyo kitu sina muda nacho hata kidogo.
 
Hahaha RR jamani
Status ni kitu kingine, profile ni kitu kingine..

Ukitoka riadha uwa hauwamotivate viewers wako na Kill marathon 😀
Viewers wangu? Runners tuna apps za kukimbia huko huwa wanapost kila kitu. Kwenye Strava app yangu napost runs zangu tu ambayo ni automatically kazi ya App.
 
Hivi Nini kinafanya mtu umpost marehemu status?
Bongo nyoso. Watu wanagombania kwenye social media kuweka ''breaking news'' za misiba. Ulimbukeni mtupu. Kna shangazi yangu alifariki, hata kabla hatujawafahamisha mahusika, ki-demu kimoja cha jirani kikapost Facebook na picha yake ''siamini kama ni kweli umetuacha''. Hakikuwa na uhusiano naye wala ukaribu. Ni kiherehere tu cha kutaka kupeleka umbeya. Na hivi ndivyo walivyo wabongo wengi. Wanadhani kupost misiba social media ni uki-sasa, kwenda na wakati.
 
whatsapp hususan messenger iko fixed sana interact yake n locally sana kila ck circle n ile ile ya watu wale wale kwny contact list hii inaboa kwa ss 2naotaka kukutana na vitu vpya na watu wapya. mwaka wa 6 huu cpo huko.
 
Sijawahi kuweka status. Kwanza profile yenyewe iko vile vile haijawahi kuwekwa kitu chochote, unaweza kudhani unawasiliana na mizimu, maana binafsi sioni hiyo haja Kwanza namuonesha Nani?...Watu Tunatofautiana na huu ndo ubinadamu.
 
Back
Top Bottom