Wewe ni nani?

20PROFF

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
8,147
7,128
Habari wanajamvi.

Natumai kila mmoja yupo sawa kabisa. Nimekuwa nikijiwekea utaratibu wa siku za weekend nikiwa off-duty, kuwa mbali na simu, TV, PC au kitu chochote cha teknolojia kitachochukua atention. Saa zingine naamua kuchukua peni na note book yangu na kuamua, either kukaa somewhere kwenye fresh air, au kwenye mchanganyiko wa watu kuangalia mizunguko na pilika zao.

Nilicho gundua kuwa mind yako inavitu vingi sana ambavyo unaweza faida navyo, tatizo hutoi au hauipi muda wa yenyewe ku-manifest zaid ya kuangalia au kusoma wanacho sema wengine,.

Jaribu siku moja kufanya hivyo utakuja gundua mengi.

Lengo la uzi si hilo lakini ni jambo linalo husiana na hilo ukiangalia kwa undani.

Labda nianze na maswali machache, mengine wadau au mwenyew unataweza jiuliza na kujiongeza kichwani.

JE , WEWE NI NANI??

IDENTITY AU UTAMBULISHO WAKO NI JINA ULILO PEWA??

UTAMBULISHO WAKO NI DINI?, KABILA?

IKITOKEA UKIBADILI DINI UTAMBULISHO WAKO UTAKUWA NINI?

UKIJIPA AKA AU JINA MBADALA UTAMBULISHO WAKO UTAKUWA MWINGINE??

Kwa kifupi tumekuwa watumwa au kufungwa kimawazo na kiimani, kupigania fake identity, image ya kutengenezewa na watu wanaotuzunguka.

Ukifikiria kwa undani utakuwa hata tabia, mienendo yako ya sasa si yako bali ni ishu unayo tawaliwa na system uliyowekewa na watu waliokupa hiyo fake identity na wewe unaisha kuifata.

Mfano, umezaliwa ukaambiwa wewe ni imani flan au kabila flan. Basi utajifunza njia na jinsi ya kuishi kulingana na hizo imani, why usijifunze kuishi kulingana na nafsi yako ilivyo ndani??

Mwisho wa siku huwezi kuwa full package kabisa au kutumia vipawa vyote ulivyo umbiwa navyo, kwa sababu vimefukia baada ya wewe kuacha your true identity, utambulisho wako halisi na kufata identity walizo weka wengine, kipindi haupo duniani..
.
IMG_20170402_191738.jpg



Ishi kwa uhuru japo kwa wiki, bila kufungwa na sheria zozote za identity yako, then utaona mengi sana.
 
"Ishi kwa uhuru japo kwa wiki, bila kufungwa na sheria zozote za identity yako, then utaona mengi sana"
ebu naomba kuelewa vizuri hapa
labda alikuwa anamaanisha uhuru gani haswa? na ni sheria gani hizo zinazotufunga?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hii kitu naanza kuifanyia kazi tumetekwa sana na mitandao hatujipi nafasi ya kujitafakar wenyew
Upo sahihi ndugu.

Cha msingi, kaaa mbali na utandawazi ,jipe muda kutafakari ulicho nacho. Utaona mengi
 
"Ishi kwa uhuru japo kwa wiki, bila kufungwa na sheria zozote za identity yako, then utaona mengi sana"
ebu naomba kuelewa vizuri hapa
labda alikuwa anamaanisha uhuru gani haswa? na ni sheria gani hizo zinazotufunga?
Dini, imani za ukabila , misingi na ratiba kulingana au kutaka kukop na mazingira au watu fulani. ..

Hapa kuna masheria kibao ambayo ya kutawala bila kujijua...
 
Kwa maana nyingine jamii inayotuzunguka ndio inatuumbia maisha tunayoishi. Tena haya mambo huku kwetu africa ndo kabisaa.Utakuta mtu unalazimika kuhudhuria hizi jumuiya za kidini bila kupenda, eti usipofanya hivo wanakutenga hasa unapopata matatizo. Hii inanikera sana. Au usipoenda kanisani au msikitini utakoma wanakusubiria upate matatizo.Sasa utakuta watu tunaishi kama watumwa wa dini na mila zetu au taratibu fulani ambazo hata sio sheria, kwa mfano utakuta wakati mwingine mtu unapenda kuishi maisha yako bila kuoa au kuolewa lakini unalazimika kufanya hivo eti kwa vile sio kawaida watu kuishi maisha hayo huku kwetu. Au wakati mwingine hujabarikiwa kupata mtoto, unalazimika kutafuta kwa nguvu ikibidi hadi kupoteza maisha kwa vile eti watu wote ni lazima wawe na watoto maishani. Huu ni utumwa. Ipo mifano mingi. Ukweli tunatakiwa kuishi maisha yetu ili mradi tusiwadhuru wengine.
 
Back
Top Bottom