Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,392
- 7,863
Hata kwenye job interview swali gumu Sana Hili who are you?
Maisha ni kuchagua.Huku duniani tuko watu waaina nyingi sana ,
Mimi shitaji kujua kwenye sayari anaishi nani mda huo ntautumia kuongeza bidii kuzalisha bidhaa na kuziuza jioni nabeba mchuchu wangu bia kiasi game la maana ,Napambana nipunguze kutokuwa sehemu ya kuumiza wengine ikiwemo wasio wanadamu ,siwezi uwa panzi kama simli wala hanidhuru ,dini kidogo sana ,naamini who ever created us main purpose ni tufanyekazi tuzalishe kisha tufurahiye kazi ya mikono yetu ,naelewa nikijiingiza kuwaza naweza jua purpose zisizonihusu za kwake ambazo ovious sio zangu then let me enjoy may time ,and die.
Mmetofautiana na mtoa mada na huyo unaemjibu kwenye context.Ivi siku zoote hizi hujui wewe ni nani?
Unapoitwa na kuitika
"Naam"
Ivi unajuaje kama umeitwa wewe ?
Au mtu akikuambia wewe ni "KOBE"
Utakubali ?
Kama utakataa basi unajijua kuwa wewe siyo kobe bali ni ......
na unatambua
Tena wewe ni wa jinsia
ya .....
na unajua
Na tufanye "MTU" kwa mfano wetu akatawale nchi na kila kilichomo.
Nina
Mwili....umbo
Nina
Nafsi....mimi
Nina
Roho...uzima
Jumla
Mtu...Binadamu.
Mwili...
-fomula ya kuniwezesha kuishi duniani hapa nilipo.
-mtendaji mkuu wa hapa duniani
-mf. Kupiga, kulima
-Huzaliwa, hukua,hufa
Nafsi...
-Utambulisho wangu unaonitofautisha na wewe, yeye,
-mwamuzi wa mambo hapa nilipo
-mf. Nakupenda, nitakuoa.
-Ukifa mwili anabaki na Roho
Roho...
-Uhai, uliopulizwa na pumzi ya Mungu,
-kiongozi mwenye mahusiano ya karibu na Mungu.
-Hafi, hauwawi na ki-adui chochote isipokuwa Mungu pekee ndiye anayeweza kumtowesha pamoja na utambulisho wake, Nafsi.
Samahanini ni mtazamo wangu tu.
Mmetofautiana kuelewana.Eti Uhuru kuwa huru
Uhuru gani mnauzungumzia haswa naona hamjawa wazi.
Aliyetengeneza gari alitoa masharti ya kuliendesha
Linahitaji mafuta, maji nk.
Wenzetu mnaodai uhuru, hebu mgundue chakula chenu tofauti na kile aliyewaumba amewaagiza mle.
Undeni hewa yenu ya kupumua
Tengenezeni maji yenu ya kunywa kwa kutafakari na kumediteti
Muwakae wanawake wasiwe wasaidizi wenu, mtengeneze aina yenu ya wasaidizi kama mnawataka
Kumbukeni mmejikuta mmezaliwa bila kuingia mkataba na mtu yeyote.
Nani mlikubaliana naye muwe wanawake au wanaume ?
Semeni wazee wa kutafakari
Leteni majibu.
Kama mmejigundua mmezaliwa bila hiyari yenu inabidi muingiwe na woga kwanza wa kuona kwanini mpo bila kuhusika katika makubaliano ya kuwepo kwenu.
Pia kwanini mlipoambiwa ,samaki, wanyama, majani ya miche na matunda, kitakuwa chakula chenu mlikubali bila kubisha.
Kwani hamuwezi kubuni chakula chenu kwa kutahajudi jadidi ?
Si mnahekima nyie, muwakatae na mama zenu kwani mnapenda eti kujipangia mambo kwa kutafakari, nani aliwachagulieni mama zenu wakuzaeni nyie, kwanini hamkushiriki kuwachagua mama zenu badala ya hao walio wazaa.
Nataka kuwaelimisha tu kuwa iko asili na ndiyo inayopanga mwanzo na hatima zetu.
Sisi tuna uhuru wa kufanya tunayo amrishwa na mu asili wetu
Kumbuka hata sasa ukitaka kufa huwezi ukafa hadi uchukue ki adui cha kukuwezesha kujiua.
Kwanini usife tu kwa kutafakari kijadidi ?
Yako mambo na kanuni umewekewa na aliye ku plani uwe, na inabidi uyafuate utake usitake kama unabisha anza leo kula mchanga badala ya chakula ulichoamliwa ule halafu subiri mwisho wake.
Mtoto mdogo akitakari kutaka kuendesha lori la mchanga litamshinda tu hataweza.
Wewe una mambo ya makamu yako ya kuyawaza na kuyafanya yameandikwa kwenye vitabu yanafundishwa mashuleni.
Wengine mnataka eti mutafakari hadi muache kiwiliwili chenu na kusafiri na roho au nafsi mtakuja kufa bule, sio mambo ya makamu yenu,
Huyo aliyewaumba atawapa uwezo huo wakati atakapo ona inafaa, kama wewe unavyo amua kumpeleka mtoto shule wakati wewe mzazi unapoona sasa amekomaa kuweza kusoma.
Mumsikilize huyo aliyewaleta duniani kuwa anataka mfanye nini cha makamu yenu.
Eti mnajidanganya tunaka kuwa huru...!
Mlijiumba ? au nyinyi ni mali yenu hata mutake kujiamulia mambo.
Mnajua jicho lenu moja tu lina thamani kuliko madini ya dunia yote ikiyauza na huwezi kulinunua.
Ivi watoto wenu hamuwafundishi lolote ? kwani hamutaki kuwapa uhuru wajitafakari na kujiamulia mambo yao wenyewe bila bugdha yenu.
Mbona hamkatai kuwa na macho, eti mna tegemea jicho la tatu, ng'oeni basi hayo mawili mtumie hilo la tatu.
Wacheni ujinga someni biblia takatifu mtapata maaria ya huyo aliyewaumba anataka nini mfanye.
Hapa hakuna uhuru, yaani mtu akuumbe halafu useme una uhuru wa kumtukana, we unakubali mtoto wako akutukane hadharani kwakuwa yuko huru kuchagua cha kusema ?
Unaweza kujitegemea hadi uwe huru? yani ujitengeneze mwenyewe na ujiishi mwenyewe.
Kama unategemea mwili uliobuniwa na kutengenezwa na mtengenezaji wako na unakula chakula chake na kunywa maji yake na kuvuta hewa yake halafu unasema uko huru unajidanganya.
Utatafakari hadi uchanike nyongo, lazima umsikilize na kufuata maagizo ya anayekulisha chakula, la sivyo utakiona cha mtema kuni kama anavyosema
na kibaya zaidi uwezo wa kumkimbia huna, ha....ha....ha....loh...
Someni biblia takatifu kwani hekima yenu ipo humo.
Ufahamu wenu umeelezwa,
Muumbaji wenu amejidhihilisha humo.
Nani unapaswa ufanye utasoma humo
Hayo mengine yanatoka kwa Ibilisi anayetaka kuwapoteza kama yeye alivyo potea.
Samahanini sina nia ya kuwaudhi bali kuwaonyesha Njia, Kweli na Uzima wenu ulipo
Uku huru kuchagua, Kifo au Maisha.
Hata hujacheza nje ya mada, ila umesema jambo, ambalo watu wengi wana lisahau.Katika maisha haya kuna mambo mengi sana ya ajabu ajabu kabisaa... Sisi binafsi tuna uwezo wa kumudu kitu chochote au jambo lolote bila usaidizi wowote, sasa shida ni kuwa tunajizoesha mno kuwa tegemezi, wa kila kitu. Mfano kuna mtu anaweza kuua Simba kwa mikono yake na kuna mtu anaweza kuua Simba kwa mkuki na kuna mtu anaweza kuua Simba kwa bunduki na mwingine kwa kutoa order tu nae ataesabika kuwa kamanda fulani alisababisha yule Simba hatari kuuwawa.
Sasa mambo hayo yote yatakinzana na ukweli halisi iliyopo ndani yetu, ambao tunaupoteza kwa kuendelea kuwa wategemezi mno. Wajuzi wa masuala ya wanyama wamesema ukimwangalia Simba bila kupepesa macho wala kuogopa utakuwa unampa wakati mgumu sana kukudhuru, lakini je? Unaweza kufanya hivyo hii leo katika ulimwengu huu tegemezi tuliojiwekea? Kweli hatujijui sisi ni nani kabisaaaaa. Kwa kumalizia tu, maana nahisi nimetoka nje ya mada, siku moja nilikuwa nataka kufanya mahesabu na mkaka mmoja hivi.. sasa si ndo nikatoa ki simu changu ili kitusaidie kufanya mahesabu!!!! Mkaka alinishangaa sana kisha akasema yeye atafanya kwa kichwa tu bila utegemezi wa kikokotoleo, na kwa kweli mahesabu yalikuwa mengi sana na alifanya vyema na kwa haraka zaidi huku mimi mtegemezi nikibaki natumbua mimacho tu, NOTE "siku hizi hata wafanyakazi wa serikalini ukiwauliza leo ni tarehe ngapi? hawajui hadi waangalie kalenda kwenye simu zao"
I second you...Katika maisha haya kuna mambo mengi sana ya ajabu ajabu kabisaa... Sisi binafsi tuna uwezo wa kumudu kitu chochote au jambo lolote bila usaidizi wowote, sasa shida ni kuwa tunajizoesha mno kuwa tegemezi, wa kila kitu. Mfano kuna mtu anaweza kuua Simba kwa mikono yake na kuna mtu anaweza kuua Simba kwa mkuki na kuna mtu anaweza kuua Simba kwa bunduki na mwingine kwa kutoa order tu nae ataesabika kuwa kamanda fulani alisababisha yule Simba hatari kuuwawa.
Sasa mambo hayo yote yatakinzana na ukweli halisi iliyopo ndani yetu, ambao tunaupoteza kwa kuendelea kuwa wategemezi mno. Wajuzi wa masuala ya wanyama wamesema ukimwangalia Simba bila kupepesa macho wala kuogopa utakuwa unampa wakati mgumu sana kukudhuru, lakini je? Unaweza kufanya hivyo hii leo katika ulimwengu huu tegemezi tuliojiwekea? Kweli hatujijui sisi ni nani kabisaaaaa. Kwa kumalizia tu, maana nahisi nimetoka nje ya mada, siku moja nilikuwa nataka kufanya mahesabu na mkaka mmoja hivi.. sasa si ndo nikatoa ki simu changu ili kitusaidie kufanya mahesabu!!!! Mkaka alinishangaa sana kisha akasema yeye atafanya kwa kichwa tu bila utegemezi wa kikokotoleo, na kwa kweli mahesabu yalikuwa mengi sana na alifanya vyema na kwa haraka zaidi huku mimi mtegemezi nikibaki natumbua mimacho tu, NOTE "siku hizi hata wafanyakazi wa serikalini ukiwauliza leo ni tarehe ngapi? hawajui hadi waangalie kalenda kwenye simu zao"