Wewe ni nani?

Wewe ni nani?

Mh huu uzi alikuja nao apoloulikaa vizur zaid naona mkuu kama umekop flan ivi
 
ukitaka kujua wewe ni nani nenda kaishi msituni,bila jina,kula matunda na mizizi,pambana na wanyama kiujumla ishi maisha yakinatural hlf jiulize wewe ni nani utapata jibu..
 
ANATOMY OF THE SPIRIT.
Wasome hiki kitabu vizuri wataelewa taratibu.........
 
Kwa maana nyingine jamii inayotuzunguka ndio inatuumbia maisha tunayoishi. Tena haya mambo huku kwetu africa ndo kabisaa.Utakuta mtu unalazimika kuhudhuria hizi jumuiya za kidini bila kupenda, eti usipofanya hivo wanakutenga hasa unapopata matatizo. Hii inanikera sana. Au usipoenda kanisani au msikitini utakoma wanakusubiria upate matatizo.Sasa utakuta watu tunaishi kama watumwa wa dini na mila zetu au taratibu fulani ambazo hata sio sheria, kwa mfano utakuta wakati mwingine mtu unapenda kuishi maisha yako bila kuoa au kuolewa lakini unalazimika kufanya hivo eti kwa vile sio kawaida watu kuishi maisha hayo huku kwetu. Au wakati mwingine hujabarikiwa kupata mtoto, unalazimika kutafuta kwa nguvu ikibidi hadi kupoteza maisha kwa vile eti watu wote ni lazima wawe na watoto maishani. Huu ni utumwa. Ipo mifano mingi. Ukweli tunatakiwa kuishi maisha yetu ili mradi tusiwadhuru wengine.
Hapo kwenye kuishi maisha yetu mradi tusiwadhuru wengine ndiyo point, ila wako wengine ambao kuwadhuru wengine ndiyo hasa uhalisia wao! So ni vema kuongozwa na miongozo iliyopo ili kupata angalau mwanzo wa kujitathmini namna tunavyoweza kuwa katika uhalisia wetu na faida tutakazo ipatia jamii inayotuzunguka kuliko kuwa wabinafsi sana sababu tu, tunataka kuwa katika uhalisia wetu na kusababisha madhara kwa wengine pasipo kufahamu.
 
Kweli kabisa mkuu.
Hata mm kuna muda huwa najaribu kuishi kama nakujiondolea sheria nilizozikuta na najikuta naienjoy sana maisha.
Ukiangalia sana ni moja kati ya mbinu inayokuwezesha kuishi maisha ya furaha.
 
Mnaongea mambo ya kufikirika tu hayana uhalisia,katika wote wanaokujaga na hizi story hakuna hata mmoja aliyejibu yeye ni nani. Hakuna maisha yenye Uhuru kwa hivyo muelezavyo nyie.
Ni sawa kabisa, kwa sababu kuna changamoto nyingi utakabiliana nazo hasa ukiwa tofauti na mfumo ulioukuta, pia inaweza ikahitajika nguvu kubwa sana kubadili mfumo uendane na uhalisia ulionao
 
Eti Uhuru kuwa huru
Uhuru gani mnauzungumzia haswa naona hamjawa wazi.

Aliyetengeneza gari alitoa masharti ya kuliendesha
Linahitaji mafuta, maji nk.

Wenzetu mnaodai uhuru, hebu mgundue chakula chenu tofauti na kile aliyewaumba amewaagiza mle.
Undeni hewa yenu ya kupumua
Tengenezeni maji yenu ya kunywa kwa kutafakari na kumediteti

Muwakae wanawake wasiwe wasaidizi wenu, mtengeneze aina yenu ya wasaidizi kama mnawataka

Kumbukeni mmejikuta mmezaliwa bila kuingia mkataba na mtu yeyote.

Nani mlikubaliana naye muwe wanawake au wanaume ?

Semeni wazee wa kutafakari
Leteni majibu.

Kama mmejigundua mmezaliwa bila hiyari yenu inabidi muingiwe na woga kwanza wa kuona kwanini mpo bila kuhusika katika makubaliano ya kuwepo kwenu.

Pia kwanini mlipoambiwa ,samaki, wanyama, majani ya miche na matunda, kitakuwa chakula chenu mlikubali bila kubisha.

Kwani hamuwezi kubuni chakula chenu kwa kutahajudi jadidi ?

Si mnahekima nyie, muwakatae na mama zenu kwani mnapenda eti kujipangia mambo kwa kutafakari, nani aliwachagulieni mama zenu wakuzaeni nyie, kwanini hamkushiriki kuwachagua mama zenu badala ya hao walio wazaa.

Nataka kuwaelimisha tu kuwa iko asili na ndiyo inayopanga mwanzo na hatima zetu.

Sisi tuna uhuru wa kufanya tunayo amrishwa na mu asili wetu
Kumbuka hata sasa ukitaka kufa huwezi ukafa hadi uchukue ki adui cha kukuwezesha kujiua.
Kwanini usife tu kwa kutafakari kijadidi ?

Yako mambo na kanuni umewekewa na aliye ku plani uwe, na inabidi uyafuate utake usitake kama unabisha anza leo kula mchanga badala ya chakula ulichoamliwa ule halafu subiri mwisho wake.

Mtoto mdogo akitakari kutaka kuendesha lori la mchanga litamshinda tu hataweza.

Wewe una mambo ya makamu yako ya kuyawaza na kuyafanya yameandikwa kwenye vitabu yanafundishwa mashuleni.

Wengine mnataka eti mutafakari hadi muache kiwiliwili chenu na kusafiri na roho au nafsi mtakuja kufa bule, sio mambo ya makamu yenu,

Huyo aliyewaumba atawapa uwezo huo wakati atakapo ona inafaa, kama wewe unavyo amua kumpeleka mtoto shule wakati wewe mzazi unapoona sasa amekomaa kuweza kusoma.

Mumsikilize huyo aliyewaleta duniani kuwa anataka mfanye nini cha makamu yenu.

Eti mnajidanganya tunaka kuwa huru...!

Mlijiumba ? au nyinyi ni mali yenu hata mutake kujiamulia mambo.

Mnajua jicho lenu moja tu lina thamani kuliko madini ya dunia yote ikiyauza na huwezi kulinunua.

Ivi watoto wenu hamuwafundishi lolote ? kwani hamutaki kuwapa uhuru wajitafakari na kujiamulia mambo yao wenyewe bila bugdha yenu.

Mbona hamkatai kuwa na macho, eti mna tegemea jicho la tatu, ng'oeni basi hayo mawili mtumie hilo la tatu.

Wacheni ujinga someni biblia takatifu mtapata maaria ya huyo aliyewaumba anataka nini mfanye.

Hapa hakuna uhuru, yaani mtu akuumbe halafu useme una uhuru wa kumtukana, we unakubali mtoto wako akutukane hadharani kwakuwa yuko huru kuchagua cha kusema ?

Unaweza kujitegemea hadi uwe huru? yani ujitengeneze mwenyewe na ujiishi mwenyewe.

Kama unategemea mwili uliobuniwa na kutengenezwa na mtengenezaji wako na unakula chakula chake na kunywa maji yake na kuvuta hewa yake halafu unasema uko huru unajidanganya.

Utatafakari hadi uchanike nyongo, lazima umsikilize na kufuata maagizo ya anayekulisha chakula, la sivyo utakiona cha mtema kuni kama anavyosema
na kibaya zaidi uwezo wa kumkimbia huna, ha....ha....ha....loh...

Someni biblia takatifu kwani hekima yenu ipo humo.
Ufahamu wenu umeelezwa,
Muumbaji wenu amejidhihilisha humo.
Nani unapaswa ufanye utasoma humo

Hayo mengine yanatoka kwa Ibilisi anayetaka kuwapoteza kama yeye alivyo potea.

Samahanini sina nia ya kuwaudhi bali kuwaonyesha Njia, Kweli na Uzima wenu ulipo

Uku huru kuchagua, Kifo au Maisha.
Hahaha umenikumbusha jamaa mmoja anaitwa Aguri aliyempatia mausia Ithnieli na Ukali, "Ni nani aliyekama upepo kwa makonzi yake? Mit 30:1- - - asante sana mtumishi. Maana maonyo uliyoyatoa hahaha, nimebarikiwa. Mwenye ufahamu na afahamu.
 
You are not what you think you are but as what you think is what you are.
 
Nita update mkuuuu nikisettle
Bro kwann umehisi kuwa kilaMTU anakitu driving factor .......bila shaka wanaokuzunguka umeona kitu cha utofaut sana na wew....

Unaweza kukaa mwaka mzima bila kuwa na smartphone????? Kama mawasiliano ukawa unatumia simu ndogo tu in case unahtaj taarfa flan may be unaazima .my point is unaweza kuwa mbali na smartphone just for a while?
 
Kuna mtu mmoja anaitwa Pascally Mayalla humu aliwahi kuja na Uzi "Physic powers" Kwa waliomfuatilia Kwa undani nafikiri wanaweza kukubali kuwa huu Uzi hauna tofauti na alichokielezea bwana Pascally, Alizungumzia juu ya ukomo wa mipaka (Limitation of boundaries), Hiki kitu kinatutesa sana na kinatufanya kuwa watumwa sana, hadi tunajikuta tunashindwa kujiamini na kuwa na maamuzi yenye tija ktk maisha yetu, kimsingi haya ni Mambo yanayohitaji ujipe muda, Lakini tunajikuta tukishindwa kujipa huo muda kutokana eidha kwa kukosa miongozo sahihi au kubanwa na ratiba za Kila siku ili mkono uende kinywani mfano mdogo ukijaribu kutafakari hivi mtu aliyegundua teknolojia ya mawasiliano alikuwa na akiri ya namna gani? Lakini unakuta ni utulivu wa hali ya juu ndo uliompa uwezo wa kundua Hiki tunachokiona ni cha ajabu, mbaya zaidi baada ya kukigundua anatuletea sisi ili tukariri tafakuri yake kwa muda mrefu kwa kile tunachodai kuwa ni elimu ya chuo kikuu, kiukweli we lost a lot of time, hatuna namna ni lazima tufuate mawazo ya walioiona Dunia mapema ili maisha yaendelee.
 
Habari wanajamvi.

Natumai kila mmoja yupo sawa kabisa. Nimekuwa nikijiwekea utaratibu wa siku za weekend nikiwa off-duty, kuwa mbali na simu, TV, PC au kitu chochote cha teknolojia kitachochukua atention. Saa zingine naamua kuchukua peni na note book yangu na kuamua, either kukaa somewhere kwenye fresh air, au kwenye mchanganyiko wa watu kuangalia mizunguko na pilika zao.

Nilicho gundua kuwa mind yako inavitu vingi sana ambavyo unaweza faida navyo, tatizo hutoi au hauipi muda wa yenyewe ku-manifest zaid ya kuangalia au kusoma wanacho sema wengine,.

Jaribu siku moja kufanya hivyo utakuja gundua mengi.

Lengo la uzi si hilo lakini ni jambo linalo husiana na hilo ukiangalia kwa undani.

Labda nianze na maswali machache, mengine wadau au mwenyew unataweza jiuliza na kujiongeza kichwani.

JE , WEWE NI NANI??

IDENTITY AU UTAMBULISHO WAKO NI JINA ULILO PEWA??

UTAMBULISHO WAKO NI DINI?, KABILA?

IKITOKEA UKIBADILI DINI UTAMBULISHO WAKO UTAKUWA NINI?

UKIJIPA AKA AU JINA MBADALA UTAMBULISHO WAKO UTAKUWA MWINGINE??

Kwa kifupi tumekuwa watumwa au kufungwa kimawazo na kiimani, kupigania fake identity, image ya kutengenezewa na watu wanaotuzunguka.

Ukifikiria kwa undani utakuwa hata tabia, mienendo yako ya sasa si yako bali ni ishu unayo tawaliwa na system uliyowekewa na watu waliokupa hiyo fake identity na wewe unaisha kuifata.

Mfano, umezaliwa ukaambiwa wewe ni imani flan au kabila flan. Basi utajifunza njia na jinsi ya kuishi kulingana na hizo imani, why usijifunze kuishi kulingana na nafsi yako ilivyo ndani??

Mwisho wa siku huwezi kuwa full package kabisa au kutumia vipawa vyote ulivyo umbiwa navyo, kwa sababu vimefukia baada ya wewe kuacha your true identity, utambulisho wako halisi na kufata identity walizo weka wengine, kipindi haupo duniani..
.View attachment 490393


Ishi kwa uhuru japo kwa wiki, bila kufungwa na sheria zozote za identity yako, then utaona mengi sana.

Mwaka 2011 au 2012, Mchungaji wetu Kanisani alitumia muda mrefu kiasi kufundisha somo la UFAHAMU. Mbali na kutoa maana ya ufahamu, kikubwa kupita vyote nilichochukua kutoka kwenye somo hilo kinatokana na maneno aliyosema kuwa USIPOKUWA NA UFAHAMU SAHIHI, UTAKUWA UNACHUKULIWA NA UPEPO WA ELIMU YA KILA AINA INAYOKUJA MBELE YAKO. Pia **** Mchungaji mwingine tena kwenye miaka hiyo hiyo alikuja kuendesha semina Kanisani kwetu, akasema kuwa SHETANI HUWA ANA VIMBWANGA VYA KILA AINA, ANAWEZA KUFANYA MAAJABU AMBAYO MWANADAMU ASIYEKUWA NA UFAHAMU SAHIHI ANAWEZA AKADHANI NI MUNGU ANAFANYA KUMBE HAPANA.Akaongeza akasema, HATA UKITAKA UUONE MOTE KATIKA UPOTEVU, UTAUONA, yaani ukitaka Shetani alete moto uuone, ni kazi rahisi tu kwake kama mtoto kunyonya ziwa la mama. Hata hivyo haya maneno nimeyaandika yakiwa si EXACT QUOTES za wachungaji hawa, ila ni exact meaning ya kile walichowahi kusema
 
Mwaka 2011 au 2012, Mchungaji wetu Kanisani alitumia muda mrefu kiasi kufundisha somo la UFAHAMU. Mbali na kutoa maana ya ufahamu, kikubwa kupita vyote nilichochukua kutoka kwenye somo hilo kinatokana na maneno aliyosema kuwa USIPOKUWA NA UFAHAMU SAHIHI, UTAKUWA UNACHUKULIWA NA UPEPO WA ELIMU YA KILA AINA INAYOKUJA MBELE YAKO. Pia **** Mchungaji mwingine tena kwenye miaka hiyo hiyo alikuja kuendesha semina Kanisani kwetu, akasema kuwa SHETANI HUWA ANA VIMBWANGA VYA KILA AINA, ANAWEZA KUFANYA MAAJABU AMBAYO MWANADAMU ASIYEKUWA NA UFAHAMU SAHIHI ANAWEZA AKADHANI NI MUNGU ANAFANYA KUMBE HAPANA.Akaongeza akasema, HATA UKITAKA UUONE MOTE KATIKA UPOTEVU, UTAUONA, yaani ukitaka Shetani alete moto uuone, ni kazi rahisi tu kwake kama mtoto kunyonya ziwa la mama. Hata hivyo haya maneno nimeyaandika yakiwa si EXACT QUOTES za wachungaji hawa, ila ni exact meaning ya kile walichowahi kusema
Nakusoma mzee. Ufaham ndio kikubwa mno ukitaka kumtumikisha tu, kwa namna yeyote.
 
Back
Top Bottom