de Gunner
JF-Expert Member
- Nov 2, 2021
- 11,375
- 22,568
Kabla sijaanza, nataka niweke wazi kuwa spiritual awakening si sawa na dini. Dini mara nyingi hutufundisha namna ya kumtafuta Mungu nje yetu, lakini spiritual awakening ni safari ya kujitambua ndani yetu. Si kuhusu kubadilisha dini, kuacha imani fulani au kuwa “mtakatifu”… bali ni kuanza kuhoji reality, ego, suffering na true nature yetu ya ndani.
Wengine hupitia hii kupitia dini, maumivu, upweke, meditation, mapenzi, au hata kuvunjika kabisa kiakili na kihisia. Mwisho wa yote, safari hii humrudisha mtu karibu zaidi na essence yake ya kweli.
Leo nataka tupige stori kuhusu hii dhana ya kiroho inayoitwa non-duality (kutokuwa na mgawanyiko wa kweli kati ya “mimi” na “wewe”). Hata kama hujishughulishi sana na spiritual matters, naamini umewahi kusikia kuhusu hii concept! Na kama bado… basi unaweza kuichunguza kidogo maana ni jambo la kuvutia sana.
Tangu nilipoanza safari yangu ya kiroho, imekuwa safari ngumu sana. Mara nyingi huwaambia watu wasikurupuke kuingia kwenye hii njia, maana ukishaingia ndani yake, hakuna kurudi nyuma mpaka upitie kila hatua yake. Na ukweli ni kwamba, inaweza kuwa ya maumivu, kuchanganya na kuvunja kabisa ule uelewa wako wa zamani.
Hatua nne zinazoweza kutokea kwenye spiritual awakening ni hizi:
1: Kutokuwa na ufahamu (Unconsciousness)
Hii ni hatua ambayo ego ndiyo inaongoza maisha yako, na utambulisho wako wote unakuwa umefungwa kwenye mawazo, conditioning na programming ulizokulia nazo.
2: Kifo cha ego (Dark night of the soul)
Hapa ndipo ule mfumo wako wa zamani wa kufikiri unaanza kuvunjika. Reality yako inaanza kubadilika, na hali hii huleta maumivu makubwa kwa sababu vitu vya kimwili vilivyokuwa vinakupa furaha au kukutambulisha vinaanza kuonekana vya uongo au havina maana tena kulingana na uelewa mpya unaochipuka ndani yako.
3: Kutafuta (The search)
Baada ya kupitia mateso na maumivu mengi, unaanza polepole kuingia kwenye ulimwengu usiojulikana. Kuna kitu ndani ya roho yako kinakuvuta kuelekea ukweli ambao bado hujaugundua kikamilifu. Inaweza kuogopesha, lakini ukiendelea mbele kwa imani, utaanza kutembea kwa faith badala ya sight.
4: Kuzaliwa upya (Rebirth)
Baada ya safari ndefu ya kutafuta, siku moja unaweza kupata glimpse ya true nature yako. Ile hali ambayo imekuwa ndani yako tangu ukiwa mtoto mdogo. Itahisi kama kukutana na soulmate wako. Hakuna maneno yanaweza kuelezea hiyo feeling. Utahisi uko nyumbani ndani yako mwenyewe na hata nje yako.
Kwa hizo hatua chache, naamini unaweza kuona jinsi safari ya kiroho ilivyo. Kumbuka, hii si journey yenye mwisho… ni deaths and rebirths zisizoisha. Na mara nyingi hizo hatua zinaweza kutokea kwa wakati mmoja au zisifuate mpangilio kabisa.
Kwa upande wangu, kila baada ya phase fulani ya awakening kwenye maisha yangu, nimekuwa nikihisi hii hali ya non-duality ambapo nahisi hakuna “mimi” wala “wewe”… kila kitu kinaonekana kuunganishwa.
Nafikiri mmegundua pia jinsi watoto wadogo au viumbe wachanga — iwe ni binadamu, ndege au wanyama — wanavyokuwa na hii hali naturally ndani yao.
Nilikuwa naangalia clip moja YouTube siku nyingine nikawaona watoto wa mbwa wakicheza na mtoto mchanga wa kibinadamu, na honestly connection yao ilikuwa beyond words. Pia mmegundua jinsi babies wanavyovutiwa sana na wanyama au hata watu wengine wenye energy fulani ya utulivu na uwepo wa kina?
Naam, hiyo ndiyo essence yetu ya msingi… sisi sote tumeunganishwa.
Kama wewe ni mtu wa kiroho, mara nyingi utaona hata wanyama wanakuwa attracted kwako. Wanaweza kuhisi hiyo pure energy inayotoka ndani ya soul yako.
Ulimwengu umeunganishwa kwenye msingi wake kabisa. Ni miaka ya hivi karibuni tu ambapo hata scientists wameanza kuzungumzia possibilities hizi kupitia quantum mechanics, lakini kwenye spiritual world mambo haya yamekuwa yakizungumziwa kwa maelfu ya miaka.
Kwa hiyo mimi, wewe na kila kitu kingine ni sehemu ya umoja mmoja. Hakuna separation ya kweli.
Ningependa kumalizia na quote niliyosikia kwenye interview ya Gabi Kovalenko. Yeye ni mmoja wa spiritual seekers ninaowapenda sana. Ana YouTube channel ambapo huzungumzia mambo ambayo honestly yanaonekana kuwa beyond her age — na ana miaka 23 tu. Wakati mwingine ni kama anachannel messages kutoka higher realms… lakini baadaye nikagundua kuwa sisi sote tuna uwezo huo, isipokuwa roho zetu zimefungwa na conditioning pamoja na programming za dunia.
“Kila mtu anapitia njia yake binafsi, lakini njia ya kurudi nyumbani ni moja kwa wote.” ~ Gabi Kovalenko
So that’s it kwa leo. Wewe unaionaje non-duality? Unaamini ni siri fulani kubwa au ndiyo true nature yetu ya msingi? Umewahi kupitia spiritual awakening? Experience yako ilikuwa vipi?
In love and light ✨