Wenye utimamu msihuzunike wengine wanaposhangilia kifo cha Membe

Usifikiri wote ni mapunguani kama nyie na huyo Makamba wenu aliyeyaongea hayo.
Ninyi enzi hizo mlikua mnashangilia kila kitu, wakati sisi huyo Makamba tulimpinga na tulionya hata kitendo cha viongozi kupenda kumwita na kumpa nafasi ya kuongea Kwenye events.
Kwa hiyo unapo comment jua upumbavu ni wako mwenyewe
Mlitakiwa kufahamu kwa sie wafuasi wa Magu (ambao ndo wengi) baada ya kifo chake tuliumia sana and we had to put up with the biggest of insults kutoka kwenu nyie mliofurahia kuondoka kwake, kwa sasa tumeshakua sugu na hatuna tena cha kupoteza.
Hamkujua ni hatari kiasi gani kupambana na mtu asiekua na cha kupoteza.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu haya mambo hukupaswa kuyaandika leo kama dhamira yako ni kujenga...

Ulipaswa kuandika mapema zaidi

Maana wanaoshangilia leo hawakua na tabia hiyo kabla...

Wamefundishwa...

Hiki ni kisasi baada ya wao kushangiliwa msiba wao...

Tujifunze kutotenda kile tusichopenda kutendewa...

Ukiwa na watoto usifurahi mtoto wa jirani akifa.
Umenena vyema
 
Huenda hamna cha kupoteza lakini mnajipoteza.
Maana ilipofika hata hamjui mkitakacho na pia msijipe wingi ambao wala hata hamnao.
 
Katika hali ya kawaida, hakuna binadamu mwenye akili timamu ambaye hufurahia kifo cha binadamu mwenzake, labda binadamu huyo aliyekufa awe ni mtu ambaye uwepo wake unasababisha vifo vya wanadamu wenzake, yaani awe muuaji, au kama binadamu huyo uwepo wake huwafanya binadamu wenzake wasiwe na amani, waishi kwa hofu, yaani awe ni hatari kwa amani na ustawi wa binadamu wenzake.

Sasa wamezuka watu, ambao naamini ni punguani, wanasema eti wanafurahia kifo cha Bernard Membe (Mungu amrehemu mja wake). Jambo linaloleta faraja kubwa, hao watu punguani, hakuna hata mmoja aliyesema kuwa anafurahia kifo cha Bernard Membe kwa sababu alikuwa ni mtu mbaya. Hakuna aliyesema kuwa Membe alikuwa muuaji au alikuwa hatari kwa ustawi wa jamii ya Watanzania au alisababisha watu kukosa amani, au kuishi kwa hofu, au alikuwa chukizo kwa mtu yeyote yule. Mtu akikuchukia ukiwa huna kosa wala uovu wowote, hustahili kuhuzunika, utambue tu kuwa mtu huyo ni mgonjwa wa akili, na wagonjwa hawa wa akili tuwahurumie na tuwakubali kuwa ni sehemu ya jamii yetu. Wapo watu wengi ambao wapo kwenye mstari unaotenganisha walip wazima na wagonjwa wa akili. Hawa hawaokoti makopo, ila utawajua ni wagonjwa wa akili kwa kauli na wakati fulani kwa matendo yao yanayokosa ustaarabu na hekima.

Watu hawa sababu pekee wanayoitoa ni kuwa wanafurahia Membe kufariki kwa sababu Mzee Makamba alisema wema hawafi, sasa wanashangaa kwa nini mtu mwema amekufa. Maana yake ni kwamba wanakubali kuwa Membe alikuwa mtu mwema.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akikuambia jambo la kijinga na wewe ukalikubali, anakudharau, anakuona na wewe ni mjinga. Kauli ile ya Mzee Makamba kuwa watu wema hawafi, kama alimaanisha kufa kwa mwili, basi ilikiwa kauli ya kijinga, na wale walioikubali na sasa kuifanya kuwa ni reference, hakika watakuwa wajinga na punguani. Ilikuwa kauli ya kijinga ndiyo maana hata Rais Samia aliikataa palepale.

Sote tunajua wapo watu wengi waliyofanya mambo mengi makubwa ya kutukuka Ulimwenguni, hawapo Duniani, wakati majambazi yapo hai, na mengine yapo gerezani. Ukifanya reference kwenye kauli ya kijinga, unaonekana ni punguani wa akili.

Tunamwomba Mungu wa rehema uipumzishe mahali pema peponi Roho ya ndugu yetu Bernard Membe uliyemwita kwako kwa kadiri ya mpango wako kwa maisha yake.

Poleni sana wafiwa. Basi tafakarini maneno haya, na yawape amani ya Bwana.

1 The 4:13-18 SUV

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
Aya ya kwanza tu inajieleza wewe upo upande upi.
Jamaa zako waliposema
1. Mungu kaamulia ugonvi na
2. Wazuri hawafi,
Ulikua na yapi ya kusema juu ya kauli hizo?
Ukweli ni kwamba tunapotafuta maridhiano ya kitaifa isiishie kwa wanasiasa pekee bali inapaswa kushuka chini mpaka kwa wananchi wa kawaida tuungane tuwe kitu kimoja.
Viongozi wanapaswa kuchunga sana kauli zao
 
Mkuu haya mambo hukupaswa kuyaandika leo kama dhamira yako ni kujenga...

Ulipaswa kuandika mapema zaidi

Maana wanaoshangilia leo hawakua na tabia hiyo kabla...

Wamefundishwa...

Hiki ni kisasi baada ya wao kushangiliwa msiba wao...

Tujifunze kutotenda kile tusichopenda kutendewa...

Ukiwa na watoto usifurahi mtoto wa jirani akifa.
Mimi ni mfano hai, nilikua naumizwa na kifo cha kiongozi ama mtu yeyote ninaemfaham.
Ila kwa alivyosemwa JPM, moyo ushakua mgumu, siwezi tu kuandika kama Lwiva ila comments za namna hiyo nazi like bila shida kabisa.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Jamani toeni order mapema, mashimo yachimbwe mangapi, vijana huko Rondo wanaendelea na uchimbaji wa handaki za kufukia mtu wenu.

Ko km na nyie mnaungana nae kufukiwa wote semeni mapemaa, hatutaki usumbufu hapo baadae baada ya j4 kupita.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kumbe na wao wanasikia maumivu ya kufiwa.Kwa page ya Nape kule Instagram utacheka hizo dhihaka anazopewa,bora hata asingepost.
 
Point unashangilia kifo cha membe kwa baya lipi alilofanya
Jiwe alitesa wapinzan wake na kuwaua kwa victim walikua na haki ya kushangilia kifo chake
Usiwapangie watu vya kushangilia, wewe ndo nani upange vya kushangilia, yaani wewe ndio chief shangilia controller? Kengelesi 1-1
 
Wewe ni pro Membe kwa hiyo hautusumbui.

Kwanza umeita watu wanaofurahia vifo vya wenzao ni punguani. Kwa hiyo hata huyo Membe umemuweka kwenye kundi la hao punguani wakiwemo wazee wako wengine kwenye ule umoja mtakatifu wa watu wema.

Umesema mtu timamu huwezi shangilia kifo lakini bado unameaminisha kuwa unaweza kufurahia kwa kutoa sababu ambazo mnajaribu kujiaminisha kwenye kundi lenu. Eti muuaji, mara anayekosesha wengine amani. Kama mwizi na mpiga dili kwa nini usikoseshwe amani.?

Wacha watu wafurahie kifo kama ambavyo Membe pia alifurahia kifo. Na bado tunaamini hizi furaha zitaendelea.
Hivi kumbe kuna mashetani zaidi ya Pombe Magufuli!
 
Katika hali ya kawaida, hakuna binadamu mwenye akili timamu ambaye hufurahia kifo cha binadamu mwenzake, labda binadamu huyo aliyekufa awe ni mtu ambaye uwepo wake unasababisha vifo vya wanadamu wenzake, yaani awe muuaji, au kama binadamu huyo uwepo wake huwafanya binadamu wenzake wasiwe na amani, waishi kwa hofu, yaani awe ni hatari kwa amani na ustawi wa binadamu wenzake.

Sasa wamezuka watu, ambao naamini ni punguani, wanasema eti wanafurahia kifo cha Bernard Membe (Mungu amrehemu mja wake). Jambo linaloleta faraja kubwa, hao watu punguani, hakuna hata mmoja aliyesema kuwa anafurahia kifo cha Bernard Membe kwa sababu alikuwa ni mtu mbaya. Hakuna aliyesema kuwa Membe alikuwa muuaji au alikuwa hatari kwa ustawi wa jamii ya Watanzania au alisababisha watu kukosa amani, au kuishi kwa hofu, au alikuwa chukizo kwa mtu yeyote yule. Mtu akikuchukia ukiwa huna kosa wala uovu wowote, hustahili kuhuzunika, utambue tu kuwa mtu huyo ni mgonjwa wa akili, na wagonjwa hawa wa akili tuwahurumie na tuwakubali kuwa ni sehemu ya jamii yetu. Wapo watu wengi ambao wapo kwenye mstari unaotenganisha walip wazima na wagonjwa wa akili. Hawa hawaokoti makopo, ila utawajua ni wagonjwa wa akili kwa kauli na wakati fulani kwa matendo yao yanayokosa ustaarabu na hekima.

Watu hawa sababu pekee wanayoitoa ni kuwa wanafurahia Membe kufariki kwa sababu Mzee Makamba alisema wema hawafi, sasa wanashangaa kwa nini mtu mwema amekufa. Maana yake ni kwamba wanakubali kuwa Membe alikuwa mtu mwema.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akikuambia jambo la kijinga na wewe ukalikubali, anakudharau, anakuona na wewe ni mjinga. Kauli ile ya Mzee Makamba kuwa watu wema hawafi, kama alimaanisha kufa kwa mwili, basi ilikiwa kauli ya kijinga, na wale walioikubali na sasa kuifanya kuwa ni reference, hakika watakuwa wajinga na punguani. Ilikuwa kauli ya kijinga ndiyo maana hata Rais Samia aliikataa palepale.

Sote tunajua wapo watu wengi waliyofanya mambo mengi makubwa ya kutukuka Ulimwenguni, hawapo Duniani, wakati majambazi yapo hai, na mengine yapo gerezani. Ukifanya reference kwenye kauli ya kijinga, unaonekana ni punguani wa akili.

Tunamwomba Mungu wa rehema uipumzishe mahali pema peponi Roho ya ndugu yetu Bernard Membe uliyemwita kwako kwa kadiri ya mpango wako kwa maisha yake.

Poleni sana wafiwa. Basi tafakarini maneno haya, na yawape amani ya Bwana.

1 The 4:13-18 SUV

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
Umeongea maneno mengi sana na yenye busara ndani yake lakini naona tatizo moja kwenye hili bandiko lako.Unajarabu kuwabeza 'wanaofurahia' kifo cha Membe lakini wakati huo huo ukijenga mazingira ya kukubaliana na waliofurahia kifo cha JPM kwa kutumia sababu kama hapa nakuquote " watu hufurahia kifo cha mtu aliyekuwa anakosesha amani katika jamii.........".

Kama umeamua kukemea hii tabia unapaswa ukemee tu bila kuegemea upande wowote.Tukubali kama Taifa tulikosea sana kuruhusu kejeli zile kipindi cha msiba wa JPM na kinachotokea leo ni mwendelezo wa zile kejeli,tofauti ni kwamba safari hii imegeukia upande wa pili. Tujisahihishe wote
 
Sema nyie watu ni wanafiki Sana , uzuri Mwenyezi Mungu ni neutral , imagine bila mshipa wa aibu unaandika na Mafungu ya Biblia ili kuhadaa watu , uzuri humu JF ID zote zilizokejeli kifo cha JPM tunazijua , au tufukue reply zako humu boss .....
Sisi tunamsoma na kumshangaa sana,sijui anatuchukulia kuwa hatuna kumbukumbu na comments zake.Pana members humu ambao wapo neutral na walikemea hili la kejeli za misiba tangu msiba wa JPM,hao wakisema na leo nitawaelewa.Bahati mbaya sana mtoa mada si mmoja wapo.
 
Back
Top Bottom