Wenye utimamu msihuzunike wengine wanaposhangilia kifo cha Membe

Wenye utimamu msihuzunike wengine wanaposhangilia kifo cha Membe

Mkuu haya mambo hukupaswa kuyaandika leo kama dhamira yako ni kujenga...

Ulipaswa kuandika mapema zaidi

Maana wanaoshangilia leo hawakua na tabia hiyo kabla...

Wamefundishwa...

Hiki ni kisasi baada ya wao kushangiliwa msiba wao...

Tujifunze kutotenda kile tusichopenda kutendewa...

Ukiwa na watoto usifurahi mtoto wa jirani akifa.
Umemaliza kila kitu Mkuu
 
Kazikwe naye kama unampenda, bahari imetulia, 1-1
Acha kujifariji ,sijawahi kuwa mfuasi wa Membe hata siku moja ,nyinyi ndiyo mnampenda sana mzee wenu wa legasi mpaka zitto akawaambia mkazikwe naye.
 
Ubaya Ni kwamba wema wameshangilia kifo Cha JPM tu, na hawana nafasi nyingine!
Ila wabaya wamepata nafasi moja kwa Membe, na wanasubiria nafasi zingine, kwa JK, MAKAMBA, NAPE, JANUARY, na SSH!
Kwa Sasa, goli ni 1-1, Ila mwisho wa siku wabaya wataondoka na ushindi mnono wa magoli 6-1
Tuendelee kusubiri,

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ubaya Ni kwamba wema wameshangilia kifo Cha JPM tu, na hawana nafasi nyingine!
Ila wabaya wamepata nafasi moja kwa Membe, na wanasubiria nafasi zingine, kwa JK, MAKAMBA, NAPE, JANUARY, na SSH!
Kwa Sasa, goli ni 1-1, Ila mwisho wa siku wabaya wataondoka na ushindi mnono wa magoli 6-1
Tuendelee kusubiri,

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hii hesabu ya 6-1 nilikuwa sijaitilia maanani aisee.Watu mnajua kufafanua
 
UKIACHANA NA WANASIASA NI WATU WA AINA GANI WALIFURAHIA KIFO CHA JPM?

Usemi kuwa wenye shida ya kodi na vyeti feki ndio walioshangilia kifo cha JPM upo sahihi ila usahihi wake una mipaka.

JPM alipofariki kuna mzee mmoja nilikuwa nazungumza nae na akasema walichinja ng'ombe na kufurahia ila baada ya miezi kadhaa aligundua hawakufanya jambo sahihi kwani walifumbwa macho na furaha sababu ya yaliyowatokea wakati JPM yupo madarakani.

YALIYOWATOKEA NI YAPI?

Tax force iliyokagua mahesabu ya nyuma ilifanya lile zoezi kisheria bila kuzingatia mazingira na hali halisi ya mfanyabiashara na matokeo yake mfanyabiashara aliumia.

Walichofanya tax force kwenye makaratasi kisheria walikuwa sahihi(Sheria inawataka wafanye ukaguzi wa hesabu) ila mfumo waliotumia kiubinadamu hawakuwa sahihi.

Hawakuwa sahihi kwa sababu kwanini wachukue hesabu za miaka 5 nyuma ambazo mfanyabiashara alizipeleka kwa wakati halafu wao hawakuzifanyia kazi kwa wakati ila leo unaweka riba kubwa ya kiasi cha kodi unachosema kimecheleweshwa wakati hukufanya ukaguzi kwa wakati? Hiyo riba isingekuwepo kama ukaguzi wa 2014 ungeufanya mapema. Unafanya ukaguzi 2018 halafu unacharge riba kwa mwezi kwa miaka 4. Huu haukuwa ubinadamu japo sheria inaruhusu kuweka riba katika kodi iliyocheleweshwa.

Kiasi cha kodi ulichokiwekea riba nacho kina walakini kutokana na mazingira halisi ya hesabu za makaratasi za mfanyabiashara. Mfano, kusema kwamba fedha zinazoingia bank ni mauzo na kama sio mauzo leta uthibitisho. Imagine miaka 5 nyuma akaunt ya bank ya mfanyabiashara imeingiza kiasi gani? Chote hicho uweke assumption kuwa ni mauzo na uyape sifa ya kulipiwa kodi bila kujali kuwa wakati mwingine mfanya biashara anaweka fedha ile ile na kuitoa bank ili kukuza mzunguko akopesheke, mfanya biashara anapika hesabu ili akopesheke, hesabu ambazo ndipo ulipotoa kodi na kuiwekea riba.

Kwa ufupi walichukua hesabu za miaka 5 nyuma wakafanya yafuatayo:

1.Kuchukua utofauti wa manunuzi yaliyopo VAT na kwenye hesabu na kuyapiga 30% tax na riba.

2. Kuchukua tofauti mauzo ya mauzo ya mashine na hesabu na kuyapiga either 30% au 18% na riba na faini ya matumizi mabaya ya mashine.

3. Wakati mwingine kuchukua fedha zilizoingia bank na kuzilinganisha na mauzo ya hesabu na mashine kisha ile tofauti kuipiga 48% na kusema ni mauzo ambayo hukutoa risiti hivyo tunataka VAT yetu na kodi ya mapato na kisha kuwekea riba kwa muda uliokaa bila kulipa na faini ya matumizi mabaya ya mashine.

Hapa palizaliwa kodi kubwa sana ambayo mfanyabiashara alitakiwa kuilipa kwa mpango maalum ikiwemo Kukamata fedha zilizo bank bila kujali ni za wateja, za mkopo au za kikundi.

Nakumbuka kuna kijana alisema alichanganyikiwa kwani wateja walimtumia fedha, zile fedha zikazuiwa zote na ukawa mwanzo wa kutoaminika tena na kuyumba.

Kuna ambaye alikuwa na mkopo bank na dhamana ni nyumba, pesa iliyopo kwenye akaunti ya biashara ni mkopo na ndiyo inapeleka marejesho. Huyu naye yakamkuta.

Tax force hawakuwasikiliza hawa, hawakutaka kujua ni nn wanapitia, wao walifanya kazi yao kisheria na masuala ya ubinadamu wakaweka kando. Wapo walioanza upya huku tin zikisoma madeni makubwa ya kodi na wengine hawakusimama tena.

Hapo katikati wakaingia vyeti feki, Hawa nao Raisi alikuwa sahihi kisheria ila kiubinadamu kama Lowasa alivyosema alitakiwa kutazama mazingira ya hawa watu kuwepo serikalini na vyeti feki angalau awatazame, Nasikia ulikuwa ni mpango wa JPM katika awamu yake ya 2 afanye hichi alichokifanya Samia kuwapa 5% ya michango yao(Sina uthibitisho)

Ukiachana na wale walionunua majina wakiwa vijana wadogo na kwenda kusoma kihalali na kumaliza kwa jina lisilo lake, Kuna wazee wengi waliajiriwa drs 7 kisha serikali ya JK ikataka wajiendeleze, sasa mzee wa miaka 45 kusoma na kufaulu ni tabu kidogo, wengi wakaingia kwenye mtego wa kununua majina, kufoji n.k. Hapa nailaumu serikali ya JK kwa kuwalea hawa, Serikali yake ilipaswa kuwa makini kuwakagua wanaporudi baada ya kuwataka wajiendeleze.

Wengi walibakisha miaka 5, 10 mpaka 15 kustaafu kipindi cha JK, kwanini uwaambie wakatafute vyeti vya form 4 na walipoleta mshahara ikaongezwa kwa kazi ile ile waliokuwa wakiifanya kwa vyeti vya drs la 7.

Hapa serikali ya JK haikufanya sawa ingewaruhusu wastaafu kwa malipo sahihi kisheria au ingewapa muda waondoke ndani ya muda sahihi badala ya kuwakubali na kuwakumbatia.

JPM aliporekebisha akarekebisha kwa kutumia fimbo kali mno huku akiwaacha sekta zingine kama jeshi. Hapa pakazaliwa huzuni, huzuni ikazaa chuki, wakakutana mtaani na wahanga wa Tax force wote wakawa kitu kimoja. MALALAMIKO FC

Walipokuwa wanalalamika wakaibuka Chawa wa JPM na kuwakejeli na kuwahadaa na kuwacheka kuwa wao ni vyeti feki na wezi wa kodi, Chuki ikazidi kumwagiliwa na kujazwa mbolea na yenyewe bila hiana ikastawi.

Wanasiasa wapinzani wa JPM wakapita na upepo huo, JPM akavikwa picha ya katili asiyejali, pakawa na matukio ya vifo matukio ambayo hata awamu zilizopita yalitokea lakini awamu hii kuna kundi la watu wenye malalamiko ambao wanakejeliwa na Chawa wa JPM hivyo wamebaki na option moja tu kuukubali ubaya wowote watakaousikia kumhusu JPM uwe sahihi au usiwe sahihi.

Nchi ikampoteza JPM kukiwa na kundi likiwa na taswira hasi juu yake, lile kundi likasahahu kuwa JPM hakuwa mbaya kwa kiwango cha kuchinja ng'ombe, mbuzi, kugonga chiaz na kufurahia kifo chake.

Wakasahau kuwa kuna mazuri mengi ameifanyia nchi na kuna kundi kubwa pia linalomheshimu kama kiongozi mwenye uthubutu. Wakashangilia wazi wazi kifo chake. Wakaionyesha furaha yao wazi wazi.

Wapendwa wa JPM wakasikitika, Chawa wa JPM wakalia na katika huzuni zao wakakejeliwa kuwa wakazikwe naye, MUNGU kaamua ugomvi n.k Tukagawanyika tukawa na makundi mawili ndani ya nchi moja.
 
Ubaya Ni kwamba wema wameshangilia kifo Cha JPM tu, na hawana nafasi nyingine!
Ila wabaya wamepata nafasi moja kwa Membe, na wanasubiria nafasi zingine, kwa JK, MAKAMBA, NAPE, JANUARY, na SSH!
Kwa Sasa, goli ni 1-1, Ila mwisho wa siku wabaya wataondoka na ushindi mnono wa magoli 6-1
Tuendelee kusubiri,

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Umeiweka vizuri sana, umesahau kumuongeza aliesema tukazikwe pembeni ya JPM. Siwezi hata kuandika jina lake maku yule

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Katika hali ya kawaida, hakuna binadamu mwenye akili timamu ambaye hufurahia kifo cha binadamu mwenzake, labda binadamu huyo aliyekufa awe ni mtu ambaye uwepo wake unasababisha vifo vya wanadamu wenzake, yaani awe muuaji, au kama binadamu huyo uwepo wake huwafanya binadamu wenzake wasiwe na amani, waishi kwa hofu, yaani awe ni hatari kwa amani na ustawi wa binadamu wenzake.

Sasa wamezuka watu, ambao naamini ni punguani, wanasema eti wanafurahia kifo cha Bernard Membe (Mungu amrehemu mja wake). Jambo linaloleta faraja kubwa, hao watu punguani, hakuna hata mmoja aliyesema kuwa anafurahia kifo cha Bernard Membe kwa sababu alikuwa ni mtu mbaya. Hakuna aliyesema kuwa Membe alikuwa muuaji au alikuwa hatari kwa ustawi wa jamii ya Watanzania au alisababisha watu kukosa amani, au kuishi kwa hofu, au alikuwa chukizo kwa mtu yeyote yule. Mtu akikuchukia ukiwa huna kosa wala uovu wowote, hustahili kuhuzunika, utambue tu kuwa mtu huyo ni mgonjwa wa akili, na wagonjwa hawa wa akili tuwahurumie na tuwakubali kuwa ni sehemu ya jamii yetu. Wapo watu wengi ambao wapo kwenye mstari unaotenganisha walip wazima na wagonjwa wa akili. Hawa hawaokoti makopo, ila utawajua ni wagonjwa wa akili kwa kauli na wakati fulani kwa matendo yao yanayokosa ustaarabu na hekima.

Watu hawa sababu pekee wanayoitoa ni kuwa wanafurahia Membe kufariki kwa sababu Mzee Makamba alisema wema hawafi, sasa wanashangaa kwa nini mtu mwema amekufa. Maana yake ni kwamba wanakubali kuwa Membe alikuwa mtu mwema.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akikuambia jambo la kijinga na wewe ukalikubali, anakudharau, anakuona na wewe ni mjinga. Kauli ile ya Mzee Makamba kuwa watu wema hawafi, kama alimaanisha kufa kwa mwili, basi ilikiwa kauli ya kijinga, na wale walioikubali na sasa kuifanya kuwa ni reference, hakika watakuwa wajinga na punguani. Ilikuwa kauli ya kijinga ndiyo maana hata Rais Samia aliikataa palepale.

Sote tunajua wapo watu wengi waliyofanya mambo mengi makubwa ya kutukuka Ulimwenguni, hawapo Duniani, wakati majambazi yapo hai, na mengine yapo gerezani. Ukifanya reference kwenye kauli ya kijinga, unaonekana ni punguani wa akili.


Tunamwomba Mungu wa rehema uipumzishe mahali pema peponi Roho ya ndugu yetu Bernard Membe uliyemwita kwako kwa kadiri ya mpango wako kwa maisha yake.

Poleni sana wafiwa. Basi tafakarini maneno haya, na yawape amani ya Bwana.

1 The 4:13-18 SUV

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
Acha tuitwe vichaa ila haki yetu kufurahi kama nanyi wenye akili timamu mlivyo furahia
Sisi tunasema kachukueni mzoga wa kenge pale mochwari unaanza kuoza pelekeni rundo huko
 
Wakati tukiendelea kushangilia vifo vya tunaodhani ni wabaya wetu, Mungu anasema hafurahishwi na kifo cha mtu muovu, bali arejelee toba na kusamehewa dhambi zake. Japo hata mimi nilifurahishwa na kifo cha muovu mmoja, ila Mungu anasema hapendi.

Basi, ndugu zangu, tuishie hapa, kwa maana matokeo ni 1-1.
Kuna kenge kama wanne wamebaki wanakula sana vfaranga
 
Acheni kuuma uma maneno muasisi wa siasa za chuki ndani ya nchi hii anajulikana.
Hivi kabla ya kufikiria haya yote kwann hamjiulizi kuwa hizi siasa za chuki mbona hazikuwepo kipindi chote mpaka zije kuonekana baada ya Jiwe kuingia Madarakani?

Kiufupi Magufuri ndo muasisi wa hizi siasa za chuki na amewaambukiza mpaka wafuasi wake na ndo hao hao wanao endeleza kazi ya jiwe kusambaza chuki ila kwa sasa hizo chuki zao hazina madhara kwa sababu hawana nguvu yeyote wamebaki kubweka na kutukana hovyo hovyo kwenye mitandao ya kijamii.

Kiufupi wafuasi jiwe wamesha athirika kisakolojia baada ya kupoteza Madaraka kwa ghafla na katika hali ya kushangaza hali takuwa walidhani wangebaki na hayo Madaraka milele ,na ndio maana wako tiyari kufanya chochote ili mradi wapate furaha bila kujali hicho kitu ni kitu cha aina gani.
Kachukue mzoga wa kenge wako unaanza kuharibika[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kumbe hujanielewa kabisa.

Mimi nipo ninaandika hapa si kwa sababu ya wema wangu, ujanja wangu au ujasiri wangu, bali ni kwa rehema za Mwenyezi Mungu ambaye huwanyeshea mvua watu, huwapa hewa watu wote, wema na wabaya.

Hakuna aliye mtakatifu ila wapo wanaopenda kuwa watakatifu, hao ndio wakeshao kuitafuta hekima ya Mungu.
Kumbuka furaha yetu ni kuwa mbaya kaondoka maana wazuri wamebaki hujaelewa nn sasa
 
Ukitaka kuona mihemko ya watu soma michango ya huu Uzi,hisia zimetawala zaidi na mwisho wamepoteza maana halisi ya Uzi.

Kifo ni hatua ya mwisho katika maisha ya mwanadam hivyo sote tu wapitaji tu katika dunia hii wale walio wekeza matumaini makubwa kwa binadamu wenzao katika maisha pale kifo kinapo tokea hubaki na masikitiko ndani ya mioyo yao hivyo hubaki kutafuta faraja tu hata kwa vitu visivyo na msingi.
We wasema ila kenge asie mwema au mzuri kaondoshwa cc full shangwe
 
Back
Top Bottom