Wenye utimamu msihuzunike wengine wanaposhangilia kifo cha Membe

Katika hali ya kawaida, hakuna binadamu mwenye akili timamu ambaye hufurahia kifo cha binadamu mwenzake, labda binadamu huyo aliyekufa awe ni mtu ambaye uwepo wake unasababisha vifo vya wanadamu wenzake, yaani awe muuaji, au kama binadamu huyo uwepo wake huwafanya binadamu wenzake wasiwe na amani, waishi kwa hofu, yaani awe ni hatari kwa amani na ustawi wa binadamu wenzake.

Sasa wamezuka watu, ambao naamini ni punguani, wanasema eti wanafurahia kifo cha Bernard Membe (Mungu amrehemu mja wake). Jambo linaloleta faraja kubwa, hao watu punguani, hakuna hata mmoja aliyesema kuwa anafurahia kifo cha Bernard Membe kwa sababu alikuwa ni mtu mbaya. Hakuna aliyesema kuwa Membe alikuwa muuaji au alikuwa hatari kwa ustawi wa jamii ya Watanzania au alisababisha watu kukosa amani, au kuishi kwa hofu, au alikuwa chukizo kwa mtu yeyote yule. Mtu akikuchukia ukiwa huna kosa wala uovu wowote, hustahili kuhuzunika, utambue tu kuwa mtu huyo ni mgonjwa wa akili, na wagonjwa hawa wa akili tuwahurumie na tuwakubali kuwa ni sehemu ya jamii yetu. Wapo watu wengi ambao wapo kwenye mstari unaotenganisha walip wazima na wagonjwa wa akili. Hawa hawaokoti makopo, ila utawajua ni wagonjwa wa akili kwa kauli na wakati fulani kwa matendo yao yanayokosa ustaarabu na hekima.

Watu hawa sababu pekee wanayoitoa ni kuwa wanafurahia Membe kufariki kwa sababu Mzee Makamba alisema wema hawafi, sasa wanashangaa kwa nini mtu mwema amekufa. Maana yake ni kwamba wanakubali kuwa Membe alikuwa mtu mwema.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akikuambia jambo la kijinga na wewe ukalikubali, anakudharau, anakuona na wewe ni mjinga. Kauli ile ya Mzee Makamba kuwa watu wema hawafi, kama alimaanisha kufa kwa mwili, basi ilikiwa kauli ya kijinga, na wale walioikubali na sasa kuifanya kuwa ni reference, hakika watakuwa wajinga na punguani. Ilikuwa kauli ya kijinga ndiyo maana hata Rais Samia aliikataa palepale.

Sote tunajua wapo watu wengi waliyofanya mambo mengi makubwa ya kutukuka Ulimwenguni, hawapo Duniani, wakati majambazi yapo hai, na mengine yapo gerezani. Ukifanya reference kwenye kauli ya kijinga, unaonekana ni punguani wa akili.

Tunamwomba Mungu wa rehema uipumzishe mahali pema peponi Roho ya ndugu yetu Bernard Membe uliyemwita kwako kwa kadiri ya mpango wako kwa maisha yake.

Poleni sana wafiwa. Basi tafakarini maneno haya, na yawape amani ya Bwana.

1 The 4:13-18 SUV

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
Kwahiyo nyie kushangilia kifo cha Magufuli ni halali lakini kushangilia vifo vya wengine ni haramu?. Yaani nyie ndondocha sijui mnatumiaga akili gani tu?.
IMG_20230327_072032.jpg
 
WATU WAZURI HAWAFI - mzee makamba.
 
1"Wazuri hawafi"-YUSUF MAKAMBA.

2"MUNGU ameamua ugomvi Bahari imetulia"-NAPE NNAUYE.

3"Wanaompenda Magufuli wakazikwe nae Chato"-ZITO KABWE

4"Mkiona Tanzania nipagumu kukaa hamieni BURUNDI"-MWIGULU NCHEMBA.

5"Magufuli hatasimama tena[emoji38][emoji1787]-BERNALD MEMBE.

Hizi ni kauli zenye maumivu kwa Taifa.
Kauli hizi za washenzi zimeligawa Taifa.
 
Sijawahi kuona andiko la ajabu kama hili uliloandika hapa, unaoenekana kuwashambulia wale wanaofurahia kifo cha Membe, huku ukiwaona wako sawa wale wanaofurahia kifo cha Magufuli.

Ajabu kabisa ni pale ulipoenda mbali ukaokoteza andiko kwenye biblia ili kusapoti hii hoja yako, sijui ni biblia ipi hiyo inayowataka wakristo washangilie kifo cha yeyote, hata kama hakuwa na matendo yakukufurahisha hapa duniani.

The fact is, hujui hata yule Magufuli usiyempenda dakika zake za mwisho alizitumia vipi, inawezekana pia ikawa alisema na Mungu wake, akatubu dhambi zake, leo yupo sehemu salama anakusikitikia wewe unaeendekeza chuki dhidi yake, sijui umepata wapi kiburi cha kujiona mwenye haki zaidi ya mwingine.

Ningekuona wa maana kama ungeachana na hii biashara ya kushangilia vifo kwa ujumla wake, bila kujali kama yule aliyefariki ulimpenda au kumchukia, lakini hiki ulichofanya hapa kwa kuwaita punguani wale wanaoshangilia kifo cha Membe, umeendeleza chuki, ndio maana nao wanakuona ni punguani pia unayeshangilia kifo cha Magufuli.
 
Tena hawa wazee wenye viherehere na kauli zao tata pamoja na vijana wao wakidondoka wafukiwe na sio kuzikwa ktk mashimo na sio makaburi ya futi 24 na sio futi sita...
Ni good riddance!!
R.I.P MY PRESIDENT, JPM.... taifa bado linakumiss pakubwa sana..
 
Sijawahi kuona andiko la ajabu kama hili uliloandika hapa, unaoenekana kuwashambulia wale wanaofurahia kifo cha Membe, huku ukiwaona wako sawa wale wanaofurahia kifo cha Magufuli.

Ajabu kabisa ni pale ulipoenda mbali ukaokoteza andiko kwenye biblia ili kusapoti hii hoja yako, sijui ni biblia ipi hiyo inayowataka wakristo washangilie kifo cha yeyote, hata kama hakuwa na matendo yakukufutahisha hapa duniani.

The fact is, hujui hata yule Magufuli usiyempenda dakika zake za mwisho alizitumia vipi, inawezekana pia ikawa alisema na Mungu wake, akatubu dhambi zake, leo yupo sehemu salama anakusikitikia wewe unaeendekeza chuki dhidi yake.

Ningekuona wa maana kama ungeachana na hii biashara ya kushangilia vifo kwa ujumla wake, bila kujali kama aliyefariki ulimpenda au kumchukia, lakini hiki ulichofanya hapa kwa kuwaita punguani wale wanaoshangilia kifo cha Membe, umeendeleza chuki, ndio maana nao wanakuona ni punguani pia unayeshangilia kifo cha Magufuli.
Andiko la ajabu lkn bado umetiririsha maoni yako. Nani wa ajabu kati yako na Mtoa mada?
 
Usifikiri kila aliyepingana na JPM au CCM au JK alikua ni mshangiliaji.
SlMnaojaribu kutu quote sisi hatuna ushabiki wala ufuasi kwa mtu

Unafiki ndio ishu yangu hapa...
Kama unaona 'wanaoshangilia' sasa hawako sahihi, nionyeshe comment au uzi ambao ulipinga wakati watu wanashangilia humu kifo cha jpm, kama unayo basi wewe uko neutral na nimekuelewa ktk statement yako, kama huna THEN ZIP IT... let people vent their jayness!! What goes around comes around...!
 
Acheni kuuma uma maneno muasisi wa siasa za chuki ndani ya nchi hii anajulikana.
Hivi kabla ya kufikiria haya yote kwann hamjiulizi kuwa hizi siasa za chuki mbona hazikuwepo kipindi chote mpaka zije kuonekana baada ya Jiwe kuingia Madarakani?

Kiufupi Magufuri ndo muasisi wa hizi siasa za chuki na amewaambukiza mpaka wafuasi wake na ndo hao hao wanao endeleza kazi ya jiwe kusambaza chuki ila kwa sasa hizo chuki zao hazina madhara kwa sababu hawana nguvu yeyote wamebaki kubweka na kutukana hovyo hovyo kwenye mitandao ya kijamii.

Kiufupi wafuasi jiwe wamesha athirika kisakolojia baada ya kupoteza Madaraka kwa ghafla na katika hali ya kushangaza hali takuwa walidhani wangebaki na hayo Madaraka milele ,na ndio maana wako tiyari kufanya chochote ili mradi wapate furaha bila kujali hicho kitu ni kitu cha aina gani.
Na ndo point ya maridhiano ikajia
Jiwe alikua anaharibu nchi mtu yeyeyote aliye kinyume chake alikua adui aliwakataza wabunge wa ccm kwenda kwenye shughuli yeyote ile ya mwanachadema

Alishawakataza wabunge wa ccm akiwemo vicky kamata kwenda kumuona lema gerezan na aliwachukia jumla
 
Unafiki ndio ishu yangu hapa...
Kama unaona 'wanaoshangilia' sasa hawako sahihi, nionyeshe comment au uzi ambao ulipinga wakati watu wanashangilia humu kifo cha jpm, kama unayo basi wewe uko neutral na nimekuelewa ktk statement yako, kama huna THEN ZIP IT... let people vent their jayness!! What goes around comes around...!
Point unashangilia kifo cha membe kwa baya lipi alilofanya
Jiwe alitesa wapinzan wake na kuwaua kwa victim walikua na haki ya kushangilia kifo chake
 
We jamaa nguruwe kweli, yaani mimi nipoteze muda wangu kujaribu kukuthibitishia wewe jambo?
Utakua umerukwa na akili wewe si bure
 
Acheni kuuma uma maneno muasisi wa siasa za chuki ndani ya nchi hii anajulikana.
Hivi kabla ya kufikiria haya yote kwann hamjiulizi kuwa hizi siasa za chuki mbona hazikuwepo kipindi chote mpaka zije kuonekana baada ya Jiwe kuingia Madarakani?

Kiufupi Magufuri ndo muasisi wa hizi siasa za chuki na amewaambukiza mpaka wafuasi wake na ndo hao hao wanao endeleza kazi ya jiwe kusambaza chuki ila kwa sasa hizo chuki zao hazina madhara kwa sababu hawana nguvu yeyote wamebaki kubweka na kutukana hovyo hovyo kwenye mitandao ya kijamii.

Kiufupi wafuasi jiwe wamesha athirika kisakolojia baada ya kupoteza Madaraka kwa ghafla na katika hali ya kushangaza hali takuwa walidhani wangebaki na hayo Madaraka milele ,na ndio maana wako tiyari kufanya chochote ili mradi wapate furaha bila kujali hicho kitu ni kitu cha aina gani.
 
Attachments

  • VID-20221209-WA0044.mp4
    1 MB
Point unashangilia kifo cha membe kwa baya lipi alilofanya
Jiwe alitesa wapinzan wake na kuwaua kwa victim walikua na haki ya kushangilia kifo chake
Mataahira hao, sasa hivi wanashangilia hadi ndege ikidondoka, basi likidondoka, wagonjwa wakifa...wanashangilia kika kitu hao.
 
There you are...
umefunguka sasa kama ulishangilia au laa... haiwezekani ulete utopolo huu wa kulishwa na kina lisu utake taifa zima likuamini, wananchi wengi wamekataa huu utopolo, utopolo huu unabaki kwa wale maboya kama wewe waliokuwa wanafaidika na njia za panya ila wakapigwa pini...
Acha watu wafurahie kifo cha membe huku wakisubiri cha shauku cha makamba na timu yake...
Tulia dawa ikuingie tu
 
Mataahira hao, sasa hivi wanashangilia hadi ndege ikidondoka, basi likidondoka, wagonjwa wakifa...wanashangilia kika kitu hao.
Sio matahira ukiwa ni mwiba kwa watu ukifa watashangilia, ukiwa mwema ukifa watahuzunika
Tuishi na watu vizuri ili tuache legacy nzuri
 
Back
Top Bottom