Wenye utimamu msihuzunike wengine wanaposhangilia kifo cha Membe

Wenye utimamu msihuzunike wengine wanaposhangilia kifo cha Membe

Utajua mwenyewe mtoa post
20230513_121524.jpg
 
Mtoa mada mada amesema tusihuzunike kuzungukwa na mapunguani, tufurahi tu. Nami nafurahi tu. Kwa akili ya kawaida tu inaonyesha ni namna gani kuna kundi lina matatizo makubwa na pengine Mungu ameruhusu hili la membe kutokea ili watu wajifunze.

Hivi, kama sio kuchanganyikiwa, JPM, aliyekuwa raisi, unamlinganisha na BKM kweli? Mbona naona huku ni kuchanganyikiwa?

Nimefurahi marafiki wa Membe hata hawajatoka kutengeneza propaganda kuwa ameuawa kama ambavyo tunashuhudia katika vifo vingine.
Sisi mapunguani tunafurahaa sana kuondoka kwa kenge huyu
 
Hakika tumefurah sana hata ukituita mapunguani haiondoi furaha yetu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Na ndo point ya maridhiano ikajia
Jiwe alikua anaharibu nchi mtu yeyeyote aliye kinyume chake alikua adui aliwakataza wabunge wa ccm kwenda kwenye shughuli yeyote ile ya mwanachadema

Alishawakataza wabunge wa ccm akiwemo vicky kamata kwenda kumuona lema gerezan na aliwachukia jumla
Weka ushahidi sehemu alipokataza najua una uchungu wa kufiwa na kenge wako
 
Point unashangilia kifo cha membe kwa baya lipi alilofanya
Jiwe alitesa wapinzan wake na kuwaua kwa victim walikua na haki ya kushangilia kifo chake
Sisi tunashangilia kwa sababu hakuwa mtu mwema watu wazuri hawafi
 
Katika hali ya kawaida, hakuna binadamu mwenye akili timamu ambaye hufurahia kifo cha binadamu mwenzake, labda binadamu huyo aliyekufa awe ni mtu ambaye uwepo wake unasababisha vifo vya wanadamu wenzake, yaani awe muuaji, au kama binadamu huyo uwepo wake huwafanya binadamu wenzake wasiwe na amani, waishi kwa hofu, yaani awe ni hatari kwa amani na ustawi wa binadamu wenzake.

Sasa wamezuka watu, ambao naamini ni punguani, wanasema eti wanafurahia kifo cha Bernard Membe (Mungu amrehemu mja wake). Jambo linaloleta faraja kubwa, hao watu punguani, hakuna hata mmoja aliyesema kuwa anafurahia kifo cha Bernard Membe kwa sababu alikuwa ni mtu mbaya. Hakuna aliyesema kuwa Membe alikuwa muuaji au alikuwa hatari kwa ustawi wa jamii ya Watanzania au alisababisha watu kukosa amani, au kuishi kwa hofu, au alikuwa chukizo kwa mtu yeyote yule. Mtu akikuchukia ukiwa huna kosa wala uovu wowote, hustahili kuhuzunika, utambue tu kuwa mtu huyo ni mgonjwa wa akili, na wagonjwa hawa wa akili tuwahurumie na tuwakubali kuwa ni sehemu ya jamii yetu. Wapo watu wengi ambao wapo kwenye mstari unaotenganisha walip wazima na wagonjwa wa akili. Hawa hawaokoti makopo, ila utawajua ni wagonjwa wa akili kwa kauli na wakati fulani kwa matendo yao yanayokosa ustaarabu na hekima.

Watu hawa sababu pekee wanayoitoa ni kuwa wanafurahia Membe kufariki kwa sababu Mzee Makamba alisema wema hawafi, sasa wanashangaa kwa nini mtu mwema amekufa. Maana yake ni kwamba wanakubali kuwa Membe alikuwa mtu mwema.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akikuambia jambo la kijinga na wewe ukalikubali, anakudharau, anakuona na wewe ni mjinga. Kauli ile ya Mzee Makamba kuwa watu wema hawafi, kama alimaanisha kufa kwa mwili, basi ilikiwa kauli ya kijinga, na wale walioikubali na sasa kuifanya kuwa ni reference, hakika watakuwa wajinga na punguani. Ilikuwa kauli ya kijinga ndiyo maana hata Rais Samia aliikataa palepale.

Sote tunajua wapo watu wengi waliyofanya mambo mengi makubwa ya kutukuka Ulimwenguni, hawapo Duniani, wakati majambazi yapo hai, na mengine yapo gerezani. Ukifanya reference kwenye kauli ya kijinga, unaonekana ni punguani wa akili.


Tunamwomba Mungu wa rehema uipumzishe mahali pema peponi Roho ya ndugu yetu Bernard Membe uliyemwita kwako kwa kadiri ya mpango wako kwa maisha yake.

Poleni sana wafiwa. Basi tafakarini maneno haya, na yawape amani ya Bwana.

1 The 4:13-18 SUV

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
Wewe mnafiki mkubwa sana!
Rule namba one: Hakuna binadamu wa kumhukumu binadamu mwenziwe, wewe ulishamhukumu bwana yule kuwa afadhali ati alikufa leo unakuja na hili. Usimhukumu binadamu mwenzio.

Rule namba 2: Usimlilie sana mwenzio, zile ni dhambi zake, unaweza kujuaje dhambi za mwenzio? Ni zako tu ndiyo unaweza kuzijua jitayarishe Kwa nafsi yako. Alipowaona wale wanawake wakimlilia yesu aliwaambia msinililie mimi lilieni nafsi zenu.

Three: jipende na umpende jirani yako, matatizo yote hutokana na kukosa upendo, kwanza ujipende utampenda mwezio
 
Kumbe hujanielewa kabisa.

Mimi nipo ninaandika hapa si kwa sababu ya wema wangu, ujanja wangu au ujasiri wangu, bali ni kwa rehema za Mwenyezi Mungu ambaye huwanyeshea mvua watu, huwapa hewa watu wote, wema na wabaya.

Hakuna aliye mtakatifu ila wapo wanaopenda kuwa watakatifu, hao ndio wakeshao kuitafuta hekima ya Mungu.
Utampendaje ambaye humjui? Umewahi kumwona Mungu? jirani humpendi at unampenda Mungu ambaye hujawahi hata kumwona, ni hisia na imani tu.
 
MaPunguwani waliochanganyikiwa wanashangilia kifo cha mtu mwema.
 
Na bado hapo hatujafika half time, jiulize ikifika dakika ya 70 na kuendelea tutakuwa na goli ngapi?. Itakuwa vifijo na nderemo
MaPunguwani waliochanganyikiwa wanashangilia kifo cha mtu mwema.
 
Ruge na Seth apo vp mjane wa mbwa Bernad
Hiyo ndo kawaida ya wafuasi wa jiwe kutukana hovyo kama vichaa na ndo urithi wa pekee alio waachia mungu wenu aliye lala chato.

Kwani Ruge na Seth walikuwa wafungwa au walikuwa watuhumiwa ambao badae hawa kukutwa na hatia?
Nyinyi si mnasema akina Membe,Nape,Makamba na JK ndo mafisadi sasa inakuwaje Jiwe hakuwafunga kama kweli alikuwa na nia ya kupambana na ufisadi.
 
Sisi tunamsoma na kumshangaa sana,sijui anatuchukulia kuwa hatuna kumbukumbu na comments zake.Pana members humu ambao wapo neutral na walikemea hili la kejeli za misiba tangu msiba wa JPM,hao wakisema na leo nitawaelewa.Bahati mbaya sana mtoa mada si mmoja wapo.
Leta andiko japo moja tu niliposema nilifurahia kifo cha JPM.

Tena nakumbuka kabisa niliandika kuwa kuna mambo ambayo sikukubaliana kabisa na marehemu, na wala siyo yote. Lakini nilieleza kuwa pamoja na yote, kifo kile kilinisikitisha. Kwa mambo yalivyokuwa yanaenda, ningefurahi asiendelee kuwa Rais, lakini siyo asiendelee kuishi.

Siandiki haya kwaajili ya kumfurahisha yeyote. Usiku ule nilikuwa nimelala, nikapigiwa simu na mtu ambaye hajawahi kunipigia simu usiku. Ndipo akanipa taarifa hiyo. Ilinishtua sana, nikaduwaa kwa muda, kisha sikulala, nikakaa kwa karibia masaa 3 kabla ya kulala tena. Japo kulikuwa na minong'ono kuwa alikiwa anaumwa lakini kichwani mwangu hakukuwa na fikra kuwa alikuwa katika hatari ya kifo.

Na siku ya pili yake nikaambiwa na ndugu yangu kuwa mke wangu aliwaambia baadhi ya watu kuwa kumbe nilikuwa namkritisaizi tu Magufuli mdomoni, moyoni nilikuwa nampenda sana, mbona inaonekana nimehuzunika. Na kwa kweli nilihuzunika, na nakumbuka neno langu la kwanza, nilipopewa taarifa nilisema tu, 'my God!'. Na ufahamu kuwa JPM kabla ya kuwa Rais, niliwahi kuongea naye mara 4 kwa simu. Na kuna mengine, kwa vile hayupo Duniani, siwezi kuyaweka hapa.

Mimi ninachoamini ni kuwa wanadamu tuna uwezo wa kusema tendo hili na lile ni mabaya, lakini hatuwezi kuhukumu. Ndiyo maana huwezi kuona japo mara moja mimi Bams eti nikaandika, oh JPM yupo jehanamu, anaungua moto, JPM ni mzoga. Yesu alisema, njooni kwangu nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo ya dhambi, nitawapumzisha, hata kama muwe na dhambi nyekundu kama damu, nitawatakasa. Sasa mimi mwanadamu nitajuaje nyakati za mwisho za marehemu na Mungu wake, hata nitoe hukumu kuwa JPM yupo jehanamu?

Bado naamini kwa kiongozi kuwaua, kuwateka, kuwatesa au kuwabambikia kesi watu unaowaongoza ni ushetani, lakini kamwe siwezi kushangilia kifo cha mwanadamu yeyote. Nitashangilia kama mtu mwovu akikoma kuwa mwovu iwe kwa hiari au kulazimishwa. Lakini pia nimewahi kuandika hapa kuwa mimi naamini kuna baadhi ya mambo mabaya yalifanyanyika bila ya kuwa na maelekezo ya moja kwa moja toka kwa marehemu. Baadhi ya wasaidizi wake, naamini walifanya baadhi ya mambo ya hovyo sana kwa nia ya kumfurahisha. Kosa lake ni kutowakemea. Niliwahi kueleza kuwa mathalani hela yangu, ilikuwa kidogo tu, hela ya mshahara wangu toka UK wakati nafanya kazi nje ya nchi TRA wakaifungia, lakini baada ya kupambana nao kwa siku 2, wakaifungulia. Sikulipa chochote, sikumhonga mtu. Sasa niamini kuwa ile pesa aliifungia Magufuli? Kama angeifungia Magufuli au angekuwa ameelekeza pesa yangu ifungiwe, kuna mtu TRA angeweza kuiachia?

Mimi siyo mnafiki, hakika ningefurahi utawala wa Magufuli kukoma, lakini siyo kukoma kwa kifo. Mimi kama mtu binafsi, sikuwahi kuguswa na chochote kibaya ambacho kilifanywa dhidi yangu kama mtu binafsi, hakuna kabisa lakini unahuzunika na wenzako ambao wanaumia kwa kuonewa. Nina uhakika walioguswa moja kwa moja kwa mabaya na utawala wa JPM, hawawezi kufika hata 10%, lakini hata wangekuwa 5% ni binadamu wenzetu, wanapoonewa au kutotendewa haki ni lazima tupaze sauti zetu.

Lakini pia kuna watu wanajifanya walimpenda sana JPM lakini ukweli ni wanafiki wakubwa, ndio wanaomfanya marehemu kutukanwa na kusemwa vibaya wakati wote kwa maana hawatulii kila siku ni kuanzisha mada za kumkejeli Samia, Mbowe, CAG Asad, Zito, Kikwete; na kuwasema kuwa si chochote wakilinganishwa na JPM. Hawa watu wanaosemwa vibaya nao wana wafuasi wao na wana wanaowaunga mkono na kuwakubali kwa yale wayatendayo, unadhani watakaa kimya? Nao watakutukania yule wanayeamini wewe ulimpenda. Hao hawana tofauti na mzee Makamba ambaye aliropoka, na sasa kauli yake inawafanya baadhi ya watu wamtukanie watu wanaoamini Makamba anawapenda.

Ukweli unabakia pale pale, utawala wa marehemu kuna mambo mabaya kabisa uliyatenda na kuna mazuri pia. Niliwahi kutamka, kwangu mimi, utawala wa marehemu, ungeacha kujihusisha na mambo ya kuua, kuteka na kupoteza watu, mengine yote ni madogo. Uhai wa binadamu mwenzako una thamani kama wa kwako. Uhai wangu una thamani sawa na wa JPM, Membe, Sanane, Azory na mwingine awaye yeyote. Kama sifurahii uhai wangu uondoke kwa nini nikafurahie wa JPM, Membe au Lisu kuondoka? Kama hakuna awezaye kumwongezea mwanadamu mwenzake hata siku moja ya kuishi, basi tuogope kabisa kumwondolea mtu mwingine siku za kuishi.

Wanaofurahia na kushangilia vifo vya wanajisumbua bure maana hao watu wamelala. Tafakari ya maisha yao ni jambo jema. Mema yaendelezwe, mabaya wazikwe nayo.
 
Kumbuka furaha yetu ni kuwa mbaya kaondoka maana wazuri wamebaki hujaelewa nn sasa
Kwa hiyo wewe na mimi ni wema sana kuliko hao waliolala? Mimi uniondoe katika hiyo kufuru. Kama wewe ni mwema basi uangalie usianguke.
 
Wewe mnafiki mkubwa sana!
Rule namba one: Hakuna binadamu wa kumhukumu binadamu mwenziwe, wewe ulishamhukumu bwana yule kuwa afadhali ati alikufa leo unakuja na hili. Usimhukumu binadamu mwenzio.

Rule namba 2: Usimlilie sana mwenzio, zile ni dhambi zake, unaweza kujuaje dhambi za mwenzio? Ni zako tu ndiyo unaweza kuzijua jitayarishe Kwa nafsi yako. Alipowaona wale wanawake wakimlilia yesu aliwaambia msinililie mimi lilieni nafsi zenu.

Three: jipende na umpende jirani yako, matatizo yote hutokana na kukosa upendo, kwanza ujipende utampenda mwezio
Kama hakuna binadamu wa kumhukumu mwenzake
Mahakama na mahikimu wanafanya nin kule mahakamani
 
Back
Top Bottom