Wenye utimamu msihuzunike wengine wanaposhangilia kifo cha Membe

Wenye utimamu msihuzunike wengine wanaposhangilia kifo cha Membe

Wewe ni pro Membe kwa hiyo hautusumbui.

Kwanza umeita watu wanaofurahia vifo vya wenzao ni punguani. Kwa hiyo hata huyo Membe umemuweka kwenye kundi la hao punguani wakiwemo wazee wako wengine kwenye ule umoja mtakatifu wa watu wema.

Umesema mtu timamu huwezi shangilia kifo lakini bado unameaminisha kuwa unaweza kufurahia kwa kutoa sababu ambazo mnajaribu kujiaminisha kwenye kundi lenu. Eti muuaji, mara anayekosesha wengine amani. Kama mwizi na mpiga dili kwa nini usikoseshwe amani.?

Wacha watu wafurahie kifo kama ambavyo Membe pia alifurahia kifo. Na bado tunaamini hizi furaha zitaendelea.
Alie ua kwa upanga atakufa kwa upanga yeye kama alishangilia kifo cha mwenzake kwa nini na sisi tusishangilie cha kwake,?
 
Hahahah huyo mzee akidondoka ningali nipo hai watu watakunywa bia nyingi sana na nyama choma.
Sikutegemea kama ungetoa comment kama hii
Nikuulize swali who is yusuphu makamba kwenye hii nchi ni mazuri yapi au mabaya yapi kwa aliyoyafanya
kwa watanzania walio wengi makamba is nobody
 
Hakuna mpasuko yule kinara wa kupandikiza chuki alishafariki march 2021
Kinara anaishi na yupo makini kweli kweli kwa kujiaminisha hivyo.

Yule unayemuita kinara wa kupandikisha chuki yeye ni matokeo ya black pope mwenyewe.
 
Sasa membe ni raia wa kawaida amefariki unataka apewe heshima gani hakua rais wa nchi
Kwani wakifa viongozi waandamizi wote hupewa heshima ya rais? Membe watu wamemzira ndio ukweli, hata magazeti mengine yanaandika taarifa za kifo chake kichwa cha habari kwa herufi ndogo..
 
Mtu anasema "mungu ameamua ugomvi" "wazuri hawafi" hadharani! Huko pembeni wameongea mangapi? Alafu huyo mtu anateuliwa kuwa waziri!

Hivi enzi hii nchi ikiwa na viongozi wenye nidhamu mtu aseme hadharani maneno ya kejeli kwa Amri jeshi mkuu aliyefia madarakani hata mwaka haujaisha angepewa uwaziri?

Lazima kilichotokea kiwekwe sawa Kitaifa maana wananchi walisikia kwa masikio yao hadharani! Yamebakia mioyoni mwao! Alafu mnaandika makala ndeeeefu! Kweli mkuki kwa nguruwe aisee!
 
Kwani wakifa viongozi waandamizi wote hupewa heshima ya rais? Membe watu wamemzira ndio ukweli, hata magazeti mengine yanaandika taarifa za kifo chake kichwa cha habari kwa herufi ndogo..
Hakuna aliyemzira membe hiyo umesema wewe nafasi ya membe aliyokua nayo ana ahaki ya kuzikwa kimya kimya mtu hata hakuwahi kuwa waziri mkuu
 
Mtu anasema "mungu ameamua ugomvi" "wazuri hawafi" hadharani! Huko pembeni wameongea mangapi? Alafu huyo mtu anateuliwa kuwa waziri!

Hivi enzi hii nchi ikiwa na viongozi wenye nidhamu mtu aseme hadharani maneno ya kejeli kwa Amri jeshi mkuu aliyefia madarakani hata mwaka haujaisha angepewa uwaziri?

Lazima kilichotokea kiwekwe sawa Kitaifa maana wananchi walisikia kwa masikio yao hadharani! Yamebakia mioyoni mwao! Alafu mnaandika makala ndeeeefu! Kweli mkuki kwa nguruwe aisee!
Viongozi huamini kwamba wana akili nyingi kuliko wanaowaongoza.
 
Sikutegemea kama ungetoa comment kama hii
Nikuulize swali who is yusuphu makamba kwenye hii nchi ni mazuri yapi au mabaya yapi kwa aliyoyafanya
kwa watanzania walio wengi makamba is nobody
Kauli ya WAZURI HAWAFI ni pana na nzito sana kwa watanzania wengi... mzee alionekana kuwa na furaha kwa kifo cha jpm ila kauli hiialimaliza kila kitu... licha ya ukawaida wake siku akifa hii kauli itaimbwa sana... na myopics ndio hawaoni upana wa hii kauli.
 
Kumbe hujanielewa kabisa.

Mimi nipo ninaandika hapa si kwa sababu ya wema wangu, ujanja wangu au ujasiri wangu, bali ni kwa rehema za Mwenyezi Mungu ambaye huwanyeshea mvua watu, huwapa hewa watu wote, wema na wabaya.

Hakuna aliye mtakatifu ila wapo wanaopenda kuwa watakatifu, hao ndio wakeshao kuitafuta hekima ya Mungu.
Tunakujua wewe ni mtu mzuri hautokufa
 
Kauli ya WAZURI HAWAFI ni pana na nzito sana kwa watanzania wengi... mzee alionekana kuwa na furaha kwa kifo cha jpm ila kauli hiialimaliza kila kitu... licha ya ukawaida wake siku akifa hii kauli itaimbwa sana... na myopics ndio hawaoni upana wa hii kauli.
Makamba ni nani kwenye hii nchi je alishawahi kuwa rais au waziri mkuu au hata mbunge unavyosema kauli yake ni kubwa yeye makamba ana kubwa gani kwenye hii nchi
 
Mtu anasema "mungu ameamua ugomvi" "wazuri hawafi" hadharani! Huko pembeni wameongea mangapi? Alafu huyo mtu anateuliwa kuwa waziri!

Hivi enzi hii nchi ikiwa na viongozi wenye nidhamu mtu aseme hadharani kwa Amri jeshi mkuu aliyefia madarakani hata mwaka haujaisha angepewa uwaziri?

Lazima kilichotokea kiwekwe sawa Kitaifa maana wananchi walisikia kwa masikio yao hadharani! Yamebakia mioyoni mwao! Alafu mnaandika makala ndeeeefu! Kweli mkuki kwa nguruwe aisee!
Mkuki kwa nguruweeeee, hakuna anae furahia kifo cha mtu ila tunawakumbusha maneno yao. Mimi nilijuwa wana bina ya maisha kumbe nao parapanda inaweza lia?

" wema hawafi"
 
Katika hali ya kawaida, hakuna binadamu mwenye akili timamu ambaye hufurahia kifo cha binadamu mwenzake, labda binadamu huyo aliyekufa awe ni mtu ambaye uwepo wake unasababisha vifo vya wanadamu wenzake, yaani awe muuaji, au kama binadamu huyo uwepo wake huwafanya binadamu wenzake wasiwe na amani, waishi kwa hofu, yaani awe ni hatari kwa amani na ustawi wa binadamu wenzake.

Sasa wamezuka watu, ambao naamini ni punguani, wanasema eti wanafurahia kifo cha Bernard Membe (Mungu amrehemu mja wake). Jambo linaloleta faraja kubwa, hao watu punguani, hakuna hata mmoja aliyesema kuwa anafurahia kifo cha Bernard Membe kwa sababu alikuwa ni mtu mbaya. Hakuna aliyesema kuwa Membe alikuwa muuaji au alikuwa hatari kwa ustawi wa jamii ya Watanzania au alisababisha watu kukosa amani, au kuishi kwa hofu, au alikuwa chukizo kwa mtu yeyote yule. Mtu akikuchukia ukiwa huna kosa wala uovu wowote, hustahili kuhuzunika, utambue tu kuwa mtu huyo ni mgonjwa wa akili, na wagonjwa hawa wa akili tuwahurumie na tuwakubali kuwa ni sehemu ya jamii yetu. Wapo watu wengi ambao wapo kwenye mstari unaotenganisha walip wazima na wagonjwa wa akili. Hawa hawaokoti makopo, ila utawajua ni wagonjwa wa akili kwa kauli na wakati fulani kwa matendo yao yanayokosa ustaarabu na hekima.

Watu hawa sababu pekee wanayoitoa ni kuwa wanafurahia Membe kufariki kwa sababu Mzee Makamba alisema wema hawafi, sasa wanashangaa kwa nini mtu mwema amekufa. Maana yake ni kwamba wanakubali kuwa Membe alikuwa mtu mwema.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akikuambia jambo la kijinga na wewe ukalikubali, anakudharau, anakuona na wewe ni mjinga. Kauli ile ya Mzee Makamba kuwa watu wema hawafi, kama alimaanisha kufa kwa mwili, basi ilikiwa kauli ya kijinga, na wale walioikubali na sasa kuifanya kuwa ni reference, hakika watakuwa wajinga na punguani. Ilikuwa kauli ya kijinga ndiyo maana hata Rais Samia aliikataa palepale.

Sote tunajua wapo watu wengi waliyofanya mambo mengi makubwa ya kutukuka Ulimwenguni, hawapo Duniani, wakati majambazi yapo hai, na mengine yapo gerezani. Ukifanya reference kwenye kauli ya kijinga, unaonekana ni punguani wa akili.


Tunamwomba Mungu wa rehema uipumzishe mahali pema peponi Roho ya ndugu yetu Bernard Membe uliyemwita kwako kwa kadiri ya mpango wako kwa maisha yake.

Poleni sana wafiwa. Basi tafakarini maneno haya, na yawape amani ya Bwana.

1 The 4:13-18 SUV

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
Kwa utangulizi tu wa mada yako unaibua mjadala.
ILIKUWAJE TUKASHEREHEKEA KIFO CHA JONIJO!
 
Back
Top Bottom