Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,529
- 41,046
Katika hali ya kawaida, hakuna binadamu mwenye akili timamu ambaye hufurahia kifo cha binadamu mwenzake, labda binadamu huyo aliyekufa awe ni mtu ambaye uwepo wake unasababisha vifo vya wanadamu wenzake, yaani awe muuaji, au kama binadamu huyo uwepo wake huwafanya binadamu wenzake wasiwe na amani, waishi kwa hofu, yaani awe ni hatari kwa amani na ustawi wa binadamu wenzake.
Sasa wamezuka watu, ambao naamini ni punguani, wanasema eti wanafurahia kifo cha Bernard Membe (Mungu amrehemu mja wake). Jambo linaloleta faraja kubwa, hao watu punguani, hakuna hata mmoja aliyesema kuwa anafurahia kifo cha Bernard Membe kwa sababu alikuwa ni mtu mbaya. Hakuna aliyesema kuwa Membe alikuwa muuaji au alikuwa hatari kwa ustawi wa jamii ya Watanzania au alisababisha watu kukosa amani, au kuishi kwa hofu, au alikuwa chukizo kwa mtu yeyote yule. Mtu akikuchukia ukiwa huna kosa wala uovu wowote, hustahili kuhuzunika, utambue tu kuwa mtu huyo ni mgonjwa wa akili, na wagonjwa hawa wa akili tuwahurumie na tuwakubali kuwa ni sehemu ya jamii yetu. Wapo watu wengi ambao wapo kwenye mstari unaotenganisha walip wazima na wagonjwa wa akili. Hawa hawaokoti makopo, ila utawajua ni wagonjwa wa akili kwa kauli na wakati fulani kwa matendo yao yanayokosa ustaarabu na hekima.
Watu hawa sababu pekee wanayoitoa ni kuwa wanafurahia Membe kufariki kwa sababu Mzee Makamba alisema wema hawafi, sasa wanashangaa kwa nini mtu mwema amekufa. Maana yake ni kwamba wanakubali kuwa Membe alikuwa mtu mwema.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akikuambia jambo la kijinga na wewe ukalikubali, anakudharau, anakuona na wewe ni mjinga. Kauli ile ya Mzee Makamba kuwa watu wema hawafi, kama alimaanisha kufa kwa mwili, basi ilikiwa kauli ya kijinga, na wale walioikubali na sasa kuifanya kuwa ni reference, hakika watakuwa wajinga na punguani. Ilikuwa kauli ya kijinga ndiyo maana hata Rais Samia aliikataa palepale.
Sote tunajua wapo watu wengi waliyofanya mambo mengi makubwa ya kutukuka Ulimwenguni, hawapo Duniani, wakati majambazi yapo hai, na mengine yapo gerezani. Ukifanya reference kwenye kauli ya kijinga, unaonekana ni punguani wa akili.
Tunamwomba Mungu wa rehema uipumzishe mahali pema peponi Roho ya ndugu yetu Bernard Membe uliyemwita kwako kwa kadiri ya mpango wako kwa maisha yake.
Poleni sana wafiwa. Basi tafakarini maneno haya, na yawape amani ya Bwana.
1 The 4:13-18 SUV
Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.