Wenye utimamu msihuzunike wengine wanaposhangilia kifo cha Membe

Wenye utimamu msihuzunike wengine wanaposhangilia kifo cha Membe

Nakuona team wema hawafi ukiwa umepoa baada ya vidonge kukuingia vizuri
Nilaumu kwa mengine lakini siyo kwa kuniweka kwenye hiyo jmayoiita, timu wema.

Hata nipungukiwe akili kiasi gani, siwezi kufikia hatua ya kusema kuwa wema huwa hawafi (yaani kifo cha mwili). Kiroho, ni kweli, watakatifu wa Mungu hawafi. Lakini mwili huu tulio nao, uaminishwe kuwa wa mtu mwema huwa haufi, nawe ukaamini, utakuwa mzima?

Makamba ambaye siku hiyo hiyo anatoa kauli hiyo, alisema pia watanzania hawahitaji katiba mpya! Halafu huyo ndiye uniweke pamoja naye?

Tafuta kwenye posts zote zinazohusiana na hiyo kauli kama utaipata post yangu au hata like kwenye 'waru wema hawafi'. Niliposikia kauli hiyo niliipuuza, maana ilikuwa ni sawa mtu akuambie kuwa watu wema huwa wanaishi bila kula chakula chochote!!!
 
Nilaumu kwa mengine lakini siyo kwa kuniweka kwenye hiyo jmayoiita, timu wema.

Hata nipungukiwe akili kiasi gani, siwezi kufikia hatua ya kusema kuwa wema huwa hawafi (yaani kifo cha mwili). Kiroho, ni kweli, watakatifu wa Mungu hawafi. Lakini mwili huu tulio nao, uaminishwe kuwa wa mtu mwema huwa haufi, nawe ukaamini, utakuwa mzima?

Makamba ambaye siku hiyo hiyo anatoa kauli hiyo, alisema pia watanzania hawahitaji katiba mpya! Halafu huyo ndiye uniweke pamoja naye?

Tafuta kwenye posts zote zinazohusiana na hiyo kauli kama utaipata post yangu au hata like kwenye 'waru wema hawafi'. Niliposikia kauli hiyo niliipuuza, maana ilikuwa ni sawa mtu akuambie kuwa watu wema huwa wanaishi bila kula chakula chochote!!!
Makamba huyohuyo wanayem quote leo kwa kauli yake ya 'Wema hawafi' ndiye huyo huyo waliyemshangilia kipindi kile anasema 'anawabatiza kwa moto'.
Huyo Makamba ni mwenzao, maana ana tabia zao zote
 
Mtu anasema "mungu ameamua ugomvi" "wazuri hawafi" hadharani! Huko pembeni wameongea mangapi? Alafu huyo mtu anateuliwa kuwa waziri!

Hivi enzi hii nchi ikiwa na viongozi wenye nidhamu mtu aseme hadharani maneno ya kejeli kwa Amri jeshi mkuu aliyefia madarakani hata mwaka haujaisha angepewa uwaziri?

Lazima kilichotokea kiwekwe sawa Kitaifa maana wananchi walisikia kwa masikio yao hadharani! Yamebakia mioyoni mwao! Alafu mnaandika makala ndeeeefu! Kweli mkuki kwa nguruwe aisee!

...zipo sababu nyingi za kukausha vyanzo vyote vya maji......visima, mifereji, mito, maziwa na hata bahari ikibidi. mawe mpaka milima isogezwe!Yaani juhudi zifanyike ujulikane Ukweli, na ndio maana naona Maridhiano au kitu chochote kinachofanana na hicho, kisiwe ndii changa la macho kana ilivyotokea Afrika ya Kusini na Tume ya Desmond Tutu R.I.P -Kulikuwa hakuna haki! na Ilificha na kuhalalisha Udhalimu wa mabeberu. Hili jambo lisitokee Tanzania tukaenda kuficha ukweli na kuhalalisha Udhalimu? Chuki na Visasi binafsi! Ukifuatilia vizuri, timu inayotoa maneno ya Chuki dhidi ya Hayati JPM ndio timu inayotaka na kushauri uwepo wa Tume kana ya Desmond Tutu-Amnesty!

MTAZAMO Umenena. Kitaeleweka.
 
Katika hali ya kawaida, hakuna binadamu mwenye akili timamu ambaye hufurahia kifo cha binadamu mwenzake, labda binadamu huyo aliyekufa awe ni mtu ambaye uwepo wake unasababisha vifo vya wanadamu wenzake, yaani awe muuaji, au kama binadamu huyo uwepo wake huwafanya binadamu wenzake wasiwe na amani, waishi kwa hofu, yaani awe ni hatari kwa amani na ustawi wa binadamu wenzake.

Sasa wamezuka watu, ambao naamini ni punguani, wanasema eti wanafurahia kifo cha Bernard Membe (Mungu amrehemu mja wake). Jambo linaloleta faraja kubwa, hao watu punguani, hakuna hata mmoja aliyesema kuwa anafurahia kifo cha Bernard Membe kwa sababu alikuwa ni mtu mbaya. Hakuna aliyesema kuwa Membe alikuwa muuaji au alikuwa hatari kwa ustawi wa jamii ya Watanzania au alisababisha watu kukosa amani, au kuishi kwa hofu, au alikuwa chukizo kwa mtu yeyote yule. Mtu akikuchukia ukiwa huna kosa wala uovu wowote, hustahili kuhuzunika, utambue tu kuwa mtu huyo ni mgonjwa wa akili, na wagonjwa hawa wa akili tuwahurumie na tuwakubali kuwa ni sehemu ya jamii yetu. Wapo watu wengi ambao wapo kwenye mstari unaotenganisha walip wazima na wagonjwa wa akili. Hawa hawaokoti makopo, ila utawajua ni wagonjwa wa akili kwa kauli na wakati fulani kwa matendo yao yanayokosa ustaarabu na hekima.

Watu hawa sababu pekee wanayoitoa ni kuwa wanafurahia Membe kufariki kwa sababu Mzee Makamba alisema wema hawafi, sasa wanashangaa kwa nini mtu mwema amekufa. Maana yake ni kwamba wanakubali kuwa Membe alikuwa mtu mwema.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akikuambia jambo la kijinga na wewe ukalikubali, anakudharau, anakuona na wewe ni mjinga. Kauli ile ya Mzee Makamba kuwa watu wema hawafi, kama alimaanisha kufa kwa mwili, basi ilikiwa kauli ya kijinga, na wale walioikubali na sasa kuifanya kuwa ni reference, hakika watakuwa wajinga na punguani. Ilikuwa kauli ya kijinga ndiyo maana hata Rais Samia aliikataa palepale.

Sote tunajua wapo watu wengi waliyofanya mambo mengi makubwa ya kutukuka Ulimwenguni, hawapo Duniani, wakati majambazi yapo hai, na mengine yapo gerezani. Ukifanya reference kwenye kauli ya kijinga, unaonekana ni punguani wa akili.


Tunamwomba Mungu wa rehema uipumzishe mahali pema peponi Roho ya ndugu yetu Bernard Membe uliyemwita kwako kwa kadiri ya mpango wako kwa maisha yake.

Poleni sana wafiwa. Basi tafakarini maneno haya, na yawape amani ya Bwana.

1 The 4:13-18 SUV

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
Mkuu wazuri hawafi pamoja na mapunguani..
 
Hakuna draw. Acha movie iendelee mpka pale walengwa haswaaaa watakapokinywa kikombe kwa kipimo kilekile. Wazuri hawafi. Aluta Continua
Ila kwanini hawa "wabaya" hawafi kwa uzee? Nini kipo nyuma ya pazia? Yaani utaskia mara upasuaji, mara moyo mara mafua ni kwanini hawafi kwa uzee wanaondoka hawajafika hata umri wa kwenye maandiko..ni kwamba wanaondolewa na kikundi cha "malaika" wanaowalinda wale "wema" wasife au?
 
Back
Top Bottom