Wenye magari jihadhari na Camel-Oil Tabata Sanene

Wenye magari jihadhari na Camel-Oil Tabata Sanene

Verily Verily

Senior Member
Joined
Jan 4, 2007
Posts
192
Reaction score
148
Kituo hiki cha mafuta kilichoko upande wa kulia kama unaelekea mjini pale Tabata Sanene ni hatari kwa magari maana wanachanganya sana mafuta ya taa na petrol na mbaya zaidi wanaiba sana mafuta pamoja na kuchakachua huko. Magari yanazimika, pump zinakufa.

Wateja walio wengi wameisha wajua na kwa sasa hawaweki tena mafuta kwenye kituo hicho. Kituo kina machine nyingi na uwanja mpana tena mzuri lakini unaweza kukuta gari moja tu tena nalo la watu walio wageni mitaa ile.

Shime epukeni hasara ndugu wananchi.

NB: Tafadhali Mod acha huu uzi ili kusudi wakazi wa Tabata wachukue tahadhari kabla hawajapata hasara ya magari yao. Ni wakati sasa kuwaadabisha wezi, wanyonyaji na wauaji wanaowaumiza wananchi kwa ajili ya kujipatia faida. Tunatoa tahadhari na kwa wezi wengine wa mafuta hatutasita kuwaanika mpaka watakapo acha tabia mbaya ya wizi na uuaji.
 
Daaaaah nimeweka pale ya sh.20,000 eeh mungu nisaidie,basi tabata hapafai coz hata ile lake oil pale tabata ni balaa gari ya uncle yangu ilikufa pump na siku tumeenda kulalamika tukakuta gari nyngn tatu pale nazo zimekufa pump!!!
 
weka picha

Immortal acha utani kwenye mambo ya msingi. Nimeweka street address ya Camel Oil Tabata Sanene na iko upande wa kulia ukiwa unaelekea mjini.

Unataka picha zaidi ya kitu gani? Petrol iliyochanganywa na kerosine, manouveur ya pump inayoiba mafuta au gari iliyozimika?? Kuwa mwazi na serious kidogo bana Immortal!!
 
Camel is the worst of them all. Ukiweka mafuta yao lazima daladala ipige miss, sio hiyo tu. Ni zote.

Mie niliwashtukia siku nyiiiiingi, huwa siweki labda niwe kwenye hatari ya kukatikiwa wese, na nikiweka hayazidi elfu kumi, ya kunifikisha kituo kingine tu.
 
Nilidhani kwa vile sasa bei ya mafuta ya taa imekaribiana sana na bei ya petrol uchakachuaji uchakachuaji ungepungua!
 
ahsante kwa taarifa maana wanatuumiza sana sie wa vigari vya mkopo.:A S cry:
 
Daaaaah nimeweka pale ya sh.20,000 eeh mungu nisaidie,basi tabata hapafai coz hata ile lake oil pale tabata ni balaa gari ya uncle yangu ilikufa pump na siku tumeenda kulalamika tukakuta gari nyngn tatu pale nazo zimekufa pump!!!

Pump siku hizi zinakufa sana!yani ni usumnufu sana!
 
Kwa mafuta safi bila kuchakachuliwa basi weka kwenye vituo vyoote engen jamaa wako vizuri sana nikweka mafuta sehemu nyingine hua inakua tofauti sana km
 
Nilidhani kwa vile sasa bei ya mafuta ya taa imekaribiana sana na bei ya petrol uchakachuaji uchakachuaji ungepungua!

Logically ungedhani hivo but hawa manyang'au wana motives nying nyingine mfano:

1. Kama petrol imeisha na kerosene ipo wanaona wachakachue biashara isisimame
2. Kerosene bado bei yake iko chini kwa sh. kama 200. Ukiuza tani kadhaa bado ni faida kubwa tu
3. Huwezijua wanachanganya na vitu vingine vingi tu zaidi ya kerosene, hata maji wanaweka!
4. Vigari vy mikopo vikifa tutakuwa wategemezi kwao kwa kila kitu
5. Etc, etc
 
mkuu mimi ni mkazi wa tabata ni ni muhanga wa hiyo sheli. niliweka wese la 50 ambalo kwa kawaida huwa naendea town wiki nzima but nilivyoweka pale hakiyanani nilienda town mara 3 tu. ni wezi sana wale jamaa hawafai.
 
Pale nishawekewa futa la 1000 mara 2 huku nmetoa 10000....jirani yangu aliwekewa futa la 2000 alitoa 20000.... Shemeji yangu aliwekea futa la buku pia katoa buku kumi....kile kituo ni majanga na wezi sana mafuta yao yanaharibu gari linamiss...nishawahi kurudi pale baada ya kuwekewa mafuta ya buku gari likazimika wale wafanyakaz wakaomba radhi na kuniwekea mafuta tena wakiomba nisiseme kwa boss wao....kile kituo usikanyage ni wezi sana......
 
Asante mkuu kwa tahadhari. Mimi nilishaacha kuweka mafuta hapo siku nyingi wakati kituo hicho kikiwa hata hakijafikisha miezi sita. Nilipakimbia hapo kwa kuwa kulikuwa na dada mmoja mweupe mnene kiasi ambaye alikuwa ni mwizi sana. Yaani ukitaka kuweka mafuta ya shilingi 20,000, basi atakuwekea ya shilingi 5,000 tu.
 
Siku utaambiwa mke wako anashikishwa ukuta halafu utasema weka picha.
wacha matusi, jadili mada. mbona mhusika amejibu vizuri, usiwe kama kagame ameshauriwa na jk badala ya kukataa au kukubali ushauri anaanza matusi kwa jk.
 
Back
Top Bottom