Foleni ya magari barabara ya Tabata jana na leo ni usumbufu na uonevu kwa raia

Kaluguyu

Senior Member
Jun 21, 2011
174
135
Kwa wakazi wa Tabata, Segerea, Kinyerezi na wanaotumia Barabara ya Tabata kupitia Tabata Reli kwa siku mbili hizi zimekuwa ni ngumu pamoja na kujitahidi kutoka mapema lakini kulikuwa FOLENI isiyo na msingi kwani ilikuwa inasababishwa na Askari mmoja au kundi la askari waliokuwa wanasimamisha magari pasipo kuwa na sababu za msingi.

Mfano ukamataji ulikuwa pale kwenye kituo cha Daladala cha Barakuda kwa wanao kwenda mjini zile Eicher zilikuwa zimejaa na wenye gari ndogo waliokuwa wanazikwepa kwa kupita njia ya kurudia toka mjini walikuwa wanakamatwa kwa kosa la KU "OVERTAKE" na kukamatwa na kuswekwa lock up tokea jana hadi leo asubuhi wengine ndio wametolewa kwa Dhamana.

Nawashauri askari wetu badala ya kusubiri watu wakosee na kuwakama au kuwatoza faini ingekuwa vyema kama mngezuia zile daladala pale kituoni.

Tahadhari! kwa waendesha magari jihadhari ku overtake gari hata kama limesimama njiani kuanzia Barakuda hadi LIWITI ni maeneo ya uonevu.
 
Kwani overtaking ni kosa? Hebu tueleweshe hilo eneo likoje na kwanini kuovateki hairuhusiwi.
 
Kwa leo hawakujali hata ile adha ya mvua na kulikuwa na askari mwanamke ambae alikuwa kasimama katikati ya barabara mbele ya bar ya Barakuda akisimamisha magari kupelekea foleni isiyokuwa na maana yeyote kwa magari yaendayo relini.
Hawakuwa na mashine za fine hivyo ilikuwa ni njia mbadala ya kujipatia pesa za kubrashia viatu.
 
Kwani overtaking ni kosa? Hebu tueleweshe hilo eneo likoje na kwanini kuovateki hairuhusiwi.
Wanashurtisha kufanya ionekane ni overtaking lakini kihalisia ni hali ya kukata corner tu kuingia njia nyingine. Kutokana na foleni hakukuwa na ulazima wa kusubiri mpaka kufika usawa wa corner kabisa hivyo kitendo cha kutoka kabla ya kufika usawa wa barabara wao wanakukamata. Cha kustaajabisha siku nyingine hao hao traffic ndio hushurtisha wale walio indicate kuelekea Barakuda kufanya hilo hilo waliloliita overtaking leo.
 
Alafu bavicha unakuta wanalialia eti hela hakuna maisha magumu!!!

Haya magari yananunuliwa na nini?
 
Back
Top Bottom