Wenye magari jihadhari na Camel-Oil Tabata Sanene

Wenye magari jihadhari na Camel-Oil Tabata Sanene

wahusika wachukue hatua haraka dhidi ya hiki kituo cha mafuta
 
Kituo hiki cha mafuta kilichoko upande wa kulia kama unaelekea mjini pale Tabata Sanene ni hatari kwa magari maana wanachanganya sana mafuta ya taa na petrol na mbaya zaidi wanaiba sana mafuta pamoja na kuchakachua huko. Magari yanazimika, pump zinakufa.

Wateja walio wengi wameisha wajua na kwa sasa hawaweki tena mafuta kwenye kituo hicho. Kituo kina machine nyingi na uwanja mpana tena mzuri lakini unaweza kukuta gari moja tu tena nalo la watu walio wageni mitaa ile.

Shime epukeni hasara ndugu wananchi.

NB: Tafadhali Mod acha huu uzi ili kusudi wakazi wa Tabata wachukue tahadhari kabla hawajapata hasara ya magari yao. Ni wakati sasa kuwaadabisha wezi, wanyonyaji na wauaji wanaowaumiza wananchi kwa ajili ya kujipatia faida. Tunatoa tahadhari na kwa wezi wengine wa mafuta hatutasita kuwaanika mpaka watakapo acha tabia mbaya ya wizi na uuaji.

duuuh ndio maana kila asubuhi huwa najikuta peke yangu wakati kituo cha lake Oil pembeni kimejaaa magari plus bodabodaa, UMENIFUNGUA MACHO JIRANI
 
Habari za uwongo + usipende kuita watu wezi,wanyonyaji wakati huwajui mwanzo wala mwisho
 
Habari za uwongo + usipende kuita watu wezi,wanyonyaji wakati huwajui mwanzo wala mwisho

Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh wote waliochangia huu uzi unaona ni waongo, ni kweli ni wezi na mimi ilinikumba niliweka mafuta ya 60,000 na yakukuwa ni kuongezea yaliyokuwepo ili tank ijae na haikufika hata robo tatu wakati ndicho kilikuwa kipimo halisi kwa gari yangu. Nilipoona gage haisogei inavyotakiwa nikaweka gari pembeni nikawatishia ninaomba mawasiliano ya kiongozi wenu wa zamu leo kabla ya meneja wa kituo na hatimaye mmiliki. Walikuwa wadada watatu na kijana mmoja pale wakaanza kutetemeka ooh mara hiki mara vile mara ohh samahani labda upepo uliingia, tunaomba tukujazie kama unavyotaka!!! Walijaza gari kama ilivyotakiwa na kuomba radhi kwa wingi. Sasa nikawakomesha, nikawa napita hapo mara kadhaa kuweka na wakiona gari tu wanakuwa makini sana na mchezo ukawa mwisho kuniibia. Anyaway, nilishaondoka maeneo hayo muda ila hakika kile kituo hakikuwa tofauti na kila kilichokuwa cha mwanamboka Kinondoni Enzi hizo, wadada wezi hatari walikuwa ukiondoa gari tu wanaleta kidumu fasta kuweka waliyoiba.
 
kituo hiki cha mafuta kilichoko upande wa kulia kama unaelekea mjini pale tabata sanene ni hatari kwa magari maana wanachanganya sana mafuta ya taa na petrol na mbaya zaidi wanaiba sana mafuta pamoja na kuchakachua huko. Magari yanazimika, pump zinakufa.

Wateja walio wengi wameisha wajua na kwa sasa hawaweki tena mafuta kwenye kituo hicho. Kituo kina machine nyingi na uwanja mpana tena mzuri lakini unaweza kukuta gari moja tu tena nalo la watu walio wageni mitaa ile.

Shime epukeni hasara ndugu wananchi.

Nb: Tafadhali mod acha huu uzi ili kusudi wakazi wa tabata wachukue tahadhari kabla hawajapata hasara ya magari yao. Ni wakati sasa kuwaadabisha wezi, wanyonyaji na wauaji wanaowaumiza wananchi kwa ajili ya kujipatia faida. Tunatoa tahadhari na kwa wezi wengine wa mafuta hatutasita kuwaanika mpaka watakapo acha tabia mbaya ya wizi na uuaji.

team majungu at work
 
Umetufungua macho inawezekana wizi huu umeenea tulijua kadhia hii iliisha baada ya mafuta ya taa kupanda bei kumbe wameona hayanunuliki wanachanganya na petrol
 
kuna oilcom pale segerea kona nilishawahi kuweka mafuta ya 30,000 kufika kibamba kupitita kinyerez, maramba mawili eti taa ikawaka na ni kama 20km tu
 
Kiboko madereva wa taxi wakienda kuweka mafuta wanaweka kwenye kidumu cha lita tano, sasa hapo watamwibia vp? Akitoka hapo anaenda kimimina kwenye tank lake.. tatizo sie na vigari vya mkopo tukifika petrol station tuna kuwa mabwanyenye sana mziki mkubwa full ac hutaki hata uone lita ngapi unawekewa ... sasa mi nauliza petrol station gani ni uhakika hatuibiwi? Mi huwa natumia sana pale total makao makuu.
 
Asante kwa tahadhari. Ukweli tunapaswa kujulishana vituo vyote vinavyochakachua kuibia wateja mafuta kwa kujaza hewa.
 
Aisee kumbe bado hawajaacha hii tabia yao? Muda mrefu saana wamekuwa wakilalamikiwa. Na hawa Ewura sijui wako wapi? Kwanini hawaendi pale?

Kwa ujumla vituo vya Oil com na Camel ni majanga.
 
Kwahiyo ni gas stations zipi ambazo mafuta yake ni mazuri hawachakachui?
 
Mimi niliweka mafuta mahali majuzi sasa gari inamisi vibaya sana. Wazo moja linaniambia nicheck plug lakini lingine linaniambia huenda mafuta niliyoyaweka yalikuwa yamechakachuliwa!
 
Vituo vya kuwekea mafuta kwa gari yako hapa dar Total , BP/Puma na Victoria hawa ndo uhakika, wengine wezi watupu.......Gapco walishaniwekea hewa mbumbavu zao, otherwise ukinunua mafuta kwao uhakikishe horse linatoa mafuta nasiyo linapuliza upepo
 
Back
Top Bottom