Wenye imani kwamba mitandao ya kijamii haiwezi kukupa mke, mume au mpenzi wa kweli bora wajitoe wabaki kwenye mfumo wa kizamani na sehemu za ibada

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,061
Utandawazi na njia za masiliano zime rahisisha namna ya kukutana na kufahamiana na watu tofauti na njia za kizamani za hadi ukutane na mtu uso kwa uso, mfano kanisani, kongamano, bar, harusini, dukani, barabarani, msibani, etc.etc.

kufahamiana kwa namna yoyote ile ni halali, kitu muhimu ni pamoja na kuzingatia mifumo yako namna ya kujenga imani na watu au mtu.

Hii Dunia imejaa baadhi viumbe wapumbavu sana, yaani kwa hiari yako mwenyewe unajiunga na mitandao ya kijamii, wakati imani yako unaamini mitandao ni sehemu iliyojaa watu wahuni wenye dhambi, na kwamba mavuno yake ni upotofu.

Je, sasa hawa walokole na wana wa Mungu wanatafuta nini huku kwenye madhabahu ya shetani?

Hatuwaoni wakieneza injili ya bwana katika maudhui yao ama katika uwepo wao kwenye mitandao.

Sasa cha ajabu unawezaje kujumuika sehemu moja na watu potofu na wenye dhambi ambao hawana sifa za kuwa mke, mume, wala mpenzi?

Mwanamke akiombwa namba ya simu anatoa, anasema wasifu wake wote hadi anapoishi na mambo mengine mengi mfano status yake ya kuwa single plus watoto, kaolewa, kaachika, na etc.etc.

Balaa la ushamba na uzuzu linaanza wakati unataka uwe na mahusiano nae anaongea ushetani mara ooh tangu lini mitandao ya kijamii ikawapatia watu wake, waume au wapenzi wa kuaminika?

Nawapa jibu moja Mungu hawezi kufanya wewe ukutane na shetani kwa maana hujapatikana kwenye madhabahu ya bwana hivyo bwana yupo popote pale wakati wowote ule. Ukiwa ni mwenye kuamini basi nalo neno lake likawe sehemu ya kunibariki kuingia nafsini mwako amen.🙏🙏🙏

Jamii ya watu wenye akili kama hizi vichwa vyao ni matope kabisa, ukijiona wewe ni msafi ama ni mtu wa Mungu achana kabisa na makusanyiko ya kidunia ambayo kwa imani baadhi ya viumbe wanahusisha na ibilisi.

Nawaambia hivi huku kwenye mitandao ya kijamii sisi watoto teule wa Mungu tupo na utajaa tu kwenye reli.

Karibu tuendelee na comments nimejaa tele kama pishi la biriani.

Shukrani 🙏🙏🙏

Wadiz
 
Back
Top Bottom