Mtazamo wangu: Mpenzi, Mume au Mke akicheat mara moja asamehewe bila kinyongo.

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,061
Wasalaam wana wa Mungu,

Kosa au dhambi unayoichukia kwa mwingine basi nawe usifanye kwa maana machukizo mbele ya Mungu ni yale yale.

Wanadamu sisi sote tu wana wa Mungu na makosa yote tumeumbiwa sisi, panapo safari iwayo yoyote ikiwemo ya urafiki wa mapenzi kukosana na kukosea ni sehemu ya mapito ya safari.

Safari zina milima na mabonde na hayo mabonde na milima tunapaswa walau kwa ujumla au aina zake tujua bayana yapi ni makwazo na yapi ni furahishi.

Utofauti wa kifikra na maamuzi katika muktadha wa jinsia ni changamoto yetu mojawapo, mfano mwanaume hutumia logic katika kutafakari na kuamua, mwanamke hutumia hisia katika tafakuri na maamuzi.

Dhana ya kusamehe 7 x 70 sidhani kama ni tenganishi katika muktadha utubu wa dhambi, je, ungamo lolote lenye kukiri kosa kwa dhati na kutubu halifai machoni pa Mungu? Kama ni ndio basi nguvu na uimara katika nguzo za Mungu makosa husemeheka ikiwemo kosa la kucheat.

Na wapingaji mjipange kwa kutazama kisa sababu na muktadha maudhui na hadhira, faida na hasara ya maamuzi, na kuridhia taswira ya ushawishi na kuaminishwa na toba ya mkosaji.

Nguzo za kuamini zijikite katika nafsi, mwili na roho ukijikita katika faida na hasara na maamuzi yako yafanye tathmini ya ubora na uimara wako katika kosa kama hilo au mengineyo yenye uzito sawa au pungufu ili hali katika Imani yote ni sawa.

Mfano umemkamata mwenzako anacheat au umepata ushahidi kuwa ana cheat, ili hali wewe pia unacheat ila hujastukiwa au vyovyote vile.

Sasa basi endapo hujaweka misingi bayana ya mambo furahishi na chukizi sambamba na faida na hasara zake, kuna kosa la kiongozi na malezi, na ukosefu wa miongozo ama guidelines and regulations.

Endapo mtu amefanya kosa ambalo lilihitaji muongozo ili lisifanyike basi ni haki na wajibu kusamehe beba kama sehemu ya uzembe wako.

Wekeni bayana namna ya kuishi faraha baina yenu na wekeni bayana njia na matendo yanayoshabihiana na machukizo.

Anafanya kwa kutokukusudia ni rahisi sana kumgundua hapa pasipo macho ya rohoni, kupitia medani za lugha ya mwili, na level za sauti hasa uzito na uhasilia wake, lugha ya macho, majuto ya hisia katika uongeaji.

Niishie hapa naomba wana wa Mungu aliyehai muongeze sababu, muktadha kadha wa kadha.

Wote tuna sifa ya kusamehe na kusamehewa mbele ya wana Mungu na Mungu mwenyewe.

Busara na hekima ya kumuishi Mungu nguzo yake ni pamoja na kuwa mjinga na mpumbavu kwenye fikra na maamuzi ya kudumisha amani na urafiki au udugu wetu

Shukrani 🙏🙏🙏

Wadiz
 
Kama Mungu mwenyewe kawaandalia waovu moto bila msamaha kwanini sasa wewe usamehe?
 
Kama nawe ni mzee wa kuchepuka samehe bila kinyongo na mpeleke shopping Dubai au Mlimani City kama uchumi hauruhusu kukwea pipa.

Lakini kama hujawahi kabisa kuchepuka wala hauna dhamira ya kuchepuka hata huko mbeleni, piga chini huyo mchepukaji mara moja bila kumpa nafasi ya kujitetea.
 
Kama nawe ni mzee wa kuchepuka samehe bila kinyongo na mpeleke shopping Dubai au Mlimani City kama uchumi hauruhusu kukwea pipa.

Lakini kama hujawahi kabisa kuchepuka wala hauna dhamira ya kuchepuka hata huko mbeleni, piga chini huyo mchepukaji mara moja bila kumpa nafasi ya kujitetea.
Kwenye kupiga chini hio option ya pili inabidi ufanye tafakuri zaidi expand ur thinking options
 
Back
Top Bottom