Mitandao ya Kijamii na uwajibikaji wa Raia wa kidigitali

Aug 5, 2019
62
87
Tangu kuanzishwa kwa mitandao ya kijamii imekuwa ni njia rahisi na nyepesi ya kuwafanya watu kukutana kwa uharaka hata kama wapo katika umbali mkubwa sana, leo hii mtu anaeishi Tanzania anaweza kuongea na kuonana kwa macho na mtu anaeishi katika nchi nyingine nyingi Duniani. Urahisi huu umeletwa na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Watu mbalimbali duniani hutumia mitandao hii katika kufanya kazi zinazowaingizia kipato pamoja maisha yao binafsi. Mfano mzuri ni wanamuziki, wachezaji mpira na watu wengine maarufu ikiwemo Viongozi wakubwa duniani hutimia mitandao hii kufikisha jumbe mbali mbali.

Ifahamike kuwa hakuna jambo lenye uhuru linalokuwa halina mipaka yake kwa maana mataifa mengi duniani baada tu ya ujio wa mitandao ya kijamii yameweza kutunga sheria mbalimbali ambazo zitaweza kuwadhibiti watu ambao watakuwa na nia ovu dhidi ya wenzao katika mitandao hii.

Lakini pia pamoja na yote mitandao ya kijamii ni sehemu ya maisha ya mwanadamu wa leo kwasababu takribani asilimia 80 ya maisha yake huitegemea teknolojia ambayo inahusiana moja kwa moja na mitandao hii ya kijamii. Mwanadamu huyu huweza kuapata taarifa mbalimbali za muhimu kupitia mitandao ya kijamii na hivyo hata yeye huweza kuripoti tatizo lake na kupata msaada kwa haraka kuliko kuanza kupiga simu na kisha aweze kusaidiwa.

Ni wazi kwamba mitandao hii ya kijamii hutumia data ambazo sisi watumiaji huzitoa wakati wakufanya usajili katika aplikesheni ama katika website husika za mtandao wa kijamii. Data zetu huwa ni pamoja na majina yetu kamili, anuani za barua pepe, wasifu wako kwa ufupi lakini pia na nambari za simu pamoja na mahali husika unapoishi wewe mtumiaji.

Kwanini leo nimeamua kuongelea kuhusu mitandao hii ya kijamii licha ya kuwa imekuwepo kwa takribani miaka 14 iliyopita:-

Sababu iliyonifanya niandike Makala hii fupi ni kwamba mitandao hii ya kijamii ambayo tumeamua kutumia na kuifanya kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku ni wazi kuwa hii mitandao inabeba sura na umiliki wa hulka zetu kwa watu baki ambao hatufahamiani na wako pia katika matumizi ya mitandao hii.

Leo hii mimi nikimtukana mtu mtandaoni kupitia mtandao wangu wa kijamii au ukurasa wangu wa mtandao wa kijamii, bhasi mtu niliyemtusi hana haja ya kujiuliza mara mbili mbili maana aliyetukana anafahamika kwa majina haya nap engine kwa sura kabisa kwasababu huwa tunaweka picha zetu asilia kwenye mitandao hii.

Lakini pia kuna wale ambao huwa hawaweki picha zao asilia huku wakijinasibu kuwa hawawezi kujulikana huwa nao pia wanajidanganya kwasababu wakiamua kukufuatilia na kujua identity yako ni suala la dakika chache tu utakuwa umeshajulikana maana dunia ya leo iko na uwazi sana katika teknolojia.

Sasa inawezekana kwa takribani miaka 5 ama zaidi ya huko nyuma tangu umejiunga na mitandao ya kijamii hukuwa mtu mwema dhidi yaw engine kwa maana umewahi labda kutoa lugha za matusi kwa watu ama kuwakejeli watu ambao hata huwajui nap engine ni watu ambao wana mamlaka ya kukuchukulia hatua kali za kisheria, unachotakiwa kufanya ni kurejea machapisho yako yote ya awali na kuyafutilia mbali ili kujiweka safi mbele za Jamii.

Ni kweli kabisa inawezekana ikawa wamesha screenshot andiko lako na watu wamelisave katika kumbukumbu zao lakini amini nakuambia chapisho lako la awali kama bado lipo na hao watu wakiwa bado na screenshot yako inawathibitishia kwamba wewe bado hujutii na hujajifunza kuwa mtu mwema kwasababu ungekuwa umejifunza kutokana na makosa bhasi ungekuwa umeshalifuta hata kama hutaomba radhi.

Nitakupa mfano wa mtandao wa kijamii ambao hukukumbusha baadhi ya machapisho yako ya huko awali na mtandao huo ni Facebook. Facebook wao hukurejeshea machapisho yako ya nyuma takribani kila mwaka kwahiyo unaweza yatazama na kama kuna ambayo unaona kabisa kwakweli kwasasa namna nilivyo na ninavyo heshimiana na watu hii haiwezi kuwa picha nzuri ama maneno mazuri mbele ya watu wanao niheshimu bhasi unatakiwa tu kiustaarabu uifute na option ya kufanya namna hiyo ipo kwenye kila chapisho lako.

Sifahamu juu ya mitandao mingine lakini nimechagua facebook kwasababu ndio mtandao ambao takribani watanzania milioni 6 kwa mujibu wa jarida la www.statica.com kwa data walizokusanya Mwezi wa February 2021. Facebook ndio mtandao wenye watu wengi zaidi Duniani lakini pia ndio unao ongoza kwa kuwa na watu wengi pia kwa hapa Tanzania.

Ahsante sana kwa kutenga muda wako na kusoma Makala hii fupi
 
Back
Top Bottom