Waziri wa ujenzi: Wananchi wengi wamejenga maeneo hatarishi kama :kando ya mito, makorongo na kwenye njia za mito ya msimu chukueni tahadhari

Madam Mwajuma

JF-Expert Member
Sep 13, 2014
7,052
6,702
Nawasalimu wote.
Maeneo mengi nchini wananchi wamejenga kiholela na ni hatari kwa maisha yao na uchumi wa nchi kwani majanga yakitokea huhudumiwa na serikali.
Nyumba nyingi zimejengwa kando ya mito ya msimu, makorongo, kwenye njia za maji kabisa na wengine hujaribu kuyatengenezea maji njia mpya pembeni ya nyumba zao.

Lakini mvua zikinyesha nyingi maji yatalazimisha kupita kwenye njia zake halisi.

Wito kwa serikali: 1. Wizara na ardhi ishirikiane na wizara nyingine wazitambie nyumba hizo na kuwashauri wakazi watafute makazi mengine. (Waandikiwe barua)
2. Wananchi waambiwe kabisa wakae umbali gani kutoka kwenye njia za maji n.k

Wito kwa wananchi:
1. Tuache kujenga kando kando ya mito, njia za maji, maeneo yenye asili ya mafuriko au maji ya kuweza kulima mpunga n.k kwakuwa tu labda mvua kubwa hazijanyesha kwa miaka kadhaa basi tukaona sehemu hiyo itafaa ipo siku mvua zitanyesha.
2. Tuhame kwa hiari maeneo hatarishi kwa usalama wa familia zetu wakati wa mvua kubwa.
3. Tuache kuziba mifereji (hasa wakazi wa Dar es salaam).
 
Bas mi nisijenge pale....nisijeacha wanangu yatima au tukafa wote.Asante kwa kutukumbusha
 
Wito kwa wananchi:
1. Tuache kujenga kando kando ya mito, njia za maji, maeneo yenye asili ya mafuriko au maji ya kuweza kulima mpunga n.k kwakuwa tu labda mvua kubwa hazijanyesha kwa miaka kadhaa basi tukaona sehemu hiyo itafaa ipo siku mvua zitanyesha.
2. Tuhame kwa hiari maeneo hatarishi kwa usalama wa familia zetu wakati wa mvua kubwa.
3. Tuache kuziba mifereji (hasa wakazi wa Dar es salaam).
wewe wazri , lazima kuwa na enforcement machinery to effect that BUT IN A HUMANE MANNER, siyo kama mnavyowafanyia wamasai
 
Back
Top Bottom