Wizara ya Afya yatoa tahadhari kwa Wananchi kipindi cha Mvua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Ili kuepuka au kupunguza madhara ya kiafya yanayoweza kuletwa na mvua kubwa au mafuriko, Wizara ya Afya inatoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhari zifuatazo wakati wa mafuriko:

1. Watahadharishe watoto na watu wengine kukaa mbali na mitaro ya maji, nguzo za umeme, kuta za nyumba na maeneo mengine hatarishi.

2. Usiruhusu watoto kucheza ndani au karibu na maji ya mafuriko.

3. Kaa mbali na maji ya mafuriko, usijaribu kuogelea, kutembea, au kuendesha gari kwenye maji kwani ni vigumu kutambua hatari au nguvu ya maji.

4. Weka vizuia maji mfano mifuko ya mchanga kwenye ukuta wa nje wa nyumba na maeneo ya wazi ya ukuta ikiwemo kwenye milango, lakini usipange mifuko ya mchanga kwa kuegemesha katika kuta za nyumba yako.

5. Zima swichi kuu ya kuingiza umeme , ondoa vifaa vyote vilivyounganishwa kwenye soketi za umeme na tafadhali usishike vifaa vya umeme kama umelowa.

6. Epuka nyaya za umeme zilizoanguka.

7. Msaidie jirani yako kwenye dharura.

8. Fuatilia utabiri wa hali ya hewa kwa wakati na chukua tahadhari stahiki.
 
Hali ya mvua ni bandika bandua huko Moshi, Mabogini.
Jua likipata upeyo kidogo watu wanavuna na kuanika mpunga.
Ikinyesha ndio tatizo.
 
Ili kuepuka au kupunguza madhara ya kiafya yanayoweza kuletwa na mvua kubwa au mafuriko, Wizara ya Afya inatoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhari zifuatazo wakati wa mafuriko:

1. Watahadharishe watoto na watu wengine kukaa mbali na mitaro ya maji, nguzo za umeme, kuta za nyumba na maeneo mengine hatarishi.

2. Usiruhusu watoto kucheza ndani au karibu na maji ya mafuriko.

3. Kaa mbali na maji ya mafuriko, usijaribu kuogelea, kutembea, au kuendesha gari kwenye maji kwani ni vigumu kutambua hatari au nguvu ya maji.

4. Weka vizuia maji mfano mifuko ya mchanga kwenye ukuta wa nje wa nyumba na maeneo ya wazi ya ukuta ikiwemo kwenye milango, lakini usipange mifuko ya mchanga kwa kuegemesha katika kuta za nyumba yako.

5. Zima swichi kuu ya kuingiza umeme , ondoa vifaa vyote vilivyounganishwa kwenye soketi za umeme na tafadhali usishike vifaa vya umeme kama umelowa.

6. Epuka nyaya za umeme zilizoanguka.

7. Msaidie jirani yako kwenye dharura.

8. Fuatilia utabiri wa hali ya hewa kwa wakati na chukua tahadhari stahiki.
He, Wizara ya afya imehamia huko! Tanzania kuna vituko kweli.
 
Ccm wanajua kununua magari tu kila kukicha, kuboresha mazingira, miundombinu ya makazi ya WaTz kaachiwa Nani? Miaka 60 ya Uhuru, tunachoweza kufanya ni kutoa tahadhari tu?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom