A
Anonymous
Guest
Habari, tunaomba mamlaka husika zifuatilie malalamiko ya wanafunzi wanaokabiliwa na changamoto za mikopo ya elimu ya juu, hususan namna wanavyohudumiwa na maafisa mikopo (Loan Officers) wanapokwenda kuwasilisha matatizo yao.
Wanafunzi wanadai kuwa baadhi ya maafisa mikopo hawawasikilizi ipasavyo na badala yake huwapa majibu yasiyoridhisha. Wakati mwingine huambiwa kuwa muda wa kusikiliza wanafunzi umeisha, hawana suluhisho la changamoto zao au waondoke kwa kuwa wamechoka.
Aidha, wanafunzi wanalalamikia pia namna baadhi ya viongozi, wakiwemo mawaziri, wanavyojibu hoja na malalamiko yao, wakidai kuwa majibu wanayopata hayazingatii uzito wa changamoto wanazowasilisha.
Tunaomba uchunguzi ufanyike kwa kuzungumza moja kwa moja na wanafunzi wenye changamoto za mikopo, pamoja na kufuatilia mijadala katika makundi ya mitandao ya kijamii yanayohusu mikopo ya elimu ya juu, ili kubaini ukubwa wa tatizo na namna wanavyohudumiwa.
Tunaiomba Serikali kuhakikisha wanafunzi wanapewa nafasi ya kusikilizwa, wanahudumiwa kwa heshima na wanapata majibu yenye ufafanuzi pamoja na mwongozo wa kutatua changamoto zao.