nikumbusheni jina la seminari la jakaya
Samuel Luhanga
nikumbusheni jina la seminari la jakaya
Kama ni hivyo, kwa nini mtu afanye udanganyifu kwenye elimu yake ili aupate huo uwaziri.Mkulu alisema hamna chuo cha uwaziri. Kwahiyo mtu yeyote anaweza kuwa waziri!!
Shahada ya kwanza kasoma wapi huyu anti? Yaani kutoka diploma hadi Masters????? Majanga.
Umesahau kama nchi yako haithamini wasomi? hasa wasomi wa upinzani,lipumba kasaidia nchi nyingi za ukanda wa bara la africa hasa uganda ila kwa TZ hajawahi thaminiwa hata siku moja,kwa hyo alichokisem kinaukweli ndani yake
Rais wetu kwa sasa anavyeo vingi sana,maana mawaziri wengi waliopo kwenye wizara nyeti hawana utofauti na mawizi vivuli,kifupi hawana sauti,kwa sasa waziri mkuu ni yeye na waziri wa fedha ni yeye na makamu wako ndiyo hasara tupu
Shahada ya kwanza kasoma wapi huyu anti? Yaani kutoka diploma hadi Masters????? Majanga.
acha kukariri...system ya elimu nje ya nchi hilo linawezekana kabisa..tatizo lenu mmekremu mfumo wa elimu wa tanzania..muulize dr slaa atakuambia vizur maana ana phd lakin degree hana
majibu tuyapate kwa shilingi yetu kupanda sio vyetiProf LIPUMBA
View attachment 135021
Waziri wa fedha amjibu Prof. Lipumba
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha.
View attachment 135020
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.
Alisema chama chake, kina wasiwasi na elimu ya Waziri Mkuya, kutokana na wasifu wake kutoonyesha vyuo alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala ya biashara.
Alisema katika tovuti ya Bunge, wasifu wa waziri huyo umeonyesha sehemu aliyosoma elimu ya sekondari na kuhitimu kidato cha sita.
Alisema katika tovuti hiyo, haionyeshi chuo alichosoma shahada ya kwanza ya biashara, ingawa inaonyesha masomo aliyochukua jambo ambalo linatia mashaka uhalali wake kuongoza wizara hiyo nyeti.
Ukiingia kwenye tovuti ya Bunge, utaona wasifu wake kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita na shule alizosoma, lakini kuanzia elimu ya shahada imeonyesha masomo aliyochukua na kupata shahada ya kwanza ya biashara, haionyeshi vyuo, jambo ambalo linatia mashaka, alisema Lipumba.
Alisema nafasi aliyopewa inahitaji kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu, kuweza kupambanua mambo yanayohusu uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha za ndani na nje ya nchi.
Napata wasiwasi kama Rais Jakaya Kikwete, aliangalia wasifu wa waziri wake kwa sababu asingeweza kumchagua kushika nafasi kubwa kama hii, wakati vyeti vyake vina mashaka, aliongeza.
Alisema kitendo cha kumuweka mtu mwenye vyeti vya mashaka, kunaweza kusababisha nchi kuyumba kiuchumi, kuongezeka kwa deni la taifa, kwa sababu uamuzi wake unatokana na ufahamu wake.
WAZIRI AJIBU
Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.
Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza.
Alisema mbali na masomo hayo, pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009.
Nimehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland.
Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam, alisema Mkuya.
source: darnewsline.blogspot.com
Lipumba alikuwa msaidizi wa raisi mwinyi wa maswala ya uchumi na mtakumbuka inflation ilifikia ngapi. Nadhani mzee alitumaini kukumbukwa kama jamaa zake kule znz. Anahasira kweli. Tunamwelewa. Haisaidii. Akifanya nchezo mama huyu atamwadhiri kwa hoja. Ni tabia ya wasomi wengi kuringia vyeti bila ufanisi. Mbona katika mawaziri mizigo ni wasomi wazuri sana?
Kumbe na mimi naweza kuwa waziri wa fweza eee -- nina Advance diploma ya miaka ile hapa IFM - nilisoma kidato cha tano na sita ECA Ubwe Sec nikatoka na ONE KALI.
Baada ya kufanya kazi miaka 5 kama mhasibu ndipo nikafanya tena MBA university of Dar miaka 8 iliyopita - thatha mbona Mh. Rais hajaniona??? maana kwa sasa nafundisha tu Secondary ya mtu binafsi.
Vipi kuhusu John Major ambae hakuwa na qualification za elimu ya juu na kushika nafasi ya Exchequer na many senstive positions kwenye serikali ya Thatcher, mpaka kumrithi madaraka ya uongozi wa taifa.
Embu tuache ulimbukeni mnataka kufananisha mawaziri wa dunia ya kwanza na ma-governor wao (especially hawa), politician anachohitaji ni stats za ajira na mapato, uchangiaji uliopo wa mapato (kodi) na priority zipangwe vipi. Sidhani kama kwa uchumi wa africa that is very complicated kwenye siasa.
Kwanini muhimu kwa wenzetu kuwa na elimu ya kutisha (sio vyuo vya kutisha maana hiyo ni debate nyingine inayotokana na privilege na upendeleo wa hawali, kutokana na vyuo), kwenye dunia ya kwanza serikali azipewi misaada, asilimia kubwa ya hela za mikopo ni through government bonds, hizo zina impact kubwa sana jinsi interest rates zinavyozibitiwa ku entice investors. na wanunuzi wakubwa wa hizi bonds ni insurance companies or large financial institutions ambao wanatumia hela za watu, kwa maana factor kama inflation also has to considered maana mtu akikupa hela yake anataka irudi kwa faida interms of market value. Bado kuna swala kuhamasisha matumizi put it this way it is very complicated issue kwenye dunia ya kwanza na kuna mambo mengi ya consumer spendings, lobbying za interest groups all those inabidi zitungiwe sera kumnufaisha stake holder. Bado ujamaliza ideology ambazo zina ambatana na tax thinking (more taxation or less) inorder for government to meet their obligations and election promises (they too have huge impact on expenditure and investment coming in the country) it is very complicated.
Sasa hako kauchumi katanzania kanataka kweli experience a 'marvin king' yeye mwenyewe akimuona huyo mama hatoweza kumuuliza maswali magumu kwa sababu anajua changamoto hizo kwenye uchumi wetu hazipo, hivyo hizo timu za ushauri wa namna hiyo hazipo, statisticians wa namna hiyo hawapo, pressure groups wa namna hiyo hawapo, so why lazima hawe na qualifications au experience ya level yake.
Mkuu kwani employers hawafanyi background check ambayo ina-include education and employment verification? Au mtu akileta resume na vyeti basi anapewa kazi?
Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.
Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza kwa njia masafa.
pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009.
amehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland.
Kwa sasa anachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam, alisema Mkuya.